Chura aua Msambaa

aduwilly

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
1,176
305
Msambaa mmoja alikuwa amepakia plastiki la maziwa kwenye baiskeli kupeleka lushoto mjini kuuza, kwa kuwa ilikuwa kipindi cha mvua, madimbwi yalikuwa ni mengi huku barabara ikiteleza sana, basi kufika njiani baiskeli ikayumba na kumwangusha. Bahati mbaya maziwa yakamwagikia kwenye dimbwi la maji na kufanya maji yote yawe na rangi ya maziwa.
Yule msambaa alipokuwa amesimama pembeni akitafakari itakuwaje mara akamsikia chura akilia toka kwenye dimbwi ambalo maji yake yanaonekana kama yote ni maziwa "Nywaa, nywaa, nywaa" na kwa kuwa nywaa kwa kisambaa ni "kunywa" basi yule msambaa akajibu "ehee nanywa mgosi"
Akaanza kunywa yale maji-maziwa, kila akiacha anamsikia chura akilia "Nywaa, nywaa, nywaa" msambaa anajibu tena "ehee nanywa mgosi" akanywa mpaka akapoteza fahamu, raia kuja kumkuta pale na kumpeleka hospitali, akafia njiani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom