Clouds FM, hiki mnachofanya ni kampeni kwa CCM

Clouds FM, hiki mnachofanya ni kampeni kwa CCM

Wakuu Radio CloudsFM ina promo ya tangazo lao la kipindi chao kipya kuhusu siasa kuelekea uchaguzi mkuu.

Kwenye tangazo lao la kipindi hicho kipya wameweka sauti ya Magufuli akiongea kwa zaidi ya sekunde kumi akisema "maendeleo ya kweli yatatoka kwenye kiongozi anayetoka CCM"

Alafu naweka sauti ya Lowassa anasema "Peopleees zungusha zungusha"

Moya kwa moja promo hii ni kampeni ya kwa CCM maana mgombea wake ana nadi sera za chama au kujipigia debe, kama wako huru na siyo kampeni kwa ccm , walipaswa kuweka sauti ya Magufuli akisema "CCM oyeee" ili kuendana na anachozungumza Lowassa kwani Lowassa anatoa salamu ya chama na Magufuli ana nadi sera za chama.

Hili ndilo bao la mkono alilosema Nape.

Watanzania tunapenda sana kulalama,mbona mimi sioni hilo tangazo kama lina shida!!
 
Clouds Ni Maadui wa watu na umma wa watanzania.

Clouds wanaongoza kwa kukalia haki za wasanii, angalia bifu ya Sugu, Lady JD, mwisho wa siku wasanii walizidi kupaa juu.

Sasa hivi wamesimama na kupinga mabadiliko wakitumia redio hiyo. Hakika wamefanikiwa kuchora mstari wa kuonyesha wao ni wapinga mabadiliko na maadui wa mabadiliko.

Wana haki ya kufanya walivyofanya, lakini kwa wengi wamepoteza nafasi yao waliyokuwa wamebakiwa nayo mbele ya wananchi.

Walioifikisha clouds hapo ilipo ni wananchi wa kawaida , na ni wananchi hao hao waliofakisha hapo walipo.

CCM haitawasaidia

Clouds ni kituo BINAFSI kwahyo wanafanya watakavyo kwa manufaa yao si kwaajili ya kukufurahisha wewe!
 
Wakuu Radio CloudsFM ina promo ya tangazo lao la kipindi chao kipya kuhusu siasa kuelekea uchaguzi mkuu.

Kwenye tangazo lao la kipindi hicho kipya wameweka sauti ya Magufuli akiongea kwa zaidi ya sekunde kumi akisema "maendeleo ya kweli yatatoka kwenye kiongozi anayetoka CCM"

Alafu naweka sauti ya Lowassa anasema "Peopleees zungusha zungusha"

Moya kwa moja promo hii ni kampeni ya kwa CCM maana mgombea wake ana nadi sera za chama au kujipigia debe, kama wako huru na siyo kampeni kwa ccm , walipaswa kuweka sauti ya Magufuli akisema "CCM oyeee" ili kuendana na anachozungumza Lowassa kwani Lowassa anatoa salamu ya chama na Magufuli ana nadi sera za chama.

Hili ndilo bao la mkono alilosema Nape.
kwa miaka 51 sasa ya utawala wa CCM hawahitaji kuleta sera tena, wananchi wameshazisikia na kuzisoma sera zao ccm na hawakuona nafuu kwenye maisha yao. Sasa hivi sera yao yenye afadhali ni barabara, lakini hawatuambii ni akina nani na kwasababu gani watu wanaiba mifuniko ya chemba za majitaka barabarani, kuiba alama za barabarani na kukata madaraja kwenye barabara hizo. Bila shaka hawa watakuwa ni wananchi waliopigika kwa umasikini uliosababishwa na sera za CCM kwa miaka 50. Watu hawataki kusikia habari za sera tena bali wanataka maji, ajira, elimu, matibabu, mikopo kwa 100% kwa wanafunzi wote, na hawataki rushwa na kupanda kwa gharama za maisha. Na mwisho watu wanataka katiba yao waliyoipendekeza sio ile ya Sitta na CCM
 
Clouds ni kituo BINAFSI kwahyo wanafanya watakavyo kwa manufaa yao si kwaajili ya kukufurahisha wewe!

