Club ya muziki ya Wadutya imekithiri kwa matukio ya ubakaji

Usalama wa mtu unaanzia kwake lakini haimaanishi kua tusitoe msaada kwa mtu wa pembeni, wadau mnauliza kwanini mleta uzi hakuingilia, kuingilia kungemaanisha kubishana na watu saba (kama anavyodai ingawa sielewi walipandaje pikipiki) wenye nia ovu.

Ingawa sioni sababu ya kutokwenda kuripoti polisi tukio zima, na pia unataka kusema hiyo klabu haina mabaunsa? Kama hawapo hapo Wadutya ugomvi ukianza nani hua anatuliza?
Anayetuliza ugomvi aulizwe ilikuaje akashindwa kuzuia tukio au kufanya observe and report.

Pole sana mkuu, napata picha mtu unapotamani kutoa msaada lakini hauwezi kuutoa kutokana na mazingira jinsi unavyojisikia.

Angalau tutafute na tumiliki bunduki, tutasaidia wengi sana.
Heri yako kiongozi umetumia hisia halisi na busara kutoa hoja yenye msingi na nguvu,
Kiongozi labda nianze kwa kukujulisha kuwa wadutya hapo zamani ilikuwa na mabaunsa kipindi hicho pesa ilikuwepo na watu walikuwepo hivyo ilisaidia kufanya uendeshaji wa club hii kuwa bora lakini tangu mh magu atinge madarakani kituo cha polisi kikapiga marufuku ukumbi wowote wa starehe kupiga muziki mpaka saa 11 alfajiri hapo ndo ugumu wa biashara ukaanza kuonekana hao mabaunsa wakaacha kazi na idadi ya wateja ikaporomoka sana na ukizingatia kupunguzwa kwa muda wa kufanya kazi ndo kukapoteza kabisa wateja na hivi juzi tu ijumaa usiku zilichapwa ngumi za hatari na atakaepigwa ndio anasalenda na ugomvi unaishia hapo ,

Mkuu hata kama yule dada alikuwa ni kahaba vipi ila kwa jinsi alivyobebwa inatia huruma sana aisee,

Laiti ningekuwa na chombo cha moto ningelimsaidia aisee.
 
Mwaka 2009 nilikuwa hapo ushirombo. Nikalal na nilihudhuria huo ukumbi siku ya jmos kwa lengo la kujiburudisha wakati wa usiku.

Sasa basi katika pita pita kuchek maua ya upendo,ndio baadhi ya wenyeji wakaniambia(ukipata mwanamke hapo nje ama eneo jingine na hapa,basi usimlete humu ndani acheze mziki,maana utapokonywa na ataxhukuliwa kwa nguvu na wenye nguvu)

Kwa kuwa sikuwa na lengo la kuwa na mwanamke siku hyo,basi nikagaili kuendelea kutafuta kiburudisho cha kucheza nacho mziki na nikaishia kutazama wasukuma wanavyosakata lumba wakiwa na nguo zao za kazini(yaan nguo walizoshindanazo siku nzima kwenye mishe mishe za viwandan ama shambani)

Kwa maana hyo mtoa post anaweza kuwa sahihi kwa hali ya kiusalama ya hapo Ushilombo,hasa kwenye huo ukumbi wa Badyuta.
Mkuu afadhali ni kipindi hicho lakini sasa hivi hakuna cha usalama wala nini yaani hakuna walinzi ,hakuna msaada wowote wa polisi ni wewe mwenyewe kujilinda na kujiepusha kutokuhudhuria eneo la wadutya haswa kama ni mwanamke yaani hakuna usalama kiujumla.
 
kuna watu wanajaribu kujustify hii ishu!! kazi sana kuishi nchi yenye wajinga wengi kama TZ.
 
Mkuu afadhali ni kipindi hicho lakini sasa hivi hakuna cha usalama wala nini yaani hakuna walinzi ,hakuna msaada wowote wa polisi ni wewe mwenyewe kujilinda na kujiepusha kutokuhudhuria eneo la wadutya haswa kama ni mwanamke yaani hakuna usalama kiujumla.

Kwani idadi kubwa ya wanaume wa Ushirombo ni vibaka?
Kwa nini mnakuwa kama wanaume
wa Dar es salaam?
Chukueni hatua stahiki,kulalamika haitasaidia kitu.
 
Katika mji wa USHIROMBO club ya muziki inayotesa na kutamba inaitwa WADUTYA CLUB iliyo mjini karibu na stand kuu ya mabasi hapa USHIROMBO,

Ratiba za club hii kama nijuavyo IJUMAA zinapigwa nyimbo za kale maarufu kama BAKURUTU maalumu kwa wazee na siku ya JUMAMOSI ni siku ya DISCO maalumu kwa vijana,

Leo Ile kufika mida ya saa 4:37 usiku nilikuwa nimeshafika wadutya.
Nikamkuta mdada mmoja amebeba mfuko uliokuwa una chipsi mayai huku akiwa na fanta orange ya take away,Huku kichwani pombe zikiwa zimemkolea nikamtania kuwa naomba chipsi nile akakubali nikawa kama namsifia kuwa ana roho nzuri akawa anacheka cheka tu maskini wa Mungu , kisha akaingia ndani ya ukumbi ,

Punde si punde vijana waliokuwa kwenye boda boda kama 5 hivi wakaanza kumiminika muda sio mrefu wakaingia ukumbini wakamtandika binti wa watu makofi kisha wakamtoa nje kwa nguvu huku binti akiwa analia kwa uchungu wakampakia kwenye pikipiki wakatokomea nae kwenda KUMBAKA ,

Aisee inasikitisha sana naomba serikali na jeshi la polisi hapa ushirombo muifungie club ya wadutya jumla kutokana na mambo yanayotendeka ya ubakaji tena hadharani binafsi nimechukizwa sana na hili jambo na kwa kweli upuuzi walioufanya hao vijana utawagharimu maisha yao yote,

Binafsi nimekereka vilivyo na sitaki kuamini kuwa jeshi la polisi halijui yanayotendeka kwa kuwa rekodi na matukio kama haya wanajua yanatokea sijui kusudi lao ni lipi , ama kweli tunapoelekea Shetani mwenyewe anajua.
Sasa wao walimpiga makofi then wakatokomea nae, wewe ulijuaje kama wameenda kumbaka??
Acha fikra mgando mkuu
 
Mtoto anakuchekea chekea wewe uka zubaa tu badala ya kula mzigo. Hadi wenzako wakaja na bodaboda kubeba mtoto na kwenda kula mzigo, usilalamike sana ndo maisha... let it go!!
Mkuu tambua sikuwa na nia ya kufanya nae ngono .
 
Back
Top Bottom