i pitty you brother, najua unatumia phpfox tena nulled...ila jambo la msingi ni iyo theme ya facebook, ndo umeniangusha tafuta theme tofauti, jaribu kuicustomize ifanane kibongo bongo lakini ukifananisha na facebook maana yake unataka kuwaambia watu unatamani kitu kama facebook
kwa taarifa yako: Nilikuwa naiba code miaka iyo zamani nikiwa sekondari hata kabla sijajua chochote kuhusu designing, nilikuwa nafanya for fun with my friends miaka kumi iliyopita.....brother mi naelewa wazo lako na malengo yako ni mazuri ila mh....hapo hata ukitaka sponsors wakikuuliza umeiba idea fb utawajibuje? Yani ungejua ungewasikiliza wadau wanachokwambia.
siitaji sponsers, sina dhiki kiasi hiki,
code ntaiba mpaka siku web duniani kote itakua open source standerd
kama wakisema nimeiba idea ya fb, nitasema ndio na isitoshe, nimeiba na users wao
Social media solutions zipo nyingi sana, je matatizo yetu hapa bongo hayawezi kutatuliwa na nyinyi wana ICT kwa kubuni solutions zake? Acha kupoteza muda na hizi social sites kwani 'value' yake ipo chini sana kwa mahitaji yaliyopo hapa kwetu.
Challenge ya innovation ni kuumiza kichwa kwenye arena ambayo haijafikiriwa na kuweka solution hapa.
Kama lengo ni kujifunza tu, sioni tatizo lakini kama comment moja hapo juu inavyosema, kuweka huo mtandao hewani unahitaji pesa, sio tu za kuhost lakini ya kuiendeleza. Social media yetu wenyewe sioni maana yake kwani ulimwengu wa leo hauna hiyo mipaka, anyway challenge kwenu wan ICT...
halafu kama nakumbuka SamJet ulishawahi kuja na kitu kama hiki. Yes! Ilikuwa inaitwa rafikibuzz ambayo nayo ilikuwa community site too. What happened?
Ni hii hapa: rafikibuzz the african number 1 social network
it is better-looking and sophisticated kuliko hiyo bongobest! Although bado muonekano kidogo unafanana na facebook.
kama huna njaa na hutaacha wizi, sasa lengo ni lipi kufanya haya unayoyafanya? Wote uwa tunaiba lakini kidogo kidogo, unaiba hapa na pale ukijumlisha na idea zako kinatokea kitu unique, sasa kama wewe kaka utaiba kila kitu huoneshi ukomavu wako katika fani hii, ni sawa orijino komedi wangekuwa mpaka huku wangekutoa kwenye ile segment yao ya vilaza wanaokopi na kupesti
Mobile version, http://www.bongobest.com/index.php?do=/mobile/
Nimechukulia ushauri wako vyema xana mkuu.
tatizo la huyu jamaa limbuken anataka mawazo halafu hataki critics watu wote walomponda kabishana nao anza mwanzo wa thread mpaka hapa utaona.
La sivyo asema hataki ushauri ye ana advertise tu
pia alileta clone nyingine ya twitter ambayo nadhani nayo haikuwa successiful, ilikuwa ukijiunga unatumiwa email karibu mia moja nikasema mungu wangu ni nini hiki.......