Citizenship Vs Nationality tofauti ni nini?

Kang

JF-Expert Member
Jun 24, 2008
5,495
2,252
Kwenye ippmedia kuna habari kuwa Masha amesema vitambulisho vya taifa vitaonyesha Nationality but not Citizenship. Kwa kuangalia kamusi yangu inaelekea hakuna tofauti kati ya vitu hivyo, naomba mtu anielimishe. Pia kama kuna mtu anajua alichosema Masha kwa kiswahili ntashukuru.
 
Nationality = utaifa. Mara nyingi utaifa uko defined na geographical location/boundries, ethinic composition, shared history na culture....nk.

Citizenship = uraia. Uraia 100% uko defined na dola (state) ama nchi. Kwa maana hii dola/nchi ndio inayotambua uraia wako sio taifa.

Kwasababu nchi/dola nyingi duniani zilianzia na taifa (nation-state), ndipo mchanganyo wa maneno ya nationality na citizenship unapoingia. Lakini haya ni maneno mawili yenye dhana mbili tofauti.

Utofauti wa nationality na citizenship unafuata mkondo wa utofauti kati ya TAIFA na NCHI (nation and state).

Hopeful this helps
 
Last edited:

Sijakupata vizuri. Labda ni situation gani inaweza kupelekea mtu kuwa na Nationality na Citizenship tofauti?
 
Sijakupata vizuri. Labda ni situation gani inaweza kupelekea mtu kuwa na Nationality na Citizenship tofauti?

Nelson Mandela ni wa taifa la South Africa na ana uraia wa Canada. Kadhalika Obama anaweza kupata uraia wa Kenya huku akiwa na utaifa wa USA. Wakimbizi wanaoishi Tz sio wa taifa la Tz kwa maana chimbuko lao sio Tz (e.g hawana historia kama ya Tz, Taifa lao lina mipaka inayokubalika kimataifa...nk), nao wanaweza kuwa raia mara Tanzania kama nchi/dola inapoamua hivyo.

Cha muhimu kukumbuka hapa ni kwamba URAIA ni HAKI YA KISHERIA, na UTAIFA ni HAKI ya KICHIMBUKO. Unaweza kunyang'anywa uraia, lakini huwezi kunyang'anywa utaifa (chimbuko).
 
turudi kwenye topic kwahio hivi vitambulisho watapewa watu wote waliokuwa nchini hili kuweza kutambua nationality zao na sio kwa watanzania peke yao au? kutokana na tofauti ya citizenship na nationality kama alivyochambua mgonja wa ukimwi.
 
Kama ndo hivyo basi utaifa sio sawa na Nationality. "status of belonging to a particular nation by birth OR naturalization" ndo nationality so Mandela ana nationality ya Canada. Kwa hiyo kitambulisho cha mmarekani aliyepata uraia wa Tanzania kitaonesha kuwa ni mmarekani? Mbona haijakaa sawa hiyo.
 
Nationality = utaifa. Mara nyingi utaifa uko defined na geographical location/boundries, ethinic composition, shared history na culture....nk.

Citizenship = uraia. Uraia 100% uko defined na dola (state) ama nchi. Kwa maana hii dola/nchi ndio inayotambua uraia wako sio taifa.

Kwasababu nchi/dola nyingi duniani zilianzia na taifa (nation-state), ndipo mchanganyo wa maneno ya nationality na citizenship unapoingia. Lakini haya ni maneno mawili yenye dhana mbili tofauti.

Utofauti wa nationality na citizenship unafuata mkondo wa utofauti kati ya TAIFA na NCHI (nation and state).

Hopeful this helps
kwa mfano kama nimepata uraia wa marekani,katika kupita pita nikakutana na form inaniulizia nationality yangu,kwahio nijaze tanzania?
 
Utaifa ni mmoja tu, yaani asili ya mtu. Uraia unapatikana kwa njia nyingi. Mtu anaweza kuwa na uraia hata wa nchi mbili au tatu kulingana na sheria za nchi mbalimbali. Hapa kwetu uraia ni mmoja tu: au uko Mtanzania au mtu wa nchi nyingine. Uraia mtu anaweza kuupoteza.

Utaifa , huwezi kuupoteza hata kama ukipoteza uraia. Ndo mana unasikia mtu anasema: "fulani ni mtanzania mwenye asili ya India, nk", yaani ni raia wa Tanzania ambaye kwa chimbuko lake ni kutoka India.
 
National Identity Cards, whose project is under way, will be issued to Tanzanians for the purpose of identifying their "nationality" not "citizenship," the government clarified in the National Assembly yesterday.

Hapa serikali imechemsha ile mbaya, tangu lini wageni ambao wanaishi nchini kwa muda wakatambuliwa kama wana Utaifa katika nchi wanayoishi? Hii Serikali haijui itendalo kwasababu hakuna tofauti yoyote ile ya 'nationality' na citizenship'. Ni mameno mawili tofauti lakini maana yake ni ile ile.
 
Tofauti ipo kati ya citizenship na nationality. Citizenship is the country that you have legal rights to live and Nationality is the state of Origin.
 
