Club Ambiance ( Corner bar) yafungwa rasmi Kinondoni

Ikiwa ni kwa kosa la kupiga muziki kwa sauti ya juu ni kweli kabisa hapo kuna kosa la kurekebisha tu ambapo mmiliki anatakiwa muziki aweke ndani aweke na sound proof kutokusumbua wananzengo.

Ila swala la machangudoa, pengine lihusishwe tu na hayo mengine ila sio jambo la msingi kwa mtu mzima sababu hao mademu, wao wapo kwa kila namna. Hiyo ni kazi ya maaskari kuwatokomeza ila kuna siku nilisikia hao machangu wanasema wao wenyewe kuwa, katika kamata kamata ile, maaskari wenyewe huwa wanawaomba pesa ili wasiwapeleke Mabatini, wakikosa pesa wana wagonga kufidia.
 
Lazima mmkumbuke mzee Lowassa. Namba Za kichina Lazima msome. Nampongeza mkuu wa nchi kwa kunyoosha watu... Tuendelee mpaka 2025
 
Hao wahudumu wapatiwe ajira ni Huyo mkuuu au familia zao zitaishi vipi sasa?
 
Serikali ya kukurupuka....sasa wamemfungia huyo basi kinadada poa watahamia kangaroo, hongera, b-bar au igo then tutaona kama hao nao watafungiwa.

Imagine wale wenye majiko wote pale leo hii hawana ajira na wanategemewa lakini mjinga aliyetoa amri yupo anazunguka kwenye landcruiser V8 na analindwa. Nahisi wateule wa mfalme wanamzunguka ili mfalme azidi kuchukiwa
 
Huu utawala wa ajabu kuwahi kutokea, fikiria ni ajira ngapi zimepotea. Kila mtu anatafuta misifa ya kijinga. Hii ni vita dhidi ya watu wa kaskazini
Hiki kichefuchefu sasa hapa mambo ya kaskazini yanaingiaje? Kwani hujui sheria inayozuia ukahaba au ku-facilitate ukahaba? Kwanini usimwambie mbunge wako aende bungeni kupeleka hoja ya kufuta sheria inayozuia biashara ya ukahaba badala ya kulilia ukanda kwa sheria ambayo ipo miaka zaidi ya 30 ila ilikuwa haijapata wa kuisimamia sawa sawa?
 
Du ofisi zimefungwa, mjini panazidi kuwa pagumu.
Ingawa serikali itakosa mapato na watu kupoteza ajira,lakini hawafuati sheria na kuharibu maadili.Kama unaishi karibu na familia yako ndio kero utajua uchungu wake.Hapa sheria zilizopo zinasimamiwa,sio kama zimetungwa jana au juzi,zilikuwepo.Wakichukia watu wawili kwa sheria kuchukua mkondo wake,mara mbili yake wanafurahi zaidi.
Na hapa isiwe mwisho,sheria ifanye kazi kwa baadhi ya makanisa yasiyofuata sheria kwa kuweka spika kubwa na kusali kwa kelele kubwa iwe usiku iwe mchana bila kujali haki za wengine,tena kwenye makazi ya RAIA wakati sheria mara nyingine haziruhusu hivyo.Kuna watoto,wagonjwa na waliochoka na kazi zakutwa wanashindwa kupata utulivu wa kupumzika.
Na hili lisiwe Dar tu,iwe nchi nzima ili kujenga utawala wa sheria.
 
Na misikiti nayo utawaambia watoe spika?
Au double standard?
 
Back
Top Bottom