Uwajibikaji katika mahakama za masuala ya kazi (CMA) juu ya unyanyasaji kwa wafanyakazi sekta binafsi

TricyLove

New Member
May 7, 2024
2
0
Hii kero inaumiza sana hasa wafanyakazi kupata haki zao pamoja na kupotezewa muda. Kuna Kampuni ya madini Kahama mkoani Shinyanga inajihusisha na uchimbaji wa madini, imetelekeza wafanyakazi bila chochote si malimbikizo ya mishahara, barua za kuvunja mkataba wala hela za NSSF, pia makato mengi ya NSSF hayakuwa yanapelekwa.

Wafanyakazi wamefungua kesi baraza la usuluhishi (CMA) hadi hukumu ikatoka wameshinda kesi lakini hawajalipwa pesa licha ya wafanyakazi hao kukazia hukumu mahakama kuu Shinyanga bado haikusaidia wao kulipwa.

Familia za wafanyakazi hao toka mwaka 2022 hadi sasa zinateseka wapo waliohamia wilayani hapo kutoka mikoa mingine, hakuna uwajibikaji na mahakama ya usuluhishi ni kama ipo upande wa mshitaki ikiwa wafanyakazi zaidi ya 25 wamesha ambatanisha hadi mikataba yao ili kupata haki zao. Kampuni hii inaitwa Aral hadi sasa haijawajibishwa
 
Back
Top Bottom