Dola Iddy Wa Chelsea
JF-Expert Member
- Sep 26, 2014
- 2,120
- 1,510
Katika mji wa USHIROMBO club ya muziki inayotesa na kutamba inaitwa WADUTYA CLUB iliyo mjini karibu na stand kuu ya mabasi hapa USHIROMBO,
Ratiba za club hii kama nijuavyo IJUMAA zinapigwa nyimbo za kale maarufu kama BAKURUTU maalumu kwa wazee na siku ya JUMAMOSI ni siku ya DISCO maalumu kwa vijana,
Leo Ile kufika mida ya saa 4:37 usiku nilikuwa nimeshafika wadutya.
Nikamkuta mdada mmoja amebeba mfuko uliokuwa una chipsi mayai huku akiwa na fanta orange ya take away,Huku kichwani pombe zikiwa zimemkolea nikamtania kuwa naomba chipsi nile akakubali nikawa kama namsifia kuwa ana roho nzuri akawa anacheka cheka tu maskini wa Mungu , kisha akaingia ndani ya ukumbi ,
Punde si punde vijana waliokuwa kwenye boda boda kama 5 hivi wakaanza kumiminika muda sio mrefu wakaingia ukumbini wakamtandika binti wa watu makofi kisha wakamtoa nje kwa nguvu huku binti akiwa analia kwa uchungu wakampakia kwenye pikipiki wakatokomea nae kwenda KUMBAKA ,
Aisee inasikitisha sana naomba serikali na jeshi la polisi hapa ushirombo muifungie club ya wadutya jumla kutokana na mambo yanayotendeka ya ubakaji tena hadharani binafsi nimechukizwa sana na hili jambo na kwa kweli upuuzi walioufanya hao vijana utawagharimu maisha yao yote,
Binafsi nimekereka vilivyo na sitaki kuamini kuwa jeshi la polisi halijui yanayotendeka kwa kuwa rekodi na matukio kama haya wanajua yanatokea sijui kusudi lao ni lipi , ama kweli tunapoelekea Shetani mwenyewe anajua.