Kuna aliyekuwa anakata mti amekaa kwenye kuti, kuna waliopita wakamwambia ataanguka. Na alianguka kweli.
Wamejiandaa na madhara ya maamuzi yao ?
 
Clouds Ni Maadui wa watu na umma wa watanzania.

Clouds wanaongoza kwa kukalia haki za wasanii, angalia bifu ya Sugu, Lady JD, mwisho wa siku wasanii walizidi kupaa juu.

Sasa hivi wamesimama na kupinga mabadiliko wakitumia redio hiyo. Hakika wamefanikiwa kuchora mstari wa kuonyesha wao ni wapinga mabadiliko na maadui wa mabadiliko.

Wana haki ya kufanya walivyofanya, lakini kwa wengi wamepoteza nafasi yao waliyokuwa wamebakiwa nayo mbele ya wananchi.

Walioifikisha clouds hapo ilipo ni wananchi wa kawaida , na ni wananchi hao hao waliowafikisha hapo walipo.

CCM haitawasaidia , nguvu ya chombo chochote ni umma, wamekwisha hao na hela mliyopata CCM ndio ya mwisho

Nyie Vp Adui Wa Mabadiliko Ya Nan?Kumbuken Hawa Ndiyo Chombo Pekee Kinachoiponda Tbc1 Kwa Kutokua Fair Katka Utangazaj Wa Magazet Kila Cku Asubuh Hawa Ndo Wanalipgia Kelele Since Last Week,af Leo Mnasema Et Adui Wa Mabadiliko Acheni Mihemko Ya Vyama Yenu Katika Kufikria....
 
Acha hisia wewe hawa ni chombo huru,na wanaofuata maadili,huo mzigo wa kukubebea mzigo wako hawawezi,huyo mlimchagua wenyewe aje amiliki ukawa mtasikia mengi dhidi yake na ninawahakikishia yapo meng mtachukia media zote
 
Yah sijaoona sera ya lowasa mpaka wamuweke akinadi sera maana ye ni kusema tu anatamani wanachi wawe matajiri hahahahahaaa huyu kweli anafaa kua mfugaji tu hata kuingea hawezi FISADI TEMBOO
Nchi imevurugika sana, wananchi hawana haja na wasanii kwa sasa wala sera bali wanataka mishahara ya kutosha kuanzia kwa askari hadi raia, wanahitaji maji, ajira, matibabu na elimu. Wameshoshwa na rushwa, jembe la mkono, ukosefu wa masoko na gharama kubwa za maisha, ndo maana CCM inakosa jambo jipya la kuwaambia wananchi mwaka huu kwakuwa yenyewe ni sehemu ya maisha ya sasa ya watanzania.
 
Nyie Vp Adui Wa Mabadiliko Ya Nan?Kumbuken Hawa Ndiyo Chombo Pekee Kinachoiponda Tbc1 Kwa Kutokua Fair Katka Utangazaj Wa Magazet Kila Cku Asubuh Hawa Ndo Wanalipgia Kelele Since Last Week,af Leo Mnasema Et Adui Wa Mabadiliko Acheni Mihemko Ya Vyama Yenu Katika Kufikria....

Watu wengne hawajielew,muda wote kulalamika tu,juzi clouds wamewachana TBC hakuna hata mmoja alieyesema kitu!
 
acha hisia wewe hawa ni chombo huru,na wanaofuata maadili,huo mzigo wa kukubebea mzigo wako hawawezi,huyo mlimchagua wenyewe aje amiliki ukawa mtasikia mengi dhidi yake na ninawahakikishia yapo meng mtachukia media zote
mkuu acha unazi wa chama na wagombea simama kwenye fact najua pengine unafakazi clouds na unahaki ya kutetea lkn sio kununuliwa na uoga wa kitoto mnamtii kwa kuwa amewapa vijicent.
 
Kuna aliyekuwa anakata mti amekaa kwenye kuti, kuna waliopita wakamwambia ataanguka. Na alianguka kweli.
Wamejiandaa na madhara ya maamuzi yao ?

Mbona juzi clouds wamewasema TBC kwamba wanapendelea chama tawala hukuja hapa kuwasifia???....
 
Wanachoweza kufanya CCM ni propaganda na kucheza na akili za watu.

Wengi wa watu wanajua wanataka nini mwaka huu ni mabadiliko tu.

Sera ni moja , mabadiliko, ongoa CCM,weka utawala wa wananchi.
Hakuna anayeweza kuzuia hilo, hatushangai mwenye ngoma kutaka wimbo.

Lakini ngoma yao ya kitoto , haikeshi na mwisho ni octoba 25

UKAWA Zaidi.
 
wape live za usoni, mimi nishaacha kuwasikiliza hawa jamaa long time. matangazo yamekuwa too much na story zao za kimbea zishanipotezea ladha ya kuwasikiliza.
 
Kumbe watz tumeamka ..nilifikiria hivyo pia..hawa jamaa wanaonyesha mahaba ya dhati kwa CCM..pia hata habari za ukawa zinatangazwa sio km zinavyostahili..mfano mwanza hawakuonyesha lile nyomi..walionyesha baadhi ya wana ukawa lkn haikua rahisi kusikia wanachokisema as sauti ilikua very poor..nadhan wanatumika kuhujumu UKAWA..u don't need to hold shahada ya uzamivu to realise that...

ITV ndio hasa wanaongoza live kwa upendeleo lakini kwa sababu ndio walewale mnafyata mikia yenu, kwanza sijaona tatizo katika tangazo hili ila tu ni mihemko yenu ya kutaka kila mtu afanye mpendavo. sijaona upendeleo wowote wa clouds kwani kila siku huwa wanaipona sana serikali na wala huwasikii wana ccm wakilalama ila ni tofauti kwa hawa wana UKIWA
 
Hata ccm wako akina Hussein Mwinyi, Leticia Nyerere, Makongoro Nyerere, Amani na Ali Karume, Riz1, Vita, Zainabu Kawawa, January Makamba, Mwele Malechela, Siyoi, Mgimwa, Sitta na mama sita, Mama Kilango Malecela, n.k. usitupotoshe sema jingine sio hili.
Hawana tofauti na wewe ambae ni MLAMBA MIGUU ya MBOWE....................Na jiangalie sana utaolewa kam hawa.............................................
UKOO WA CHADEMA BUNGENI WAANIKWA: GAZETI LA UHURU










BAADHI ya wabunge wameiumbua CHADEMA, wakieleza kuwa chama hicho ndicho kinaongozwa kwa utawala wa kifalme.


"Lissu kaja na dada yake. Ukienda kwa Mwenyekiti wa Chama ana ndugu watatu, Slaa kuna mke wake, nani ana utawala wa kifalme? Ndesamburo amekuja na mtoto wake na mkwe wake, Samahani Mh. Ndesamburo"

Akichangia juzi, muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2011,
Assumpter Mshama (Nkenge –CCM), alisema utawala wa kifalme upo CHADEMA.

"Mfadhili wao amekuja na mtoto wake, kuna mdogo wake, ukienda kwa Lissu kaja na dada yake. Ukienda kwa mwenyekiti wa chama ana ndugu watatu, nani ameleta ufalme zaidi," alihoji.

Aliongeza: "Slaa kuna mke wake, nani ana utawala wa kifalme, Ndesamburo amekuja na mtoto wake na mkwe wake, samahani mheshimiwa Ndesamburo.

"CCM ilitengeneza utaratibu wa kupata viongozi wa viti maalumu, wao si kifalme tu, tuseme ni kaskazini tu, nawashangaa watu wanaojiita CHADEMA, wenzako wako bungeni huulizi wamepatikanaje."

Kwa upande wake, Livingstone Lusinde
(Mtera-CCM), akichangia jana, alisema CHADEMA ndiyo yenye tabia ya kupeana madaraka kwa kufuata unasaba.

Alisema viti maalumu vimetolewa kwa unasaba, na kama hilo lingefanywa na CCM ingekuwa wimbo kila siku.

"Ndiyo maana humu ndani wamo wakwe, dada, kaka, ingekuwa ni kwa CCM ingekuwa wimbo kila siku. Nashangaa wanaposema rais anaongoza kifalme," alisema.

Lusinde alisema wanaotoa vitisho vya kuandamana na kwamba wapo tayari kufa kwa ajili ya katiba waachwe wafanye hivyo kwani wa kuzuia fujo wapo.

