City Water yatakiwa kuilipa Dawasa bilioni 14/-

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,794
287,947
Kumbe tunaweza kuyafukuza makampuni uchwara ya kigeni na bado tukashinda kesi.

City Water yatakiwa kuilipa Dawasa bilioni 14/-
Maulid Ahmed
HabariLeo; Thursday,January 10, 2008 @21:02

MAMLAKA ya Maji Safi na Maji Taka mkoani Dar es Salaam (DAWASA) imeshinda kesi dhidi ya kampuni ya City Water ya kukatisha mkataba na kampuni hiyo. Sambamba na kushinda kesi, Mahakama ya Usuluhishi ya Umoja wa Mataifa imeitaka City Water kuilipa Dawasa Sh bilioni 13.765 zikiwamo Sh bilioni 2.1 kama gharama za kesi.

Sasa Dawasa italipwa Sh bilioni 6.99 kutokana na awali kuchukua Sh bilioni saba ambazo City Water iliziweka kama dhamana. Akitoa taarifa za hukumu ya kesi hiyo iliyotolewa Desemba 31, mwaka jana, jijini London, Uingereza, na jopo la watu watatu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Patrick Rutabanzibwa alisema City Water inatakiwa kulipa fedha hizo haraka na ikichelewa italazimika kulipa riba. Kwa mwaka riba ni asilimia 14.9.

Katika hukumu hiyo ya kurasa 66, Dawasa imeonekana haikufanya kosa kufuta mkataba na City Water kama ambavyo kampuni hiyo ilivyodai wakati inafungua kesi hiyo. Serikali ilivunja mkataba na City Water Juni 2005 na kuundwa kwa kampuni ya Dawasco ambayo hadi sasa inatoa huduma za maji safi mikoani Dar es Salaam na Pwani. Ilibainika kuwa City Water ilianza kuvunja mkataba tangu Oktoba 2003, ikiwa miezi miwili baada ya kupewa mamlaka ya kutoa huduma hiyo.

“Katika hukumu hiyo imeonekana pia utendaji wa City Water haukufikia wa Dawasa, ilikiuka masharti ya msingi ya mkataba na kushindwa kuboresha na kupanua mfumo wa maji,” alifafanua Rutabanzibwa. Katika kesi hiyo ambayo iliendeshwa na jopo la majaji wawili kutoka Uingereza na mmoja kutoka Marekani, Dawasa ilikuwa ikitetewa na kampuni ya uwakili ya Mkono kwa kushirikiana na kampuni ya Freshfield ya Uingereza.

Katika kesi nyingine, kampuni ya BiWater Gauff (Tanzania) Ltd, imeishitaki serikali katika Mahakama ya Usuluhishi ikidai serikali imetaifisha mali zake. Kesi hiyo iliyofunguliwa mwaka 2005 inaendelea katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi The Hague nchini Uholanzi. BiWater ambayo ilikuwa na hisa nyingi katika City Water, inaidai serikali ya Tanzania fidia ya Dola za Marekani milioni 25.

Rutabanzibwa alisema mpaka sasa katika kesi zote mbili serikali imeshatumia Sh bilioni tano na kuongeza, “katika kesi zote tunadaiwa tulipe shilingi bilioni 30, hivyo kwa sababu tumeshitakiwa tusingeweka mawakili wetu tungelipa fedha hizo. Imetulazimu kuweka mawakili ili tuokoe fedha kama tulivyoweza kuokoa katika kesi ya kwanza baada ya kushinda.”

Copyright @TSN 2006 All Rights Reserved
 
Rutabanzibwa alisema mpaka sasa katika kesi zote mbili serikali imeshatumia Sh bilioni tano na kuongeza, “katika kesi zote tunadaiwa tulipe shilingi bilioni 30, hivyo kwa sababu tumeshitakiwa tusingeweka mawakili wetu tungelipa fedha hizo. Imetulazimu kuweka mawakili ili tuokoe fedha kama tulivyoweza kuokoa katika kesi ya kwanza baada ya kushinda.”

Nadhani huyu jamaa kweli naye ni fisadi. Sentensi hiyo haonyeshi uamainifu wowote, inatia picha ya kulazimisha uhalali wa matumizi ya Sh Bilioni tano.
 
Hapa ndio unashangaa watendaji wa $erikali yetu, hawajui kabisa kuangalia ishara za nyakati! Huyu bwana hakupaswa kuongelea mambo ya "figures" kama alikuwa hajaandaa "breakdown"; sasa anataka sisi tumpe benefit of doubt?

Watendaji wa $erikali, please you should learn how to win the public. Its a shame to believe pipo will accept such huge expenditure without breakdown (accountability)!! Au mpaka muundiwe TUME?! Hawa watu wamesoma wapi???!!!!
 