Tofauti ipo kati ya citizenship na nationality. Citizenship is the country that you have legal rights to live and Nationality is the state of Origin.
Pakawa kwa kukuunga mkono, kwenye suala hili nitoe mfano mmoja hapa.
Kuna hawa ndugu, jamaa na marafiki zetu walio ondoka nchini na kuamua kuishi nchi kama Uingereza, Ireland au Canada. Uko walipo wamejipa utaifa wa Nchi zingine zenye machafuko, kama vile Somalia, Burundi nk.

Pale wanapokubaliwa kuwa wao ni wakimbizi, Vitambulisho vyao vinaonyesha: Nationality: Somali or Burundi nk. Lakini Citizenship yao ni hapo walipo.
Na hata wanapo pata Passport zinaonyesha asili ya nchi walizo dai wanatoka.
 
Tofauti ipo kati ya citizenship na nationality. Citizenship is the country that you have legal rights to live and Nationality is the state of Origin.

That's just incorrect dictionary.com definition of nationality:
"the status of belonging to a particular nation, whether by birth or naturalization".

immigration.com definition "The country of a person’s citizenship or country in which the person is deemed a national." Therefore nationality is the same as Citizenship.

I think the word ippmedia was looking for is maybe "Nativity" ="birth with reference to place or attendant circumstances: of Irish nativity. ".

But that still doesn't make any sense on Masha's part, why would the national ID show a persons nativity and not his Nationality/Citizenship??
 
Pakawa kwa kukuunga mkono, kwenye suala hili nitoe mfano mmoja hapa.
Kuna hawa ndugu, jamaa na marafiki zetu walio ondoka nchini na kuamua kuishi nchi kama Uingereza, Ireland au Canada. Uko walipo wamejipa utaifa wa Nchi zingine zenye machafuko, kama vile Somalia, Burundi nk.

Pale wanapokubaliwa kuwa wao ni wakimbizi, Vitambulisho vyao vinaonyesha: Nationality: Somali or Burundi nk. Lakini Citizenship yao ni hapo walipo.
Na hata wanapo pata Passport zinaonyesha asili ya nchi walizo dai wanatoka.

Nadhani hao hawajapewa Citizenship, wamepewa Refugee asylum ndo maana inaonyehsa hivyo ID yao.
 
Kama ni kweli kwamba utaifa na uraia ni vitu viwili tofauti, na kama ni kweli kuwa serikali itatoa vitambulisho kwa watu wenye utaifa na si uraia wa Tanzania. Ndiyo kusema hata wale wote waliokwishaukana uraia wa Tz na kuchukuwa uraia wa nchi nyingine (kama sheria zetu zinavyotaka) nao wanatakiwa wapewe vitambulisho, maana uraia wao ni mwingine lakini utaifa wao bado ni wa Tz. Na wale wote raia wa Tz wenye asili ya nchi nyingine (kama wenye asili ya Asia, mashariki yati na hata nchi jirani) hawatakiwi kupewa vitambulisho hivyo maana utaifa wao (asili yao) si wa Tz.
Nadhani hapa kuna kuchemsha...
 
Nationality usually describes the country where you were born.

Citizenship is a legal matter, that you have been registered with the government of a country as having rights as a full citizen in that country. For most people, that is the country where they are born and continue to live, but if a person moves to another country, citizenship may be obtained in the new country, by applying to the government.

Residence is the place where you have a permanent residence, where you spend most of your time during a year.

So a person who is born in England, moves to Canada as a child and applies to Canada for citizenship, then spends time in France as a teacher, for example, could have English nationality, Canadian citizenship and French residence.
 
Hata kwenye zao passport mkuu.

kwenye pasport ya kiingereza hawaandiki nchi uliyotoka,wanaandika nationality;british citizen,mke wangu ni mbongo lakini ana pasport ya UK na hakuna sehemu kwenye pasport yake waliyoandika asili yake
 
Kwanza kwenye passport hakuna sehemu inasema CITIZEN au CITIZENSHP. Kuna inayosema NATIONALITY tu.
 
Lakini SMZ wamesha sema Hivyo vitambulisho vyenu mwisho wake chumbe .
 
Pakawa kwa kukuunga mkono, kwenye suala hili nitoe mfano mmoja hapa.
Kuna hawa ndugu, jamaa na marafiki zetu walio ondoka nchini na kuamua kuishi nchi kama Uingereza, Ireland au Canada. Uko walipo wamejipa utaifa wa Nchi zingine zenye machafuko, kama vile Somalia, Burundi nk.

Pale wanapokubaliwa kuwa wao ni wakimbizi, Vitambulisho vyao vinaonyesha: Nationality: Somali or Burundi nk. Lakini Citizenship yao ni hapo walipo.
Na hata wanapo pata Passport zinaonyesha asili ya nchi walizo dai wanatoka.

sasa hao wazungu hawalijuwi hilo la kudanganywa ?au ndio mana hata serekali yetu huwadanganya hao wazungu kwa ujuha wao na kuleta pesa zao kwa wingi hapa TANZANIA na sisi kunufaika huku wakiwacha baadhi ya watu wake kuwa homeless .
 
Back
Top Bottom