Nimekuelewa mkuu.
Unajua hapa kwnye hii thread kumejaa ushabiki mwingi, lakini uhalisia upo. Na uhalisia wenyewe ni kwamba Clouds still hawajapata mpinzani wa kweli., ukiondoa zile kasoro ambazo wanalalamikiwa kwa miaka kadhaa lkn kwenye content hawana mpinzani wa kweli. Jamaa wana vipindi vizuri mno, lakini pia wamevipangilia vizuri sana..watangazaji wao wengi wana vipaji vya kweli sio wazugaji, kwa hali hiyo clouds hawawezi kushushwa kizembe kwa kiki za muda mfupi.
Mfano mimi, nilikua #1 fan wa clouds..haikuwah kupita siku sijasikiliza xxl, Amplifaya na Sports extra. Zile kasoro zao chache (ukabila, migogoro isiyoisha na wasanii, shutuma za unyonyaji nk) Vikanikimbiza. Mpaka leo Sijawahi kupata radio mbadala yenye package kama Clouds..wengi wanajaribu lkn hawafanyi kweli.
Pamoja na hayo yote sijafikia hatua ya kuamini kwamba Wasafi FM ni mbadala wa Clouds(kwa sasa, labda tuwape mda). Ni fursa kwao kuangalia yale mapungufu ya Clouds na wayafanyie kazi..kwenye yale mazuri wafanye zaidi. Kuna mdau hapo juu amesema mwisho wa siku wasafi fm watakua na watangazaji, radio zitapimanishwa kwa kuwaangalia wao na sio kiki za (wamiliki) wao plus uzuri wa vipind na mpangilio wake. Pia usikivu wke hata huku interior, that's the only way kufight clouds sio hizi kelele za kupita.
Clouds nao wanayo nafasi ya kuangalia ni wapi wamejikwaa na wakarudi waendeleze ufalme wao mana bado hawa (wapinzani) wako wako too slow.