Chupi imeleta kizaazaa

Chupi imeleta kizaazaa

Hayawi hayawi, yamekua.

Kumbe ndio amedondokea kuwa Nyumba yako ndogo!

Hongera sana Kiongozi
 
Mke wako hajakua Bado. ILA na wewe Du mambo ya kufua vyupi vya watu tena Dah! Ushawahi kufua ya Mke wako? Kama hapana hapo ulikosea sana. Na ulijuaje kama ni ya huyo binti hadi kuifua? Hapo una lakujibu boss. Endelea kumbembeleza Mke atarudi tu. Akigoma chukua huyo single atakufaa.
 
Habari zenu wana JF,

Ni hivi mimi naishi nyumba ya kupanga na my wife wangu na kuna wapangaji wengine katika nyumba hiyo,sasa kuna binti single kahamia katika chumba kimoja katika hii nyumba,basi baada ya kuzoeana naye mke wangu anasema hamuamini ingawa nimemuhakikishia kuwa sijafanya naye mapenzi wala sifikirii,basi mke wangu akaanza kumletea vituko huyu binti mpaka wakagombana na hapa niandikapo ni kuwa hawaelewani.

Sasa tatizo leo hii yule binti kaingia maliwatoni na kuacha chu pi yake akining'inia nyuma ya mlango.

Basi mke wangu naye akaenda kuniwekea maji maliwatoni ili nikakoge,basi nilipoingia nikaiona ile chupi nyuma ya mlango na mie kuanza kujimwagia maji baridi.

Lakini nikiwa naendelea kukoga ile chupi ikaanguka kwenye yale maji ambayo ni machafu,basi nikaona ngoja niisuuze ili niirudishe tena nyuma ya mlango na nimtaarifu mwenye chu pi kwa kilichotokea,basi nikiwa naisuuza ile chu pi mke wangu akaingia maliwatoni na kunikuta nikiisuuza ile chupi ya mpangaji mwenzetu,basi likaanza bonge la zogo na kuniambia kuwa kumbe yule mpangaji mwenzangu nina uhusiano naye yaani mpaka chu pi namfulia!basi yeye kaamua kurudi kwao.

Yule mpangaji mwenzetu ikabidi nimuambie jinsi ilivyokuwa ili amuaminishe mke wangu kuwa hakunipa nimfulie ile chu pi yake,lakini yule binti mpangaji mwenzetu kagoma kuongea na mke wangu kwa madai kuwa mke wangu anaringa sana.

Jamani nimechanganyikiwa sijazoea kulala peke yangu.

Nalog off
Usivae chupi Kwan lazima
 
Mke wako hajakua Bado. ILA na wewe Du mambo ya kufua vyupi vya watu tena Dah! Ushawahi kufua ya Mke wako? Kama hapana hapo ulikosea sana. Na ulijuaje kama ni ya huyo binti hadi kuifua? Hapo una lakujibu boss. Endelea kumbembeleza Mke atarudi tu. Akigoma chukua huyo single atakufaa.
Teyari mke wangu kasharudi na mrembo mwenye chupi amekuwa nyumba ndogo
Nalog off
 
Back
Top Bottom