clouds fm muda huu..

Nyleptha

Member
Jun 19, 2012
69
0
Clouds fm, wanapatanisha ndoa kati ya Tobby na Tausi, hivi kweli ndio njia sahihi.
Nimesikiliza kipindi hicho cha njia panda ambapo wanandoa Toby na Tausi wana mgogoro au ugomvi, wameshirikisha wazazi imeshindikana ndio Tausi kaja redioni anasimulia hadi mambo ya ndani kabisa loh! Binafsi nimeona si sahihi kuelezea mambo hayo redioni, ni kujidhalilisha tu! Lakini sijajua wanatakiwa wayajadili wapi kama wazazi wameshindwa!
 

adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
11,099
2,000
Clouds fm, wanapatanisha ndoa kati ya Tobby na Tausi, hivi kweli ndio njia sahihi.

Sio sahihi hata kidogo. Kutangaza kupitia redio mambo ya ndoa sio sahihi na hayo siyo matanngazo ya mpira.

Upatanishi wa mambo ya ndoa unahitaji hekima na utulivu kwa wachache wenye sifa hizo, kuanika udhaifu wenu kwa kila mtu ni kujichimbia handani litakalo ifukia na kuizika ndoa kabisa.
 

Lateni

JF-Expert Member
Jun 11, 2012
677
225
Kama walikua na ugomvi na wamefanikiwa kupatanishwa ni vizuri, haijalishi njia waliotumia,
 

Pomboo

Senior Member
Jun 8, 2010
130
225
Hakuna aibu mbaya kama kujidhalilisha mwenyewe,mambo ya ndani na redio wapi na wapi!
 
Top Bottom