Chupi imeleta kizaazaa

Chupi imeleta kizaazaa

Mimi ninakubaliana na wewe asilimia mia moja kuwa hujatembea na huyo dada...hilo ninaamini toka moyoni, lakini kiuhalisia huko mnapoendelea mbeleni na hasa kama mkeo asingekuwa anapiga kelele ungetembea nae tu.

Mkuu ukiingia kwenye ndoa unaanza maisha mapya, inawezekana huko nyuma ulikuwa na njia zako za kuishi ila ukiwa katika ndoa kama hizi njia za maisha yako ya nyuma zinamkera mwenzio huna budi kuacha... ukiwa katika ndoa lazima ukubari kupoteza vitu flan na mambo flan flan ambayo ulikuwa unayapanda lakini mwenzio sasa anayaona ni kikwazo.

Mkeo amesahonyesha kuwa anawasiwasi na huyo dada, kinachokufanya uwe nae karibu ni nini? ni nini utakosa ukiwa nae mbali mkawa mnasalimiana tu? sasa kung'ang'ania kwako kuwa nae karibu ndio kutimiza hayo ya hapo juu, bado unang'ang'ania maisha ya zamani ambayo ni kikwazo kwa umpendaye? kwa maana nyingine upo tayari mkeo akereke huku wewe na huyo mdada mkiendeleza ukaribu mlionao...hapa hutendi haki kaka, na ndo maana nlitanguliza kusema hujatembea nae ila huko mbeleni inawezekana mkadoo...kama hamna hilo wazo kwako kwa nini kumng'ang'ania?

Acha hizo kama, angalia ndoa yako..makapi yasiyo na msingi ambayo yanaharibu umbo la ndoa lako yapepete.. achana na huyo dada, acha ukaribu nae.. muwe mnasalimiana tu then uone kama hilo zogo litaendelea...

"MWANAUME MPUMBAVU HUVUNJA NDOA KWA MIKONO YAKE MWENYEWE"
 
sasa fanya kweli kabisa maana hapo utakosa vyote...wife na huyo mpangaji mpya. pole lkn wa kufua chupi ya asiye kuhusu. wife wako huwa unamfuluia lkn?
 
hiyo imekaa kikomedi hivi hyo bafu haikuwa na mlango mpaka mkeo anakuja direct then ww hata hukuhc kama mtu anakuja maana chupi ya kike mtu akiona umeishika unakuelewa vingine
 
....basi nikiwa naisuuza ile chu pi mke wangu akaingia maliwatoni na kunikuta nikiisuuza ile chupi ya mpangaji mwenzetu....
Kuna maswali kadhaa yanahitaji ufafanuzi:
1.Ulijuaje ile chupi ni ya nani kama nyumba ni ya kupanga na lazima kuna wanawake kadhaa ?
2. Mkeo aliingiaje toilet kwani hamna mlango ? au ni zile za kuning'inia gunia ?
3.Mkeo aliwezaje kuihusisha chupi ile na yule mpangaji haraka hivyo ikiwa mkononi kwako imeloa/kunjika ?
 
nawe kweli WASHAWASHA mana una kisebu sebu hiyo chupi uliishika ya nini??????????
 
Ukilog off uondoke kabisa! Hako ka-nalog off kako kananikera kila nkisoma post zako! Aaagh! Nalog off! Lol!
 
Mi namshauri huyo mkeo asirudi kuishi tena na wewe maana 100% unaonekana sio mwaminifu ulishaonywa mara kibao ila still unajidai kuonyesha upendo kwa mwanamke baki wakati kwa mkeo hujawahi kuuonyesha.. kwa hali hii Wanaume tutaendelea kushika namba 1 ya kucheat.

Na Login
 
Baba huo mzigo kuna dalili kuwa umechapa na kama huja uchapa kulikuwa na kila dalili ya si muda mrefu unge uchapa. Lakini mwishoni nimekupata tena umesema dada huyo yupo cngo na hujazoea kulala peke yako. Muombe huyo dada akupe hifadhi ya muda hadi mama watoto atakapo rudi.
Inachekesha kidogo inaonekana haupo serious na mkeo. Je ingetokea hivyo kwa mkeo si ungesha mng'oa meno.
 
Baba huo mzigo kuna dalili kuwa umechapa na kama huja uchapa kulikuwa na kila dalili ya si muda mrefu unge uchapa. Lakini mwishoni nimekupata tena umesema dada huyo yupo cngo na hujazoea kulala peke yako. Muombe huyo dada akupe hifadhi ya muda hadi mama watoto atakapo rudi.
Inachekesha kidogo inaonekana haupo serious na mkeo. Je ingetokea hivyo kwa mkeo si ungesha mng'oa meno.
Naunga mkono hoja
 
Nimecheka sana hapa.maana mpangaj mwenzangu ni bachela nae akifua kuful zake huzianika nje,mvua ikinyesha na acpokuwepo huwa napata wakat mgumu sana!NIMUANULIE?au niziache?

imeandikwa mpende jirani yako.
 
Haya mabafu ambayo ni ya ku-share na milango haina makomeo kaaz kwel!

Au ulifanya kusudi kutofunga mlango ili jirani aje kuchukua chupi yake?

Ha ha ha haa!
Hapana sikufanya kusudi ila kuanguka kwa hii chu pi kumeniharibia sana.

Nalog off
 
Vituko vya duniani na wewe. Unaonaje ungeokota ile chupi ukaitundika mlangoni bila kufua. Obvious una mahusiano nae mpaka chupi yake ikakuvutia kuishika na kufua.

Hama hiyo nyumba, mfuate mkeo huko alikoenda umrudishe, akikataa kurudi njoo kwangu mimi nitakupokea.
Hapana CD huyu binti chu pi yake ilianguka sasa ningeiacha angeniletea uzushi,nikaamua kufanya ustaarabu kwa kuisuuza. Nakwenda kuangukia nikitoswa nitaku PM.

Nalog off
 
Habari zenu wana JF,

Ni hivi mimi naishi nyumba ya kupanga na my wife wangu na kuna wapangaji wengine katika nyumba hiyo,sasa kuna binti single kahamia katika chumba kimoja katika hii nyumba,basi baada ya kuzoeana naye mke wangu anasema hamuamini ingawa nimemuhakikishia kuwa sijafanya naye mapenzi wala sifikirii,basi mke wangu akaanza kumletea vituko huyu binti mpaka wakagombana na hapa niandikapo ni kuwa hawaelewani.

Sasa tatizo leo hii yule binti kaingia maliwatoni na kuacha chu pi yake akining'inia nyuma ya mlango.

Basi mke wangu naye akaenda kuniwekea maji maliwatoni ili nikakoge,basi nilipoingia nikaiona ile chupi nyuma ya mlango na mie kuanza kujimwagia maji baridi.

Lakini nikiwa naendelea kukoga ile chupi ikaanguka kwenye yale maji ambayo ni machafu,basi nikaona ngoja niisuuze ili niirudishe tena nyuma ya mlango na nimtaarifu mwenye chu pi kwa kilichotokea,basi nikiwa naisuuza ile chu pi mke wangu akaingia maliwatoni na kunikuta nikiisuuza ile chupi ya mpangaji mwenzetu,basi likaanza bonge la zogo na kuniambia kuwa kumbe yule mpangaji mwenzangu nina uhusiano naye yaani mpaka chu pi namfulia!basi yeye kaamua kurudi kwao.

Nyumba ina wapangaji wengi wakiwamo Wanawake, labda kama wanawake katika nyumba hiyo ni mkeo na huyo mdada ndio wanawake pekee. Kama kuna Wanawake wengine ndani ya hiyo nyumba ulijuwaje kama hiyo chupi ni huyo mdada?
 
Back
Top Bottom