Maoni, mitazamo kuhusu sheria ya utoaji mimba kwa wanaopata ujauzito bila ridhaa yao

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Wiki iliyopita katika makala ya Sheria ya katazo la Utoaji Mimba Tanzania dhidi ya uhalisia wa maisha halisi ya mtaani nilielezea kuhusu uhalisia ulivyo kwa sasa wa matukio mengi ya unyanyasaji wa kingono yanayotokea kwenye jamii zetu.

Makala iligusia jinsi Wasichana wadogo wanavyobebeshwa ujauzito bila ridhaa yao, wengi wakilazimika kubaki na hali hiyo kwa kuwa Sheria ya Tanzania inazuia kutoa ujauzito, wapo wanaopitia maumivu makali wakati wa kujifungua, kupata majeraha ya muda mrefu na wengine kupoteza maisha.

Makala ilieleza jinsi Tanzania ilivyosaini MKATABA WA MAPUTO, ambayo Ibara ya 14 2 (c) inaelezea haki ya utoaji mimba kwa kuzingatia sababu kadhaa ikiwemo kubakwa au kufanya ngono na ndugu wa karibu, lakini Tanzania imechukua kigezo kimoja tu cha kuruhusu kutoa kama mimba inahatarisha afya ya mama.

Haya ni maoni ya Wadau kuhusu IBARA YA 14 YA MKATABA WA MAPUTO 2c, kuhusu kama kuna umuhimu wa Tanzania kuongeza vigezo vya utoaji mimba au sheria ibaki kama ilivyo:

Reuters.jpeg
WILLIAM MADUHU
~Afisa Programu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)

Anasema “Mkataba wa Maputo una vipengele vingi ambavyo kama Nchi umevifanyia kazi vingi lakini hicho cha kuruhusu utoaji mimba kiliachwa kwa kuwa ni kitu ambacho hakiendani na tamaduni zetu, Nchi ilifanya hivyo kutokana na mazingira na sheria zetu za ndani.

“Kwani inapotokea kuna mkataba wa kimataifa unaopingana na sheria za ndani inamaanisha zile za ndani lazima zinakuwa zimekufa.

“Inapotokea amepata mimba bila ridhaa yake kama vile kubakwa na mtu mwenye VVU (HIV) au matatizo mengine ya kiafya ni wazi itaingia kwenye kipengele cha kutoa kwa ruhusa ya afya ya mama na itafanya hivyo.”

LOVENESS JOSEPH MUHAGAZI
~Ofisa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)
Ni kweli mazingira ya mwanamke kupata mimba bila ridhaa yake inatokea, na wengine wanapata pasipo kulazimishwa bali inatokea tu amekosea tarehe au alipitiwa, kisha anagundua hana uwezo wa kiuchumi kuhudumia ujauzito na hata kiumbe kinachokuja.

“Ndio maana sasa hivi matukio ya watoto kutupwa, kuuliwa na kutelekezwa yametokea kwa wingi, inawezekana nyuma ya pazia kuna mazingira kama hayo ya mimba pasipokuwa na uwezo na mipango ya kuitunza.

“Nikizungumza kwa imani ya dini yangu hilo jambo siyo sawa lakini katika maisha ya uhalisia tunaiyoshi kuwa na mtoto ambaye kesho yake hujui utakuwaje ni jambo gumu na linalowatesa wengi.

“Juzi hapa kuna video ilisambaa ikimuonesha mwanamke anamshushia kipigo kikali mwanaye kama vile anapiga kitu ambacho hakina uhai, wakati mwingine msongo wa mawazo na matatizo ya kisaikolojia ya wamama ndiyo yanasababisha matukio kama hayo japo si wote.

“Kisaikolojia pia mama anavyolea mimba kwa kisirani na akiwa hana uwezo inaweza kuathiri hata katika makuzi ya mtoto.

“Mfano kwa sasa kuna ‘singo maza’ wengi Tanzania, hivi unadhani hao wote wanafurahia hali hiyo? Jibu ni Hapana, wengine wametelekezwa, wamekimbiwa au wamesusiwa, wanashindwa kutoa mimba kwa kuwa Sheria inawazuia, wanabaki nayo, mwisho wake wapo ambao wanawalea watoto katika mazingira mabaya.”

misoprostol pills 3.jpg

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake
~Kwa sababu za kimaadili ya kazi jina lake limehifadhiwa

Anasema: “Mimba zinatolewa katika mazingira ambayo si salama, ninaposema hivyo nimaanisha inaweza kuwa kutokana na vifaa vinavyotumika au watoaji kutokuwa na uelewa mzuri kuhusu zoezi hilo.

“Matokeo yake Wanawake wengi wanapata matatizo ya kutoka damu sana, wanapata maambukizi, wengine athari zinakuwa kubwa wanatolewa kizazi au ini au kupoteza maisha kabisa.

“Hiyo ni kwa nini? Kwa sababu Sheria inawabana na inawezekana Kiserikali haitakiwi lakini ukifuatilia kuna mazingira mengi yanayoonesha michakato hiyo inafanyika mitaani kiholela.

“Nasema hiyo kwa kuwa hao wakishatolewa kiholela, wanapata madhara na mwisho wake ndio wanakimbilia hospitali kwa ajili ya kutibiwa wakati huo hali imeshakuwa mbaya.

“Mitaani wapo ambao wanatumia dawa za Misoprostol kiholela, wakishaharibikiwa ndio wanakimbilia hospitalini.

“Binafsi nashauri Serikali ifikirie kuongeza vigezo vinavyotakiwa kuongeza kutoa mimba kama wataona kuna umuhimu huo.”

HERIETH MAKWETTA
~Mwandishi mzoefu wa Masuala ya Afya wa Gazeti la Mwananchi, anasema:
herieth-2.png
“Nazungumza kama mdada, mwanamke, mwandishi na mwanajamii kutoka mtaani, kuna matumizi mengi ya vidonge vya P2, matumizi ya Dawa za Misoprostol, ambazo zinatumika kutoa mimba katika njia ambazo si sahihi kiafya, madhara yakishakuwa makubwa Serikali inaingia gharama kuwatibu waathirika hospitalini.

“Pia kuwa na mimba ambayo imeingia kwa kulazimishwa ni mbaya kisaikolojia.

“Kabla hatujafika hatua ya kuongeza vipengele vya utoaji mimba, Serikali inatakiwa iweke msisitizo wa kujikinga na ngono zembe na kuhusu elimu ya uzazi hasa kwa vijana ambao miili yao inakuwa na mihemko.

“Baada ya hapo wafikiri kuhusu haki ya kuongeza vipengele kuhusu mimba kwa kuwa, mwili wa mtu ndio unaokuwa na dhamana ya kubeba kiumbe kwa miezi tisa, baada ya hapo yanafuata malezi, ni vema Serikali ikafikiria kuhusu hilo.”

GEORGE FRANCIS
~Mwanasheria
Anasema “Nashauri Serikali iruhusu kuongeza vigezo vya utoaji mimba, mfano mtu kabakwa inaweza kuleta kumbukumbu mbaya kwa mama mtu pindi anapokuwa na mtoto wake.

“Kumbuka pia unapoharibika kisaikolojia ndio mwanzo wa kuharibu mambo mengine pia.”

DKT. AIFELLO SICHALWE
~Mganga Mkuu wa Serikali
Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichalwe 1.jpg
Anatoa neno: “Ni kweli kutoa mimba Tanzania hairuhusiwi isipokuwa kwa sababu za kitabibu kama maisha ya mama yapo hatarini.

“Wizara ya Afya ilishatoa mwongozo wa kuhudumia wahanga wa matatizo ya kubakwa.

“Matukio hayo na yanayofanana ya kubakwa kuna huduma zinazopaswa kutolewa ndani saa 24 sawa na mwongozo zikiwamo pamoja na uzazi wa mpango ili kuzuia na kukinga mimba zisizotarajiwa.

“Sheria ipo wazi na pana ambayo ipo na imefafanuliwa mwongozo wa huduma baada ya mimba kutoka.”

Nini maoni yako kuhusu suala hili?
 
Sheria iliyopo sasa ni nzuri maana inawabana wenye nia ovu.Jamii inapaswa kuelishwa njia salama za kuzuia mimba na ikitokea dharura kama kubakwa nk basi muathirika apatiwe huduma stahiki ndani ya masaa 72 kuzuia mimba.Ila sababu za kutoa mimba ibakie kua ni kwa sababu za kiafya za kumlinda mama mjamzito.
 
Wakatoliki wanavaliaga njuga hii ishu kana kwamba ikipitishwa watakuwa wanalazimishwa kutoa, nonsense!
 
Back
Top Bottom