Nadhani huyu jamaa kweli naye ni fisadi. Sentensi hiyo haonyeshi uamainifu wowote, inatia picha ya kulazimisha uhalali wa matumizi ya Sh Bilioni tano.
Mambo yakiwekwa wazi lawama, yakifichwa lawama...!MMhm kazi kwelikweli
 
Dawasa ilikuwa ikitetewa na kampuni ya uwakili ya Mkono kwa kushirikiana na kampuni ya Freshfield ya Uingereza.

Aliyeshinda Mkono! Hivi kwenye kesi hiyo nyingine nani anatuwakilisha? Hao jamaa wa AG Chambers walishindwa kweli kutafuta kampuni ya nje kushirikiana nayo kama anayvofanya Mkono? Pengine tufanye uamuzi AG Chambers ifutwe au ipunguzwe ukubwa na kesi zote i-outsource kwa njia iliyo wazi.
 
Mambo yakiwekwa wazi lawama, yakifichwa lawama...!MMhm kazi kwelikweli
Hakuweka mambo wazi, ama sivyo nisengetia shaka. Ameficha mengi katika taarifa yake, ndiyo maana anatafuta namna ya kuyahalalisha. Nadhani labda wewe huoni kuwa statement zake zina upungufu.
 
Kumbe tunaweza kuyafukuza makampuni uchwara ya kigeni na bado tukashinda kesi.

City Water yatakiwa kuilipa Dawasa bilioni 14/-
Maulid Ahmed
HabariLeo; Thursday,January 10, 2008 @21:02

MAMLAKA ya Maji Safi na Maji Taka mkoani Dar es Salaam (DAWASA) imeshinda kesi dhidi ya kampuni ya City Water ya kukatisha mkataba na kampuni hiyo. Sambamba na kushinda kesi, Mahakama ya Usuluhishi ya Umoja wa Mataifa imeitaka City Water kuilipa Dawasa Sh bilioni 13.765 zikiwamo Sh bilioni 2.1 kama gharama za kesi.

Sasa Dawasa italipwa Sh bilioni 6.99 kutokana na awali kuchukua Sh bilioni saba ambazo City Water iliziweka kama dhamana. Akitoa taarifa za hukumu ya kesi hiyo iliyotolewa Desemba 31, mwaka jana, jijini London, Uingereza, na jopo la watu watatu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Patrick Rutabanzibwa alisema City Water inatakiwa kulipa fedha hizo haraka na ikichelewa italazimika kulipa riba. Kwa mwaka riba ni asilimia 14.9.

Katika hukumu hiyo ya kurasa 66, Dawasa imeonekana haikufanya kosa kufuta mkataba na City Water kama ambavyo kampuni hiyo ilivyodai wakati inafungua kesi hiyo. Serikali ilivunja mkataba na City Water Juni 2005 na kuundwa kwa kampuni ya Dawasco ambayo hadi sasa inatoa huduma za maji safi mikoani Dar es Salaam na Pwani. Ilibainika kuwa City Water ilianza kuvunja mkataba tangu Oktoba 2003, ikiwa miezi miwili baada ya kupewa mamlaka ya kutoa huduma hiyo.

“Katika hukumu hiyo imeonekana pia utendaji wa City Water haukufikia wa Dawasa, ilikiuka masharti ya msingi ya mkataba na kushindwa kuboresha na kupanua mfumo wa maji,” alifafanua Rutabanzibwa. Katika kesi hiyo ambayo iliendeshwa na jopo la majaji wawili kutoka Uingereza na mmoja kutoka Marekani, Dawasa ilikuwa ikitetewa na kampuni ya uwakili ya Mkono kwa kushirikiana na kampuni ya Freshfield ya Uingereza.

Katika kesi nyingine, kampuni ya BiWater Gauff (Tanzania) Ltd, imeishitaki serikali katika Mahakama ya Usuluhishi ikidai serikali imetaifisha mali zake. Kesi hiyo iliyofunguliwa mwaka 2005 inaendelea katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi The Hague nchini Uholanzi. BiWater ambayo ilikuwa na hisa nyingi katika City Water, inaidai serikali ya Tanzania fidia ya Dola za Marekani milioni 25.

Rutabanzibwa alisema mpaka sasa katika kesi zote mbili serikali imeshatumia Sh bilioni tano na kuongeza, “katika kesi zote tunadaiwa tulipe shilingi bilioni 30, hivyo kwa sababu tumeshitakiwa tusingeweka mawakili wetu tungelipa fedha hizo. Imetulazimu kuweka mawakili ili tuokoe fedha kama tulivyoweza kuokoa katika kesi ya kwanza baada ya kushinda.”

Copyright TSN 2006 All Rights Reserved

Sasa mbona watanzania wanaogopa kumbe mambo yanawezekana kanisa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom