four eyes
JF-Expert Member
- Jan 11, 2017
- 905
- 1,406
Kama ni mtazamaji au msikilizaji wa clouds fm na clouds tv utakuwa umeshaona kampeni mbalimbali ambazo hawa jamaa huzianzisha,kuzipigia debe sana mpaka zinaingia vichwani mwa watu ktk jamii.
Iwe ni kampeni za fursa,au kuchagiza hali ya kujitambua,au za burudani na show zao,vituo hivi hupiga kampeni hizi Kwa msisitizo na ubobevu mkubwa mpaka zinapata mafanikio wanayohitaji kupitia kampeni hizo.
Licha ya wakati mwingine mimi binafsi kukerwa na msisitizo uliopitiliza wa kampeni zao Kwa kuzizungumzia mara Kwa mara lakini najikuta pia nikiwapa heko Kwa ubobevu wao katika taaluma yao na uwezo wao wa ushawishi katika jamii kupitia vyombo vyao hvyo.
Hili linanifanya niamini kwamba hata mafanikio waliyonayo mpaka kupigiwa simu mara Kwa mara na mheshimiwa rais hayaji Kwa bahati mbaya ila ni Kwa stratergy na umahili mkubwa wa kina ruge na think tank wengine wa ndani ya kampuni hiyo ya media.
Pamoja na mapungufu yao yanayozungumzwa sana na wasanii na wasikilizaji ikiwemo matangazo ya biashara kuwa mengi mno,no baadhi ya wasanii wasiotaka kufuata wanachotaka kubaniwa,bado nawapa heko Kwa umahili wao mkubwa uliowezesha kuvifunika Kwa umaarufu vituo walivyovikuta siku nyingi kama radio one,ITV nk.
Kutokana na hayo nawapa heko mastrategist wa clouds media,wako vizuri.naomba kuwasilisha