"Wanaotaka kufanya vurugu waachwe tu, wengine wanasema wapo tayari kufa kwa ajili ya katiba. Mimi sipo tayari nataka nione katiba mpya, ambayo Watanzania wamekuwa wakiitaka kwa muda mrefu," alisema.

Lusinde aliohoji busara ya wazee wa CHADEMA ambao wameshindwa kutoa kauli baada ya vijana wao kuchafua hali ya hewa.

Mbunge huyo alisema CHADEMA inafanya hivyo kutokana na ahadi ya fedha waliyopewa na Ujerumani.

CHADEMA imesusa kujadili muswada huo unaohitimishwa leo, baada ya kujadiliwa kwa siku nne, kwa kile wanachodai umekosa uhalali kwa kukiuka Kanuni za Bunge.

Hata hivyo, CHADEMA imekuwa ikijibu hoja zinazojadiliwa na wabunge bungeni, kupitia mikutano na waandishi wa habari inayofanyika kila siku mchana, ambapo katika mkutano wa jana imeliomba bunge kutopitisha muswada huo.

Mikutano hiyo imekuwa ikiitishwa na viongozi wa CHADEMA, John Mnyika (Ubungo) na Tundu Lissu (Singida Mashariki), ambaye Jumatatu wiki hii aliwasilisha maoni ya Kambi ya Upinzani Bungeni, kuhusu muswada huo.

Katika maoni hayo, alipendekeza baadhi ya mambo kwenye muswada huo na pia aliwachefua wabunge kutokana na hoja zake kuhusu Muungano na pia kutamka kuwa Tanzania ina urais wa kifalme.

John Lwanji (Manyoni Magharibi-CCM), alisema wanachofanya CHADEMA ni sawa na kiini macho katika mazingaombwe, akitumia neno abrakadebra.

Benardetha Mushashu (Viti Maalumu-CCM), alihoji CHADEMA walitoka bungeni kwa kanuni gani na mbona hawachukuliwi hatua.

"Wanawalaghai wananchi, Lissu alichangia muswada. Wanaharakati wanatangaza kufanya maandamano yasiyo na kikomo kama kwamba hakuna serikali, wakijaribu wataona," alisema.

Alisema kinachoendelea Arusha ni matokeo ya maandamano ya kila siku, ambayo hivi sasa yameanza kushamiri Mwanza, ambapo watu wanapigwa mabomu ya machozi.

"Libya walianza na maandamano, Gaddafi ameuawa, lakini hivi sasa wanauana," alisema.

Wakati huo huo, Spika wa Bunge, Anne Makinda, amesema hamlazimishi mbunge kuingia kwenye kamati, bali anachofanya ni kufuata Kanuni za Bunge na Katiba.

Alisema hayo bungeni jana, kutokana na malalamiko yanayotolewa na CHADEMA na NCCR-Mageuzi kwamba, spika alilazimisha wabunge kuingia katika Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, kujadili muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2011.

Spika Anne alisema CHADEMA hawakutumia busara kutoka ndani ya ukumbi wa bunge, bali wangewasilisha hoja zao, na endapo wangeshindwa, basi wangeshindwa kishujaa.














 
huwezi kuwapangia.......Mara ya mwisho kuwasikiliza sijui lini .....maana nikisilikiza sichelewi kukureka...
 
kwa miaka 51 sasa ya utawala wa ccm hawahitaji kuleta sera tena, wananchi wameshazisikia na kuzisoma sera zao ccm na hawakuona nafuu kwenye maisha yao. Sasa hivi sera yao yenye afadhali ni barabara, lakini hawatuambii ni akina nani na kwasababu gani watu wanaiba mifuniko ya chemba za majitaka barabarani, kuiba alama za barabarani na kukata madaraja kwenye barabara hizo. Bila shaka hawa watakuwa ni wananchi waliopigika kwa umasikini uliosababishwa na sera za ccm kwa miaka 50. Watu hawataki kusikia habari za sera tena bali wanataka maji, ajira, elimu, matibabu, mikopo kwa 100% kwa wanafunzi wote, na hawataki rushwa na kupanda kwa gharama za maisha. Na mwisho watu wanataka katiba yao waliyoipendekeza sio ile ya sitta na ccm

wanaiba mifuniko ya chemba ni ndugu zako,
 
Back
Top Bottom