Clouds kwa hili la Clouds Plus mmezidi!

Clouds kwa hili la Clouds Plus mmezidi!

Egwugu

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2011
Posts
17,558
Reaction score
8,551
Ni ajabu wewe kila kitu unatafuta jinsi ya kuteka pesa iwe kiharali ama kwa mizengwe. Sie watumiaji wa Azam TV tuna vifurushi vyetu 3 ambavyo kwa idadi ya chaneli zote zilizopo zitapatikana pale utakapoweza kulipia kile cha juu kabisa. Sasa sijui huu ndo utaratibu gani kwamba unaamua kachaneli kako ka clouds plus basi wewe unaingia na kifurushi chako cha kipekee kabisa na unahitaji 3000.

Kwamba naweza nikalipia kifurushi cha juu kabisa na nikapata zote ziwe za ndani ama nje, michezo ama habari, vichekesho ama burudani na ntazipata zote isipokuwa ile ya kwako ya Clouds Plus. Hii ni hatari, inaonesha ni kwa kiasi gani wewe ni wa kipekee lakini pia labda chaneli yako ni ya kipekee na nzito kupita zote katika dekoda nzima ya Azam TV .

Najiuliza tu, ikiwa na Azam angesema sie wanamichezo tunatakiwa kulipia labda 5000 kwa ajiri ya chaneli ya Azam sports2 na labda ikasemwa pia kwa sie wafatiliaji wa muvi za Nigeria tukaambiwa tulipie 3000 ili kuiona Chaneli ya AMC sielewi kama leo watizamaji tungeweza kweli kugharamia dekoda kama dekoda na bado tukaweza kumudu kulipia kila chaneli kwa pesa yake. Tunamshukuru sana Bakhresa kwa hili ijapo bado wengi wetu tunajiuliza ni nini haswa nia ya Ruge na Clouds Plus yake.

Kama ni njaa ya pesa basi hii itakuwa ni hatari sana. Tunaelewa umetoka kuchukua viingilio vya ndondo, sahivi unajiandaa kupiga za Fiesta na bado inakuingia akilini kuchajisha bei yako kwa ajiri ya chaneli yako tukufu. Huu kama siyo kukosa utu na aibu basi itakuwa ni tamaa kali sana. Ingekuwa ndo mwendo kwamba tulipie kila kitu kwa kitu sijui kama kweli tungefika, haya bwana.
 
Mkuu aisee hata me nimeshangaa jaman ndio hivyo tunaopenda ile channel inabidi tujiunge tu kwa shingo upande ila hawatutendei hakiii kabisaa
Wajinga ndiyo waliwao na kazi ya mjinga ni kuumia..!
 
Pesa zinamfuata mwenye pesa...
Ukikosa idea ya kuzalisha pesa usimulaumu mwinzio kumbuka yule ndio mzee wa kufungua fursa!!!

Ukweli mchungu!
Ingekuwa ndo hivyo hata Mengi na Bakhresa pia kwasababu hata wao wana pesa na bado zinawafata wangesema hata zao tuzilipie moja moja. Lakini naona Azam Sports2, Azam Sports HD, AMC, ITV n.k zote si bure ila ni katika vifurushi vyetu vya kawaida ila kwa Ruge hii ni hatari sana. Tamaa mbaya sana hii ama labda kafikiri huku Azam kuna wajinga kama anavyofanya huko kwingine na THT anavyowapiga. Huku kaula wa chuya
 
Jamaa anajua kucheza na akili za watu..achana name hilo.hebu fikiria kaja na tatu mzuka..yote hiyo ni kutengeneza mifereji ya pesa..ila uzuri ni kwamba hulazimishwi..uamuzi ni wako.
 
Ingekuwa ndo hivyo hata Mengi na Bakhresa pia kwasababu hata wao wana pesa na bado zinawafata wangesema hata zao tuzilipie moja moja. Lakini naona Azam Sports2, Azam Sports HD, AMC, ITV n.k zote si bure ila ni katika vifurushi vyetu vya kawaida ila kwa Ruge hii ni hatari sana. Tamaa mbaya sana hii ama labda kafikiri huku Azam kuna wajinga kama anavyofanya huko kwingine na THT anavyowapiga. Huku kaula wa chuya
Acha kulalama....hiyo ni add-on channel, lipa hela uione....
Azam wanazo add ons nyingi za kihindi...not a new phenomenon...
Kama huna hela tulizana na package uliyolipia, siyo kuja kutujazia sever kwa useless thread...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom