Clouds "Amka na Pests Man" na mrejesho wake

mayowela

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2014
Posts
2,125
Reaction score
1,757
Mwaka 2017 iliendeshwa harambee ya kumchangia msanii Pests Man anaeishi Mwanza, huyu jamaa aliugua muda mrefu sana tatizo ni Uti wa mgongo na alikuwa kitandani kwa muda mrefu sana mpaka hapo walipojitokeza clouds

Jamaa anaimba miondoko ya Dancehall na pia ni beat maker, Kupitia Godfrey Kusolwa mtangazaji wa kituo tajwa ndio alikuwa mkusanyaji wa pesa kwa ajili ya matibabu kuelekea India na Kituo tajwa kiliingilia kati kusimamia michango hiyo na kuhamasisha watu wachangie mpaka ikafikia kipindi cha Clouds 360 kilienda kufanyika Mwanza Nyumbani kwa kina Pests Man na hari kweli ilikuwa ya kusikitisha.

Pia Pests Man alisema anauwezo wa kutengeneza Beat kupitia computer aliyonayo na ikanunuliwa na wasanii kama mchango wa matibabu yake,

sasa wananzengo wanahitaji kufahamu baada ya ile hamasa ya michango iliyofanywa na kusimamiwa na watu kutoka kituo tajwa, Hari ya Mgonjwa inaendeleaje au amefikia hatua zipi mana Nzengo ilichanga inahitaji kufahamu.
 
Kweli Aisee tuyajue yote haya sasa hivi! Wasije kuwa wanatumia fursa afu wanapiga pesa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaburi la kwanza bint kipepeo.
Ili litakua lapili nadhani,,,,
Jamani msifukue makaburi,,mbona hamsikii nyinyi,,,
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nahisi wanataka kurudisha gharama zao kwa namna mbili ya kwanza itakuwa Kapona au Hamna dalili ya kupona tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 

This is Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…