Clouds FM yatusaliti!
The whole week PJ wa Power Breakfast (clouds FM) alikua anatembelea migodi ya Barrick. Akaja na bla bla bla kwamba wamepeleka maendeleo katika vijiji vilivyo zunguka migodi. Mie nimemuona yeye na waliemtuma kwamba ni wa puuzi. Sababu ni hizi:
1. Mikataba ya migodi ni mibovu - Nani analaumiwe kwa mikataba mibovu? Barrick au serikali yako na Bunge lako ''tukufu''? Mikataba yao hata kama ni mibovu lakini iko kwa mujibu wa sheria ya madini ya mwaka 1998 iliyopitishwa na mbunge wako. Barrick hawakuingia Bungeni kupitisha sheria hiyo!
2. Tunapata ONLY 3% from revenue ya madini - Nani wa kulaumiwa? Barrick au serikali yako? Na je wajua kwamba kampuni ya Alex Sterwart inalamba 1.7% out 3% tunayokusanya kwa kukagua mauzo ya dhahabu!? Nao huo si mkataba mbovu kati ya serikali yako na Alex Sterwart?
3. Migodi imetililisha sumu katika mito kama Tighitte na watu pamoja na mifugo imekufa - Je serikali yako imechukua hatua gani katika kuwawajibisha wahusika wa hili>? Kama ushahidi upo kwanini wasifikishwe mahakamani?
4. Watu waliwahi miminiwa risasi na walinzi wa migodi na wengine waliuwawa na hamna aliekamatwa kwa kuua - Kama walikiuka sheria za ulinzi wa migodi ulitegemea nini? Kumbuka pale kuna dhahabu kwa hiyo ulinzi mkali wa kutumia silaha unaruhusiwa kwa mujibu wa sheria. Na je walikuwa raia wema au majambazi? Kama kuna ushahidi kwanini kesi hiyo isipelekwe mahakamani?
Leo hii PJ na Power Breakfast, niseme Cluods FM wamesimama na kufagilia migodi ya walanguzi. Hii ni haki? Si ni usaliti huu?
PJ, unadhani hatujui kwamba ulikaribishwa na wana Barrick, ukalipiwa malazi na ukapandishwa ndege yao, unategemea sisi tutaamini kwamba utawaponda? Unatakiwa kumwomba radhi PJ kwa kumdhalilisha kiasi hiki. Sidhani kama yeye ni masikini kiasi cha ''kununuliwa'' kwa kupandishwa ndege, kupewa chakula na malazi ya mgodini ili kumsafisha mtu au taasisi iliyo ovu. Yeye ametoa maoni yake kulingana na aliyoyaona!
Hao jamaa wanafanya PR ili tuwaone niwasafi na wanatusaidia. Hamna kitu. Ni capitalist wanataka kupata faida lukuki ya madini na watimke baadae na kutuachia mashimo - Huo ndio ukweli japo ni mchungu sana! Hakuna bepari yeyote duniani anayefanya kazi bila kutegemea faida kubwa. Msingi wa ubepari ni mtaji unaozaa faida. Suala la kuachiwa mashimo ni kuzungumza wewe na mbunge wako!
Mimi na wewe PJ tutabaki hapa hapa TZ. Hiyo cheap PR unawapa haitafautiani na ile ya Richmond kuweka matangazo katika magazeti na kudai ni kampuni halali. Nani aliamini? Wapo watu wenye upeo mdogo wakuchambua mambo wakaamini. Na wewe unatakata tukuamini? Mimi nitoe!
Ukasema tena kwamba eti hatuwezi kuiendesha migodi sababu gari moja inayobeba mchanga wa madini linaizwa $1,000,000. Tujilize, walieba hela kupitia Kagoda waliiba liasi gani? Tsh. 40billion. Hizo hela zinaweza nunua migari haina hiyo mingapi? Na Liyumba je? Anashutumiwa kuiba Tsh. 220billion, nae angenunua migari mingapi? Sasa nikuulize PJ, hao jamaa zako wa Barrick, hizo investment wanatoa mifukoni mwao au wanakopa? Sisi hatuwezi kukopa au kuiba BOT tuka invest katika migodi yetu? - Hapa sasa ndipo unapothibitisha kwamba serikali yako imeoza na haiwezi kufanya chochote kwa sababu ya wizi na ubadhirifu wa mali ya umma. Tanesco hiyo hapo mbona inawashinda kuendesha? Mashirika ya umma mbona yaliwashinda kuendesha? ATCL, TRL mpaka kesho yamewashinda! Mgodi wa Mwadui mliampora mkoloni mbona umeshinda kuendesha? Hao wezi wa BoT si ndio hao hao wangekwenda kuiba huko migodini?
Huu ni ujinga watu kama PJ na watawala wengine wanataka tuamini kwamba hatuna uwezo wakuchimba madini yetu. Nakataa. - Hakika ninakuambia leo hii, mimi siwatetei Barrick au wachimbaji wengine hata kidogo. Ninachosema, bora wao wanaendesha uchimbaji huu kwa ufanisi na matunda yake tunayoaona kutokana na kodi, ajira na mirahaba wanayolipa. Jukumu hili ingeachiwa serikali yako ungeshangaa migodi imekufa, faidi haijulikani imekwenda wapi na hakuna wa kuwajibiswa! ''I see the glass half full while you see the glass half empty''