Katika kile kinachoonekana kwamba ni kuchoshwa na Uongozi mbovu wa kiwanda cha Cocacola kwanza Limited chini ya mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho cha kutengeneza vinywaji baridi kilichoko Dar es salaam katika eneo la viwanda la mikocheni, wafanyakazi wa kiwanda hicho wameweza kuvunja ukimya na kuweka bayana kwamba hali inayoendelea Kiwandani hapo kwa sasa si nzuri na inayoweza kupelekea machafuko makubwa na hata maafa katika siku za usoni , mbali na kutishia kuweka sumu katika bidhaa zinazozalishwa na kiwanda hicho kilichojizolea sifa na heshima kubwa katika miaka ya nyuma kabla ya kukumbwa na kashfa kadhaa zilizopelekea wafanyakazi kadha na wenye uzoefu mkubwa kufukuzwa na wengine kuacha kazi kwa hiari na kwa usalama wao. Wafanyakazi hao waliendelea kusema kwamba mbali na kutojali kabisa suala la maslahi yao uongozi wa Kiwanda hicho umekuwa ukiwatendea mambo kadhaa ambayo yamekuwa yakienda kinyume kabisa na haki za binadamu kama walivyoweza kuorodhesha hapa chini:
1. Ubaguzi uliopindukia na dharau kwa wafanyakazi wazawa achilia mbali kuthaminiwa na kuwatukuza zaidi raia kutoka nje (Kuajiri zaidi raia kutoka nje katika nafasi zote za juu hiyo ikiwa ni pamoja na kuwalipa mishahara minono na gharama zinazokadiriwa kufikia zaidi Sh. Mil. 50,000,000 kwa mwezi hiyo ikiwa ni kwa raia mmoja wa kigeni, achilia mbali gharama hizo ambazo Uongozi wa kampuni hiyo tajiri umekuwa ukisingizia na kubeza kwamba umelazimika kuwaajiri wataalam hao kutoka nje kutokana na Tanzania kukosa wataalamu wanaoweza kufanya kazi hizo jambo ambalo si la kweli na hiyo inajithibitisha kutokana na ukweli kwamba pindi raia hao kutoka nje wanapoajiriwa baadae Uongozi huwashurutisha wafanyakazi ambao ni wazawa kuwafundisha kazi raia hao wa kigeni ambao idadi yao mpaka sasa ni zaidi ya 12 wakiongozwa na mkurugenzi mtendaji wa kiwanda hicho Maschela Seshibe raia kutoka afrika kusini na swahiba wake wa karibu ambaye ni mkurugenzi wa idara ya fedha Josephat Mwagi raia kutokea nchi jirani ya Kenya ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya kiunyanyasaji ikiwa ni pamoja na kuwadharau wafanyakazi wazawa na hata kuwawinda na kuwatafutia makosa hewa kuwasimamisha na hata kuwafukuzwa kazi kinyume na sheria za nchi kwa kule tu kujali maslahi yao binafsi hata kama ni yale yanayolenga katika kuisababishia kampuni hasara. Uongozi wa kibabe na maneno ya dharau yameweza kujithibitisha mara kwa mara si tu kutoka kwa mkurugenzi mtendaji pekee bali hata kwa mkurugenzi wa idara ya fedha bwana Josephat Mwagi ambaye kwa habari tulizozipata kutoka katika moja ya vyanzo vyetu vya habari aliweza kusikika akitamka waziwazi kwamba anawachukia watanzania na hawapendi wafanyakazi wa muda mrefu wa kampuni hiyo kutokana na kujifanya kwamba ni wajuaji wa kazi na hivyo kumtengenezea mazingira magumu kushindwa kutimiza nia zake zikiwamo zile za kujipatia fedha kutokana na wizi kupitia katika mtandao maalum unaotumiwa na kiwanda hicho katika kuendesha vitengo mbalimbali vya kampuni hiyo, kwa minajili hiyo mkurugenzi huyo wa Fedha alisikika wazi akitamka kwamba atafanya kila linalowezekana kuhakikisha anawafukuza kazi wafanyakazi hao na kuajiri wafanyakazi ambao watakuwa wakifanya kazi kama atakavyo yeye na sio vinginevyo, taarifa hiyo ya mkurugenzi huyo wa idara ya fedha ilifanikiwa kusambaa kwa haraka na kuweza kuwafikia wafanyaakazi wa idara hiyo ya fedha na kusababisha baadhi ya wafanyakazi wa idara hiyo kuacha kazi na wengine wakijikuta wakiziona ofisi zao kama jehanamu au jela kutokana na hali ya kutokuwa na uhakika kama wataendelea kudumu katika ajira ndani ya kampuni hiyo. Kwa ufupi baadhi ya Viongozi wa kampuni hiyo wanaotuhumiwa kuwa na tabia zinazowakashifu, kuwadharau na kuwakera wafanyakazi ukiachilia mbali mkurugenzi mtendaji na mkurugenzi wa idara ya fedha wengine ni pamoja mkurugenzi wa idara ya Ufundi na uzalishaji Louis Cortezee raia kutoka afrikaa ya kusini, pamoja na Meneja wa idara ya Ufundi na uzalishaji kanda ya Dar es salaam Ernie Van Vreden raia kutoka afrika ya kusini ambaye kwa muda mwingi imeweza kujidhihirisha wazi kwamba hakuna kazi yoyote ya kitaalam anayoifanya zaidi ya kushangaashangaa majengo ya kiwanda huku na huko kwani mara nyingi amekuwa akizurura tu kutoka katika ofisi moja kwenda ofisi nyingine kwa kile anachokizungumzia yeye kwamba watanzania ni wezi na hivyo kulazimika kuacha kazi zake zisizoeleweka na kuwafuatilia huku na huko hiyo ni licha ya kampuni hiyo kuwa chini ya ulinzi mkali wa kampuni maalumu ya ulinzi achilia mbali kamera za ulinzi zilizoko katika kila kona ya kiwanda hicho. Mwingine ambaye hawezi kusahaulika katika orodha hii ni Mkurugenzi wa idara ya masoko na maendeleo Muhabi Mahaphe raia kutoka afrika ya kusini ambaye naye amekuwa akihusishwa na tabia ya kuwadharau wafanyakazi wazawa kutokana na majibu yake ya kashfa na chuki kwa mfanyakazi yeyote wa idara yake anayeonyesha kuchapa kazi vyema kwa kile kinachoonekana kwamba ni kutojiamini katika nafasi na utendaji wake na hivyo kuhisi kwamba katika muda wowote anaweza kunyang'anywa nafasi hiyo na kupewa mtu mwingine mbaya zaidi ikiwa ni mfanyakazi wa chini yake kutoka katika idara anayoiongoza. Mwingine ambaye orodha hii haitoweza kukamilika bila kutajwa ni Sebastian Mpemba ambaye kutokana na hali mbaya iliyojitokeza kiwandani hapo habari za kuaminika zinaripoti kwamba tayari ameshamwandikia mkurugenzi mtendaji barua ya kuacha kazi, huyu ni mwajiriwa mzawa ambaye amekuwa anatumika kama kiunganishi kikuu kinachotumika katika kuwagandamiza wafanyakazi wazawa wa kampuni hiyo na anachukiwa na wafanyakazi haswa kutokana na kauli zake zinazolenga katika kuwadharau na kuwazalilisha wafanyakazi wazawa, kwa mfano usemi wake kwamba Tanzania hakuna wataalamu wenye kuweza kushika nafasi za juu katika kiwanda hicho na ndio sababu inayoipelekea kampuni hiyo kutumia gharama kubwa kuajiri wataalam kutoka nje, na alipoulizwa kuhusiana na nafasi yake ilihali yeye ni mzawa alijikanyaga na kusema kwamba imeigharimu sana kampuni hiyo na kuichukua muda mrefu kupata mtaalamu mzawa kama yeye kuweza kushika nafasi ya juu katika kampuni hiyo. Maneno kama hayo na mengineyo mengi yameelezwa kuwa ni yenye kulenga katika kuwashushia hadhi na kuwadharau wafanyakazi wazawa na hatimaye kuonekana hawajui chochote licha ya elimu na wataalam mbalimbali walizofuzu katika vyuo mbalimbali vinavyoeshimika nchini Tanzania. Kuthibitisha hilo wafanyakazi hao walisema ubaguzi unaofanywa na uongozi wa kampuni hiyo unaweza kujithibitisha vyema kwa kuangalia mfumo na mpangilio mzima wa uongozi wote wa juu umebeba raia wa aina gani na kutoka katika nchi gani.
