Hanifer Mjanja
Senior Member
- Dec 10, 2019
- 189
- 270
Clinic ya Marie Stopes iliyoko jijini Mwanza wanajihusisha na vitendo vya utoaji mimba. Mimba zinatolewa sana hapa, hasa za wanafunzi wa vyuo vikuu maarufu vya hapa Mwanza (sitaki kuvitaja) na wake za watu waliopata mimba za michepuko.
Mchezo unaofanyika ni kwamba wanawake wanaohitaji hiyo huduma hufika hapo na huulizia huduma ya abortion, au kwa kujifanya mimba imeharibika. Pia, wale wanaokuja kupima mimba wakipatikana kuwa wana mimba na wakaonyesha hali ya kutofurahia au kushtuka, huwa mara nyingi wanauziwa wazo la kuichoropoa.
Kinachofuata, mhusika anafanyiwa huduma inaitwa "dilatation and curateage", ambayo kimsingi ni kutanua njia ya shingo ya kizazi, kisha kuharibu mimba kwa kusafisha kizazi.
Sasa, the way wana record hiyo ili kuficha huo uozo ni wana record kama vile mtu alikuja na "miscarriage" tayari au "incomplete abortion" halafu kuwa wao wakasafisha tu kizazi kuondoa mabaki yaliyobaki kwenye kizazi, lakini ukweli ni kwamba wanakua wameharibu mimba na kufanya abortion ila kwenye rekodi zao wanaonyesha kama vile ni incomplete abortion.
Kuna uwezekano pia timu ya usimamizi wa huduma za afya ya halmashauri na hata ya mkoa inajua kabisa mchezo unaoendelea lakini wananyamazishwa kwa bahasha, maana hizi habari ziliwahi kuripotiwa kwao lakini hakukua na hatua zozote ziulizofuata.
Pia, hawa watu kuanzia wakati wa usahili kama unataka kuajiriwa pale kama daktari au muuguzi, wanakuuliza kabisa wewe mtazamo wako kuhusu utoaji mimba ukoje, na wanakupa scenario kuwa ikitokea wakati unatimiza majukumu yako halafu akaja mteja ambae anataka kutoa mimba je utachukua hatua gani? Ukitoa majibu ambayo yanaonyesha kama vile unapinga mambo ya abortion, wanakuchinjia baharini hupati hiyo kazi.
Tukumbuke kuwa kwa nchi yetu, utoaji wa mimba (abortion) ni kinyume cha sheria.
Nimeona nifichue hili jamani nimechoka vitendo hivi kila siku nashiriki utoaji mimba ila ni kwa sababu ya njaa tu, nimeona nije kutoa ripoti huku, Wizara ya Afya Tanzania fuatilieni hili mchukue hatua.
Nendeni pale kagueni records zao muone walivyo na "incomplete abortion" kibao ambazo wanazifanyia dilatation and curatage, hizo zote ni mimba ambazo zimetolewa hakuna cha incomplete abortion wala nini.
Fanyeni uchunguzi kwa makini, mtagundua kitu, ila msiende kichwa kichwa.
Asante.