Clouds media group na mfumo wa ubepari unavyowanufaisha

Mpogolo wa mahenge

New Member
Mar 11, 2016
3
2
Kwanza niwapongeze familia nzima ya clouds media group wakiongozwa na viongozi wao(RUGE&KUSAGA)kwa kazi nzuri ya kuhabarisha umma.Asilimia kubwa ya watanzania wanawafuatilia vipindi vyenu nimekuwa mdau wenu kwa muda mrefu tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000 hadi sasa.
Kitu nilichojifunza kutoka kwenu kuwa mnaweza kutumia fulsa zinazokuwa mbele yenu na zikawapatia faida kubwa na kuvipaisha vituo vyenu na kuwa na wafuatiliaji wengi ukilinganisha na vituo vikinge(Hongereni sana kwa ubunifu).Nikiutazama mfumo wa ubepari kwenye stage zote 3(merchantilism,Industrialization and monopoly).
Hasa nikiangalia stage ya kwanza(mercantilism)inayosema"to use any means to accumulate capital"kwa wanaofahamu wanaelewa namaanisha nn hapo,nikioanisha hiyo stage na clouds wanavyoitumia(kwa uzuri hawavunji sheria)kujinufaisha na kuongeza idadi kubwa ya wafuatiliaji wa vipindi vyao na matangazo ya biashara.Kuna vitu vingi ambavyo huvitumia kwa jamii huonekana vya kawaida ila wao ndio fulsa ya kujipatia capital.
Kuna kitu walikifanya ambacho vituo vingine vilikuwa vimeshafanya yaan suala la clouds tv kuonekana DSTV,suala hilo chanel ten walikuwepo muda mrefu ila clouds walivyofanikiwa kuwepo huko walivyolitangaza utazan wao ndio wa kwanza kuwepo kule hadi ufunguzi ulifanyika pale escap na wakaingiza hela ya kutosha tu,kwa tukio hili tu limewaongezea sana matangazo mengi ya kibiashara.
Sasa leo hili tukio la Rais magufuli kupiga simu kwenye kipindi cha clouds 360,hii lazima waitumie kama fulsa na hapo watajibrand vilivyo na matangazo lazima yaongezeke.
MYTAKE,Fulsa zipo nyingi sana ila tunashindwa kuzitumia,ww unaweza ukaona ujinga wenzako huo ujinga wanautumia kama fulsa na kujipatia fedha nyingi.Hongereni sana clouds media group kwa kazi nzuri mnayofanya.
 
Clouds wapo vizuri katika kujiuza. Madisco yote ambayo yanamilikiwa na Clouds yanajaza sana watu, kwa sababu ya umuhimu wa matangazo, wapo vizuri sana kwenye marketing. Joseph alianza shughuli za u-dj zamani, alijua alikuwa anatafuta nini, wakati wengine wakizama kwenye ulevi na matanuzi yeye alikuwa anajipanga atoke vipi maishani. Wale wengi wa umri wake waliokuwa wanakunywa sana pombe na kuserebuka na warembo kwenye stage wakati yeye akihangaika na nyimbo kwenye ile sehemu ya kupigia muziki, wameondoka duniani mapema yeye bado anadunda na anafanya makubwa.
Jambo jema sio kuwaanzishia bifu Clouds bali ni kuwatumia kama changamoto ya kufanya vizuri maishani. Wanao udhaifu mwingi tu lakini siku zote wanajitahidi kufanya kitu fulani katika mtindo tofauti na wengine.
 
Ujanja ujanjani, hawa wanatukuzwa kwa sababu ya kuibebea ccm wakati wa uchaguzi, kituo hiki ni mahakama ya maendeleo ya vijana
 
Wameshaanza kuwalipa wasanii mirabaha!? maana wao ndio Wa kwanza kuwaambia wasanii saini hapa kuwa umekubali nyimbo zako zipigwe bure kwamba usiwadai chochote. Hutaki sahau kusikika.
 
Hivi amesifia radio station au TV? .....au zote? Nadhani wa Tz tuna tatizo kwenye kusikiliza na kuwakilisha ulichokisikia! .......Juzi JPM ameongea power za RC kuwaweka ndani watumishi ambao watawasumbua....nashangaa media imesema ni wacheza pool: kwa wachez pool amesema wapelekwe kwenye makambi wakalime sio wakamatwe masaa 48:
 
Back
Top Bottom