Malaamiko yangu kuhusu Clouds Media Group (clouds fm na clouds tv) ni vyema niyaweke hapa maana najua nikifungua uzi wake, unaweza ukafutwa na Mods (it happened before)
Wafanyakazi wao, baadhi hawana maadili ya kazi na katika jamii.
Hapa nitawazungumzia watatu
1. Perfect Crispin, huyu alimkosea Vanessa Mdee live on air kwenye interview, kipindi cha XXL kwenye ile studio yao ya zamani, nadhani ilikuwa 2017, wakati Vanessa amesimama anaongea kwenye mike, Perfect alikuja kwa nyuma akambahishia Vanessa, watu wakacheka mule studio ila Vanessa akageuka hakujua ni kitu gani kimetokea, ila huyu jamaa bado ni mfanyakazi wa Clouds hadi leo. Video ya tukio ipo YouTube waliiweka wenyewe.
Hilo tukio ni sexual harassment simple and clear.
2. Loveness Malinzi "Diva", huyu ndio huwa haguswi pamoja na kufanya vituko mitandaoni.
Miezi 3 iliyopita alijitamba kuwa katembea na Alikiba (mume wa mtu).
Tatizo linakuja pale kuwa yeye ndio anaendesha kipindi cha Mapenzi na mahusiano, sasa anashauri vipi watu kwenye Mapenzi wakati yeye ndio anavunja ndoa za watu?!
Alitolewa on air kwa miezi miwili ila leo yupo on air kama kawa.
3. Mwijaku, huyu jamaa anapenda sifa sana na kujifanya ni fundi wa mapenzi na kuwa kwenye ndoa iliyo "perfect", ila leo kafikishwa mahakamani kwa tuuma za kusambaza picha za uchi (Menina)
Ila hii July kapewa na kipindi cha Leo Tena na clouds Tv yupo na Soudy Brown
Sasa huwa najiuliza hii Clouds Media huwa wanazingatia nini kwenye kuajiri Wafanyakazi wao?!?
Maana hao ni wachache tu ila wenye vituko wapo wengi.