Mimi ninakubaliana na wewe asilimia mia moja kuwa hujatembea na huyo dada...hilo ninaamini toka moyoni, lakini kiuhalisia huko mnapoendelea mbeleni na hasa kama mkeo asingekuwa anapiga kelele ungetembea nae tu.
Mkuu ukiingia kwenye ndoa unaanza maisha mapya, inawezekana huko nyuma ulikuwa na njia zako za kuishi ila ukiwa katika ndoa kama hizi njia za maisha yako ya nyuma zinamkera mwenzio huna budi kuacha... ukiwa katika ndoa lazima ukubari kupoteza vitu flan na mambo flan flan ambayo ulikuwa unayapanda lakini mwenzio sasa anayaona ni kikwazo.
Mkeo amesahonyesha kuwa anawasiwasi na huyo dada, kinachokufanya uwe nae karibu ni nini? ni nini utakosa ukiwa nae mbali mkawa mnasalimiana tu? sasa kung'ang'ania kwako kuwa nae karibu ndio kutimiza hayo ya hapo juu, bado unang'ang'ania maisha ya zamani ambayo ni kikwazo kwa umpendaye? kwa maana nyingine upo tayari mkeo akereke huku wewe na huyo mdada mkiendeleza ukaribu mlionao...hapa hutendi haki kaka, na ndo maana nlitanguliza kusema hujatembea nae ila huko mbeleni inawezekana mkadoo...kama hamna hilo wazo kwako kwa nini kumng'ang'ania?
Acha hizo kama, angalia ndoa yako..makapi yasiyo na msingi ambayo yanaharibu umbo la ndoa lako yapepete.. achana na huyo dada, acha ukaribu nae.. muwe mnasalimiana tu then uone kama hilo zogo litaendelea...
"MWANAUME MPUMBAVU HUVUNJA NDOA KWA MIKONO YAKE MWENYEWE"