CLOUDS MLIJITAKIA MSIMLAUMU YEYOTE.

Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
11,541
12,401
Wana bodi habari Leo,
Ukisikiliza na kufuatilia yanayo-trend kwa issue ya Clouds Media kuvamiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam akiwa na wanausalama wasiopungua sita ni dhahiri utagundua yafuatayo;

1. Wafanyakazi wa Clouds Soudy brown, Qwessy ambao ni presenters wa kipindi cha SHILAWADU na chris kama Producer walishirikia na pengine walilipwa ili kutengeneza video ile, kwa kufanya hivyo walikuwa intentionally na Sound minded na hivyo walikusudia kurusha kipindi kile kama walikuwa hawako tayari kurusha kipindi kile hawakupaswa hata kushiriki hata kutengeneza video hiyo. Kwa sababu walikubali matakwa ya RC Makonda wasilmaumu mtu walijitakia

2. Ruge anakili ndiye aliyetoa kauli ya mwisho kuwa kipindi kisurushwe, kwa nini asingewasiliana na RC Makonda kumweleza uamuzi huo ili akae akijua kuwa kumetokea tofauti na kile alichoahidiwa na akina Soud Brown. Communication is the Two way Traffic, alipaswa kumjulisha upande wa pili ili ategemee tofauti na tarajio lake. Ruge kwa kufanya hivyo ni kujitakia asmlaumu yeyote.

3. Mbaya kabisa mazoea aliyoyaweka kwa RC Makonda ndiyo yaliyomu-encourage RC huyo kwenda bila woga na akasahau kuwa ile ni kazi na badala yake RC makonda akaegemea kwenye mazoea na urafiki badala ya kufuata taratibu. Ikumbukwe kuwa Moja ya tukio siku ya RC makonda kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa alimwagiwa maji pale jambo ambalo linaonesha mazoea kupita kiasi….Mazoea haya yalijengwa na nini wenyewe Clouds Media msimlaumu yeyote kuzoea zoea watu mwishowe mtazoea majini!


4. Clouds media wa Uzandiki na unafiki wenu mlishindwa kusimamia ukweli, Kama mlimpenda sana kwa nini mlishindwa kuzungumzia suala la vyeti vya huyu mtu hata kwa kutaka aseme chochote kuhusiana na yasemwayo, au ninyi wenzetu news tip mnataka mtoe wapi zaidi kwa haya mnayoyasikia. Nina uhakika mngejaribu kumwuliza angejua msimamo wenu juu ya kusimamia ukweli sasa mlivyookaa kimya akajenga trust na kuamini ninyi mpo upande wake (na ndo ukweli) kwa kufanya hivyo mlimjenga Kisaikolojia kuwa ninyi ni mpo upande wake ….msimlaumu mtu mazoea mliyoyajenga ndiyo yaliyowafikisha hapo.




HITIMISHO:

1. Dunia ina ups and down,

Ups inasaidi kutu encourage na kutupa confidence kuendelea kufanya mazuri zaidi.

Down inatupa somo kujirekebisha tulipokosea, Ni muda sasa wa kujirekebisha pale mlipokosea, mwache kuzoea watu eti kwa ajili ya opportunities, najua mlijipendekeza kwa RC makonda mkiamini kuwa hiyo ni Opportunity kwenu hasa kibiashara.


2. Opportunists itawa cost sana kama hamtajirekebisha

Wengine mjifunze kuwa mnatakiwa kufanya kazi kwa sheria na taratibu, kujipendekeza ipo siku yatawakuta ya Clouds (GSM hii inawahusu)


Nawasilisha
 
Hebu ishi maisha yako ndugu achana na mambo ya watu - Haki, haki ukiulizwa tafsiri halisi ya HAKI Unaijua
 
wewe unaakili kipande aisee, Ruge angewasiliana vipi na makonda wakati makonda hakumtaarifu kabla (two way traffic). mbili unaevidence ipi kuwa walipewa hela na huyu bashite, tatu..kuzoeana sio dhambi, nne...sioni logic ya ulichokiandika (toa matapu tapu yako)..tano. kulikuwa na sababu gani ya kwenda na wale mgambo pale..sita..ongeza uwezo wako wa kufikiri.
 
wewe unaakili kipande aisee, Ruge angewasiliana vipi na makonda wakati makonda hakumtaarifu kabla (two way traffic). mbili unaevidence ipi kuwa walipewa hela na huyu bashite, tatu..kuzoeana sio dhambi, nne...sioni logic ya ulichokiandika (toa matapu tapu yako)..tano. kulikuwa na sababu gani ya kwenda na wale mgambo pale..sita..ongeza uwezo wako wa kufikiri.

athari za kumbeba beba ndo hizo......opportunist ina-cost sometime jifunze pia!
 
Back
Top Bottom