Club Ambiance ( Corner bar) yafungwa rasmi Kinondoni

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
CLUB AMBIANCE ( CORNER BAR) YAFUNGWA RASMI KINONDONI

Club maarufu ya KONA Bar imefungwa rasmi leo na maafisa biashara na mazingira wa manispaa ya Kinondoni kufuatia agizo la Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi baada ya kupokea malalamiko ya wananchi juu ya baa hiyo kuwa sugu kwa upigaji wa muziki na kuwa kijiwe cha makahaba na hivyo kukiuka sheria za mazingira na masharti ya leseni yake ya biashara.
Maafisa biashara wa Kinondoni walidai mbele ya DC Hapi kuwa mmiliki wa Bar hiyo maarufu amekwishapewa onyo na kupigwa faini mara kadhaa.

Club hiyo ambayo ni maarufu kwa biashara ya kina dada wanaojiuza maarufu kama "dada poa" imefungiwa kwa muda usiojulikana na mmiliki wake kutakiwa kujisalimisha manispaa ya Kinondoni.
DC Hapi aliagiza bar na kumbi zote zinazofuga na kuruhusu biashara hiyo haramu kufanyika katika maeneo yao kuanzia sasa zianze kuwa zinachukuliwa hatua
[HASHTAG]#KinondoniYetuFahariYetu[/HASHTAG]
[HASHTAG]#TunaletaMaendeleo[/HASHTAG]
[HASHTAG]#TunasikilizaTunatatua[/HASHTAG] .
1488135527760.jpg
 
Tatizo watawala wa serikali ya Leo mmmmh sidhani kama wanafanya tathimini yakinifu kabla ya kufanya jambo maana kila kona mtu anajitamukia tu.., labda ndio uwoga maana njaa mbaya.h
Wao wanaona sawa tu

Ova
 
Siungi mkono shughuli zilizokuwa zikifanyika ndani ya baa hiyo...hata ivyo hii inawezafanyika Tanzania tu, yaani hii nchi ukifanya biashara kuna sheria lukuki zinazoongoza uanzishaji wa biashara, lakini pia kuna mamlaka kibao zinazoweza zikaamua biashara yako iwepo au isiwepo...mfano, TRA, TFDA, Manispaa, nk..na sasa ameibuka mamlaka nyingine wakuu wa mikoa, walaya, wenyeviti wa CCM, madiwani, nk..Only in Tanzania.
 
Njooni Kimara 5N nako ni kero.
In fact Mbezi kuna mauzio ya miili sehemu nyingi sana
 
Kuna watu huwa unasikia amepotea duniani unafurahi maana wanayotendea wenzao kama vile waliubwa na almasi
 
Back
Top Bottom