Ni kwamba mmesahau Jay Dee alipotangaza hadharani kwamba Clouds wasipige nyimbo zake na hata akifa wasiende, au? Anyway, Alikufa kwa Ngoma ni wimbo wa FA lakini Jide nae kashirikishwa, kuna sauti yake humo! Sasa ikiwa mtu ametangaza hadharani kwamba hata akifa hao Clouds wasiende, mnawalaumu vipi ku-mute sehemu ambazo yeye ameingiza sauti? Mbaya zaidi, Jide mwenyewe ana bifu hata na huyo Mwana-FA mwenye huo wenyewe!
Tukija la Majani... huyu si ndo yule alitangaza hadharani kwamba Clouds ndo wanahusika na vifo vya wasanii? Yaani watu na upumbavu wao wanakula unga huko, wanasingizia wanakula unga kwa ajili ya stress wanazopewa na Clouds, kama si upumbavu tuite nini?? Matokeo yake siku moja, kuna msanii wa zamani wa Majani alienda Clouds, nadhani alikuwa Jay Mo kama sikosei! Kati kati ya mahojiano, yule msanii akawa anamrusha Majani na mwenyewe akasema Majani amemuomba atakapofika studio amrushe... sasa ikiwa mnahitaji service za watu, jeuri za nini??!!!
Sasa anaposema nyimbo zake zisipigwe ni kwamba anawaambia akina Ruge au Joe hapo? Ruge anakaa studio? Kusaga aanakaa studio? Tangu lini Ruge au Kusaga akapiga nyimbo studio? Kwanza yeye hakusema Ruge au Kusaga wasipige nyimbo zake bali alisema Clouds wasipige... sasa Clouds ni mtu au taasisi? Alitaja majina kwenye msiba... hapa alisema wazi kwamba siku Jide akifa, Joseph Kusaga na Ruge wasikanyage kwenye msiba wake na kwamba wakienda, watu wawapige mawe!Hata kama Lady Jay Dee alisema hivyo,aliwaambia watu nadhani ni Ruge au Joe na si Taasisi kama Taasisi,sioni tatizo kwa jide kuwa na beef na ruge au joe,tatizo lililopo ni Taasisi nzima ya clouds kuwa na beef na jide hilo ndio tatizo.
Na mkitokea kwenye msiba, mpigwe mawe!Eti nina kampuni binafsi, af unatangaza bifu, unatangaza mapinduzi, unatutusi, unatangaza vita, hutaki tupige ngoma zako na msiba tusije wala kuongea chochote... Af mnataka wapige tu!.... Clouds wana mambo ya kifala lakini hata mimi naku-mute!...