Chupa za plastic kwa ajili ya juice

ipyax

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
4,147
6,521
Habari wapendwa wa jamii forums, nina hitaji chupa za plastic kwa ajili ya juice za size kama ya chupa za azam energy, MO chungwa nk. Kama kuna mtu anaweza nishauri sehemu ya kuzipata au anauza itakua msaada mkubwa sana kwangu.
 
Kama sijakuelewa hivi mkuu.

Ni chupa ambazo zimeshatumika au unataka kutengenezewa kabisa kutoka kiwandani...?

Dadavua uzuri mkuu. Thanks.
 
Mkuu vifungashio vilivyopo ni vile disposable ambavyo huwa vinawekwa juicy lakini ukitaka chupa kabisa kama za kina Azam, Mo, Sayona na Jambo ni mpaka uende viwandani wakutengenezee - So hapo inategemea na mtaji wako au else uamue kutumia "Used" ingawa hadhi yake ni ndogo kwa watu wa kipato cha kati au watu sensitive kuhusu Afya zao
 
Nahitaji mpya toka kiwandani mkuu.
 
Mkuu vifungashio vilivyopo ni vile disposable ambavyo huwa vinawekwa juicy lakini ukitaka chupa kabisa kama za kina Azam, Mo, Sayona na Jambo ni mpaka uende viwandani wakutengenezee - So hapo inategemea na mtaji wako au else uamue kutumia "Used" ingawa hadhi yake ni ndogo kwa watu wa kipato cha kati au watu sensitive kuhusu Afya zao
Kutumia chupa used ni ngumu kwangu kutokana na soko ambalo nimelenga kulihudumia. Kama unafaham kiwanda cha chupa unaweza nielekeza niende huko moja kwa moja pia.
 
Nenda Kipawa kuna Kiwanda Kimeandikwa OPIL - Omar Packaging Industries Limited - Ni kiwanda cha Bakheresa na kinazalisha mara nyingi ni vifungashio vyake mwenyewe. Nenda ukaongee nao, hata mimi ninataka pia ingawa sijawahi kwenda kuulizia gharama zao - Ukipewa majibu usinisahau kuhusu Feedback !
 
Poa mkuu, asante sana.
 
Mkuu nimeenda kipawa kwenye hicho kiwanda cha bakhressa, MO nimeambiwa hawauzi chupa kwani wao wanatengeneza kwa ajili ya viwanda vya vya vinywaji.
 
Kama wanatengeneza kwa ajili ya vinywaji kwani wewe unataka kuweka kitu gani kwenye hizo chupa mkuu...?

Kama wanatengeneza si ungeweka order kwa sababu maelezo yako umesema hutaki used unataka kutengeneza zako kwa nini usiwaambie ukatengenezewa mkuu...?

Kama sjakuelewa hivi.
 
Wanatengeneza chupa kwa ajili ya viwanda vyao tu mkuu.
 
Mkuu nimeenda kipawa kwenye hicho kiwanda cha bakhressa, MO nimeambiwa hawauzi chupa kwani wao wanatengeneza kwa ajili ya viwanda vya vya vinywaji.
Okay - Jaribu na MURZAH pia wana kiwanda, Ni hapo hapo Kipawa
 
Unataka kuwekea pombe zilizopo kwenye viroba au vp funguka tukupe mbinu
 
Back
Top Bottom