2. Mishahara midogo isiyoendana na hadhi ya kampuni na hali ya Maisha sambamba na Kampuni kukosa mfumo maalumu wa kulipia mishahara kwa uwiano unaoendana na kazi hili ni tatizo lingine ambalo limeweza kusababisha tofauti kubwa za mishahara isiyoendana na kazi na hata kwa wafanyakazi wanaoshirikiana kiutendaji au kufanya kazi zinazofanana. Wafanyakazi hao walizidi kuweka wazi kwamba si jambo la ajabu kukuta wafanyakazi mkifanya kazi ya aina moja na wenzako licha ya kuwa na uzoefu na elimu hata kumzidi lakini ukakuta mwenzako yeye analipwa mara tatu zaidi yako na pindi utakapoamua kwenda mbele katika ngazi za juu kutafuta ufumbuzi ndipo hapo matatizo yanapojitokeza ikiwa ni pamoja na kukashifiwa kwa maneno ya dharau kwamba "ukiona hivyo utambue ya kwamba hauuziki na ndio maana unalipwa kidogo" zaidi ukiwekwa wazi kwamba kama unaona huridhiki na kile unachokipata geiti liko wazi kwako kuweza kuacha kazi. Wafanyakazi hao ambao walikuwa wakiongea kwa huzuni na masikitiko makubwa licha ya kuonekana kuwa ni wanyonge na waliokata tamaa ya kuendelea kuifanyia kazi kampuni hiyo kwa moyo walisema kwamba kumekuwepo kwa majadiliano ya muda mrefu baina ya Uongozi wa kampuni na Chama cha wafanyakazi TUICO Tawi la Cocacola kwanza ili kuweza kufikiwa kwa mkataba wa hali bora kwa wafanyakazi (Nyongeza za Mishahara na motisha nyinginezo wafanyakazi wanazostahili) lakini mpaka dakika hii Uongozi wa kampuni ya cocacola kwanza umekuwa ukileta hali ya ubabaishaji wa makusudi ili kupoteza muda hatua ambayo uongozi wa kampuni unatambua wazi kwamba itapelekea migongano na machafuko baina ya Wawakilishi wa chama cha wafanyakazi na wafanyakazi wa kawaida na hivyo maana nzima ya majadiliano ya mkataba wa hali bora kwa wafanyakazi kupotea kama ambavyo dhamira na mbinu hiyo ilivyoweza kutumika kwa miaka kadhaa sasa na Uongozi wa kampuni hiyo kufanikiwa kutowaongeza mishahara wafanyakazi wa kiwanda hicho kwa miaka kadhaa sasa. Rushwa pia ni nguzo mojawapo ambayo uongozi wa kiwanda hicho umekuwa ukiitumia kuwarubuni baadhi ya wajumbe wa chama cha wafanyakazi, kwa mfano katika miaka miwili iliyopita Uongozi wa kiwanda hicho ulifanikiwaa kutoa Rushwa kwa aliyekuwa katibu wa chama cha wafanyakazi tawi la Cocacola kwa wakati hao almaarufu kwa jina la Mushi kutoka idara ya uzalishaji ambaye baada ya wafanyakazi kugundua hali hiyo alijikuta katika wakati mgumu na hatimaye kuamua kuacha kazi, na katika awamu hii Uongozi wa kampuni ya cocacola kwanza limited umefanikiwa Kumrubuni mmoja kati ya wajumbe kutoka katika chama cha wafanyakazi aliyejulikana kwa jina la Bahati John kutoka idara ya uzalishaji ili kuweza kukwamisha harakati za chama cha wafanyakazi TUICO kupigania maslahi ya wafanyakazi. Mpaka muda ambao tunapokea habari hii habari ya kuaminika inaripoti kwamba Chama cha wafanyakazi TUICO tawi la Cocacola kwanza kwa Ushirikiano na Chama cha Wafanyakazi TUICO mkoa wa kinondoni kwa pamoja walifikia hatua ya kuvunja majadiliano ya mkataba wa hali bora kwa wafanyakazi baada ya kukubaliana kutokubaliana na Uongozi wa kiwanda hicho na hatimaye kutangaza mgogoro ambao tayari umeshafikishwa katika mahakama ya kazi (CMA) na tayari kesi hiyo ilishatangazwa kuanza kusikilizwa tangu tarehe 29.08.2011. Katika hayo yote kikubwa kinachoonekana kuendelea katika kampuni ya Cocacola kwanza limited ni Ubaguzi wa kimaslahi baina ya wafanyakazi Fulani na Fulani na sio kitu kingine na ndio maana kwa miaka kadhaa ya hivi karibuni kampuni hiyo nzuri kwa nje lakini mbaya kwa ndani imekuwa ikijitahidi kwa kila hali kuficha uozo wake kwa kuwalipa mishahara minono na kuwatumia visivyo viongozi wa nafasi za kati na zile za chini katika kuwashurutisha na kuwatesa wafanyakazi wa kawaida na hatimaye kuwatengenezea mazingira magumu wafanyakazi hao kwa falsafa ya kutofanikiwa ili waendelee kuitumikia kampuni hiyo katika muda wote wa mikataba yao ya kudumu.
3. Matumizi mabaya ya bidhaa zilizopitwa muda wake kwa walaji: Tabia ya Uongozi wa kiwanda hicho kutoa motisha ya bidhaa wanazozizalisha kwa wafanyakazi wake na hata raia wa maeneo ya jirani kuweza kutumia vinywaji ambavyo wanajua moja kwa moja kwamba vimepita muda wake wa kutumika na hivyo kuhatarisha afya na hata uhai wa walaji.
