Clouds FM acheni Utoto

Clouds FM acheni Utoto

Amalinze

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2012
Posts
6,780
Reaction score
5,318
Habari Wanabodi,

Nipo nasikiliza Clouds FM kipindi cha XXL Segment ya "Album Review". Leo wana Review Album (2003) ya Mwana FA ya "Toleo Lijalo" yenye nyimbo kama 'Wanapendana', 'Alikufa kwa Ngoma' etc. Kwenye wimbo wa 'Alikufa kwa ngoma' ameimba na Anaconda (Lady Jay Dee) cha kushangaza kwenye huo wimbo wakati wana review ikifika sehemu ya chorus ya Jide wana-mute inasikika beat tu. Kitendo cha Clouds FM kama taasisi kampuni nzima kuweka beef na msanii mmoja inajidhihirisha Clouds FM ni radio ya wahuni tu.

Clouds FM sio mara ya kwanza kufanya upumbavu huo, nakumbuka kipindi cha nyuma Inspector Haroun alienda nao tofauti, kipindi hiko wimbo wake wa "Buzi" ndio ulikuwa una-hit basi jamaa kila ikifika pale anapochana Inspector sauti wanaondoa inasikika beat tu.

Kwenye ngoma ya Ben Pol "Jikubali" kuna moja ya mstari unaimbwa "Nampenda Lady jay Dee,namzimia Zitto" ile sehemu ya neno Lady Jay Dee wanaisugua (Scratch) na ilo neno halisikiki kabisa.

Kwenye kuadhimisha miaka 15 ya Dully sykes, kwenye promo walikuwa wanapiga nyimbo za nyuma za Dully Sykes, kuna ngoma inaitwa Bijou inavyoanza ina neno "Okay mbili sifuri sifuri nne, P-funky kinywele kimoja" ilipoanza hapo kwenye P-funky wakaikata kabisa wakaipeleka mbele.

Kwa Mchezo huo wa kitoto unaofanywa na Clouds Media inaishushia hadhi sana hiyo kampuni. Kitendo cha kampuni hiyo kufanya mambo ya utoto ni wazi redio inaendeshwa na makanjanja na sio watu wenye weledi. Clouds FM ikubali pia matakwa ya wasanii, kama msanii akikataa kufanya deal kwa sababu anaona haimfaidishi yeye ni haki yake kukataa na si kigezo cha kutopiga nyimbo zake.

Kuna watu watasema kwamba redio zipo zaidi ya 60 na TV zaidi ya 20 kwanini wasanii wailalamikie Clouds tu? Hapa tunacholalamika ni kufinya (mute) sauti yeyote iliyopo kwenye nyimbo alizoshirikishwa msanii walioenda nae tofauti. Kama wanapiga wimbo wa Ben Pol waachie wimbo kama ulivyo na si ku-mute majina ya watu waliotajwa wenye beef nao.

CLOUDS MEDIA ACHENI UTOTO.
 
Ni kwamba mmesahau Jay Dee alipotangaza hadharani kwamba Clouds wasipige nyimbo zake na hata akifa wasiende, au? Anyway, Alikufa kwa Ngoma ni wimbo wa FA lakini Jide nae kashirikishwa, kuna sauti yake humo! Sasa ikiwa mtu ametangaza hadharani kwamba hata akifa hao Clouds wasiende, mnawalaumu vipi ku-mute sehemu ambazo yeye ameingiza sauti? Mbaya zaidi, Jide mwenyewe ana bifu hata na huyo Mwana-FA mwenye huo wenyewe!

Tukija la Majani... huyu si ndo yule alitangaza hadharani kwamba Clouds ndo wanahusika na vifo vya wasanii? Yaani watu na upumbavu wao wanakula unga huko, wanasingizia wanakula unga kwa ajili ya stress wanazopewa na Clouds, kama si upumbavu tuite nini?? Matokeo yake siku moja, kuna msanii wa zamani wa Majani alienda Clouds, nadhani alikuwa Jay Mo kama sikosei! Kati kati ya mahojiano, yule msanii akawa anamrusha Majani na mwenyewe akasema Majani amemuomba atakapofika studio amrushe... sasa ikiwa mnahitaji service za watu, jeuri za nini??!!!
 
clouds fm, tv ni watoto na ni wadogo sana hawana lolote ni washamba kaibisa huwezi media nzima kama hiyo kuwa na bifu na mtu kwanini lakini huo ni upuuzi kabisa kuanzia kiongozi wao hadi wafanyakazi hawana cha kiutu uzima ni utoto unawasambua
 
Ni kwamba mmesahau Jay Dee alipotangaza hadharani kwamba Clouds wasipige nyimbo zake na hata akifa wasiende, au? Anyway, Alikufa kwa Ngoma ni wimbo wa FA lakini Jide nae kashirikishwa, kuna sauti yake humo! Sasa ikiwa mtu ametangaza hadharani kwamba hata akifa hao Clouds wasiende, mnawalaumu vipi ku-mute sehemu ambazo yeye ameingiza sauti? Mbaya zaidi, Jide mwenyewe ana bifu hata na huyo Mwana-FA mwenye huo wenyewe!

Tukija la Majani... huyu si ndo yule alitangaza hadharani kwamba Clouds ndo wanahusika na vifo vya wasanii? Yaani watu na upumbavu wao wanakula unga huko, wanasingizia wanakula unga kwa ajili ya stress wanazopewa na Clouds, kama si upumbavu tuite nini?? Matokeo yake siku moja, kuna msanii wa zamani wa Majani alienda Clouds, nadhani alikuwa Jay Mo kama sikosei! Kati kati ya mahojiano, yule msanii akawa anamrusha Majani na mwenyewe akasema Majani amemuomba atakapofika studio amrushe... sasa ikiwa mnahitaji service za watu, jeuri za nini??!!!

Hata kama Lady Jay Dee alisema hivyo,aliwaambia watu nadhani ni Ruge au Joe na si Taasisi kama Taasisi,sioni tatizo kwa jide kuwa na beef na ruge au joe,tatizo lililopo ni Taasisi nzima ya clouds kuwa na beef na jide hilo ndio tatizo.
 
Eti nina kampuni binafsi, af unatangaza bifu, unatangaza mapinduzi, unatutusi, unatangaza vita, hutaki tupige ngoma zako na msiba tusije wala kuongea chochote... Af mnataka wapige tu!.... Clouds wana mambo ya kifala lakini hata mimi naku-mute!...
 
Hata kama Lady Jay Dee alisema hivyo,aliwaambia watu nadhani ni Ruge au Joe na si Taasisi kama Taasisi,sioni tatizo kwa jide kuwa na beef na ruge au joe,tatizo lililopo ni Taasisi nzima ya clouds kuwa na beef na jide hilo ndio tatizo.
Sasa anaposema nyimbo zake zisipigwe ni kwamba anawaambia akina Ruge au Joe hapo? Ruge anakaa studio? Kusaga aanakaa studio? Tangu lini Ruge au Kusaga akapiga nyimbo studio? Kwanza yeye hakusema Ruge au Kusaga wasipige nyimbo zake bali alisema Clouds wasipige... sasa Clouds ni mtu au taasisi? Alitaja majina kwenye msiba... hapa alisema wazi kwamba siku Jide akifa, Joseph Kusaga na Ruge wasikanyage kwenye msiba wake na kwamba wakienda, watu wawapige mawe!
 
Back
Top Bottom