Hii kitu inashangaza sana, mtu kajenga jengo lake la kibiashara pale mbele ni eneo lake na analenga wateja wenye magari waegeshe magari ili waingie kupata huduma, halafu anatokea mtu wa jiji anaokota parking fee kwenye eneo ambalo siyo mali yake na hajawekeza chochote.
Haya tuseme wanazuia mlundikano wa magari katikati ya jiji, vipi huku mitaani hizi parking fee hadi kwenye maeneo ya strarehe kama kwenye baa wanachukua kwa lengo gani hasa........au ndo pesa zinatafutwa kwa udi na uvumba kulipa madeni.