4. Kampuni kukosa mfumo rahisi wa malipo ya gharama mbalimbali inazokuwa ikidaiwa na mashirika ya nje na hivyo kusababisha usumbufu na lawama kwa wahusika wanaokuwa wakidai malipo mbalimbali kutokana na huduma au vipuri mbalimbali wanavyokuwa wameiuzia kampuni hiyo inayojitaja na kujitambulisha kwamba ni ya kimataifa ilihali mwenendo wake haulingani kabisa na hadhi ya kimataifa.
5. Ubaguzi na Unyanyaswaji wa makusudi wanaofanyiwa Viongozi wa chama cha wafanyakazi TUICO Tawi la Cocacola kwanza na Uongozi wa kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na kuwawinda na kuwatafutia visingizio na makosa mbalimbali yasiyo na mashiko kuwasimamisha na hatimaye wawafukuze kazi na hivyo kufanikisha malengo yao ya kudhorotesha harakati za chama hicho katika kupigania haki na maslahi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo. Mpaka muda ambao tumezungumza na wafanyakazi kutoka katika idara tofauti tofauti za kiwanda hicho ili kuweza kupata taarifa sahihi na za kina wafanyakazi hao wa Cocacola kwanza ambao ni Jimka Ally kutoka idara ya mauzo, Salvatory Mkami (Mwanaharakati) kutoka idara ya uzalishaji na mitambo na Omary Mohamed kutoka idara ya Mauzo, Charles Adriano kutoka idara ya uzalishaji, wameshasimamishwa kazi na kama bado watakuwa hawajafukuzwa basi wako mbioni kufukuzwa kazi kwa visingizio kadhaa vya uonevu vinavyochochewa zaidi na mkurugenzi wa kampuni kiyo Maschela Seshibe kuwapinga vikali na kuapa kwamba kwa njia yoyote ile atafanya kila awezavyo na kwa gharama yoyote kuhakikisha wamba anawafukuza kazi viongozi hao wa chama cha wafanyakazi TUICO kutokana na kuonekana kwao kwamba wamekuwa katika mstari wa mbele katika kutetea maslahi ya wafanyakazi na kupinga vikali ufujaji wa fedha za kampuni hiyo unaofanywa kwa makusudi na Mkurugenzi huyo na timu yake katika kiwanda hicho kwa kule kujali maslahi binafsi haswa mengi yanayolenga katika kuisababishia hasara kampuni na kuwafanya Wafanyakazi kuhudhunishwa na hali nzima Utawala inayoendelea kukitafuna kama sio kukiua kiwanda hicho. Kwa kuzidi kuonyesha wazi ni kwa jinsi gani Uongozi huo wa juu wa Kiwanda hicho cha Cocacola kwanza limited unavyowaandama Kuwabagua na Kuwapiga vita wafanyakazi wazawa haukuishia hapo bali uliweza kuwasimamisha kazi kwa hila baadhi ya Viongozi katika Idara mbalimbali akiwemo bwana Valence Pantaleo Kutoka idara ya fedha, Paul Andrea kutoka idara ya Rasilimali watu (HR) Salum Ngururu kutoka katika Idara ya Mauzo, Gerald mushi kutoka Idara ya Rasilimali watu, Joel Njama Kutoka katika idara ya mauzo achilia mbali Wafanyakazi wengine 12 kutoka katika idara hiyohiyo ya mauzo, wafanyakazi hao walizidi kuripoti kwamba wapo wafanyakazi wengine waliosimamishwa na kufukuzwa kazi kwa hila lakini tulipowadadisi zaidi wafanyakazi hao walishindwa kutupa uthibitisho wa kutosha na hivyo kutulazimu kutowataja kwa kuogopa kuupotosha umma kwa kuandika habari ambazo hazitokuwa na usahihi. Kwa ujumla wafanyakazi wa kiwanda hicho wameeleza kwamba hali kiwandani hapo sio shwari kabisa ingawa Uongozi wa kiwanda hicho unajitahidi kwa gharama kubwa kuficha na kutumia kila namna kuonyesha kwamba hali ni shwari.
Zaidi ya hayo wafanyakazi hao waliweza kutupatia Email ya Mwenyekiti na mmiliki wa Kampuni hiyo raia wa Afrika ya Kusini Bwn. Philliph Gutsche ambayo ni
gutschep@cocacolasabco.co.za ili kwa muda na wakati wetu tuweze kuwasiliana nae na kuhoji kulikoni kwa uamuzi wake wa kukabidhi kampuni hiyo mikononi mwa watu wanaolenga katika kumuua kibiashara. Mbali na taarifa hiyo wafanyakazi hao walionya kwamba iwapo Wafanyakazi wenzao hawatorudishwa kazini katika muda muafaka kwa misingi ya haki na kutofuatwafuatwa na Uongozi wa kampuni hiyo hatua watakayoichukua itakigharimu sana kiwanda hicho.