Kinachowamaliza watanzania wengi ni ile hali au tabia ya kutopenda kutenda haki ila ni watu wakupenda tu wao watendewe haki.
Watanzania wengi ni madhulumati, wamejawa na chuki, hila yani mitabia mibaya mibaya mingi sana.
Hivyo sababu hizo hapo zinafanya kuwaondoa kwenye ile 'moral authority' ya kukemea, kulaani, kukosoa na kupinga ubaya na udhalimu unaofanywa hata na watawala pia achilia mbali raia wa kawaida anapokosea.
Unawezaje kunikosoa mimi kwa uovu ninaofanya hali hata wewe mwenyewe unafanya?
Mtanzania hata yule raia tu wa kawaida ni ile tu amekosa mamlaka/power ila akipata utaona mabaya anayoyafanya, na ukitaka kujua tabia za hovyo za watz wengi we fatilia tu maisha halisi wanayoishi utajua haya nayoeleza.
UKISHACHAFUKA NENDA KWANZA KAJISAFISHE UWE MSAFI NA HAPO UTAWEZA KUWASAFISHA WENGINE WALOCHAFUKA.