Chupa mpya, mvinyo ule ule...(?)

kitu ambacho nimeshindwa kujirekebisha kabisa kwenye ni "kinyongo" huwa nina kinyongo sana esp nijue kabisa hapa nadanganywa na nina hakika unanidanganya then hutki kuniambia ukweli bado mbishi tu na bac hapo kinyongo changu hakiishi, ukitaka kiishe niambie ukweli, eg wakati ule nilipomfumania alianza maelezo akitanguliza uongo uongo fulani kujitetea nilimshikia bango na ndio ingekuwa mwisho wetu ule lakini alivyosema ukweli roho ilitulia na kinyongo kikaisha, cpengi kudanganywa nikijua nadanganywa...kitu kingine ni "ukali" hili watu wengi esp mr huwa ananiambia mie mkali, lakini kila mwenzangu anaponiambia nipunguze cjijui naupunguzia wapi au nianzie wapi, hapa cjuagi kabisa nifanyaje....kingine ni kulalamikiwa bila sababu maalum, mr ana ile tbia kama akikucal/sms umeshindwa kujibu kwa wakati maalum bac hapo tatizo tayari, ntahicwa/shutumiwa kwa kila aina ya jambo.

Sasa mpenzi duh.............Mr ana-cope vipi na hili lako?? hasa ukali maana hilo la kinyongo ataavoid kwa kuwa mkweli but la ukali??!!
 
safi sana kwa comments,ila mtihani upo hapo kwenye kujishusha yaan mmoja kukubali tabia za mwenzake na kuendelea nazo ivyo ivyo zilivyo hata kama ni kero kwake
 
Mie kwakweli na hasira za haraka limenifanya mara nyingi nionekane mkorofi,lakini huwa sijui kuweka kinyongo nikikasirika ntakwambia na ndio imeisha huwezi nisikia nakumbushia makosa yaliyopita.

sasa sijui na hii ni tabia mbaya na imenishinda kuacha kabisa, huwa napenda kuwa muwazi sana kwa mweza wangu wakati mwingine huwa najikuta nimemueleza vitu ambavo nahisi sikutakiwa kusema,ukikuta sio muelewa basi ndo kinabebewa bango mwaka wote.

Napenda sana kuwa na marafiki zangu na wakati mwingine huwa nasahau kuaga basi tifu lake, taratibu siku izi nimejifunza kuaga ingawa wakati mwingine bado najisahau.
 
Sipendi kununa na sipendi kununiwa wajameni! napenda kuwa na furaha wakati wote, ikitokea naichukulia kama changamoto tu
 
Nathamini sana napokuwa naagwa,
jaribu tu kusema hata kwa ufupi tu.................
usiondoke kimya kimya kwani kwa kufanya hivyo,
wengine tunaona kama umetudharau/hutujali...............
dada yako nae nyumbani ana tabia hii kwakweli!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
kiukweli tunagombana sana kwenye hili, lakini maisha inabidi yaendelee kusonga!!!
 
Sipendi kununa na sipendi kununiwa wajameni! napenda kuwa na furaha wakati wote, ikitokea naichukulia kama changamoto tu

mbaya zaidi ukutane na yule anaejua kununa, na kusonya kuliko pitiliza lol...
 
Yani Bacha huo mtabia mbaya sana sijui niliutoa wapi.Najitahidi sana kujirekebisha siku hizi hata nikienda dukani mtaa wa pili basi namtumia sms kama yupo kazini.

Nathamini sana napokuwa naagwa,
jaribu tu kusema hata kwa ufupi tu.................
usiondoke kimya kimya kwani kwa kufanya hivyo,
wengine tunaona kama umetudharau/hutujali...............
dada yako nae nyumbani ana tabia hii kwakweli!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
kiukweli tunagombana sana kwenye hili, lakini maisha inabidi yaendelee kusonga!!!
 
kitu ambacho nimeshindwa kujirekebisha kabisa kwenye ni "kinyongo" huwa nina kinyongo sana esp nijue kabisa hapa nadanganywa na nina hakika unanidanganya then hutki kuniambia ukweli bado mbishi tu na bac hapo kinyongo changu hakiishi, ukitaka kiishe niambie ukweli, eg wakati ule nilipomfumania alianza maelezo akitanguliza uongo uongo fulani kujitetea nilimshikia bango na ndio ingekuwa mwisho wetu ule lakini alivyosema ukweli roho ilitulia na kinyongo kikaisha, cpengi kudanganywa nikijua nadanganywa...kitu kingine ni "ukali" hili watu wengi esp mr huwa ananiambia mie mkali, lakini kila mwenzangu anaponiambia nipunguze cjijui naupunguzia wapi au nianzie wapi, hapa cjuagi kabisa nifanyaje....kingine ni kulalamikiwa bila sababu maalum, mr ana ile tbia kama akikucal/sms umeshindwa kujibu kwa wakati maalum bac hapo tatizo tayari, ntahicwa/shutumiwa kwa kila aina ya jambo.

Nyamayao nimeboreka kweli maana nilikujibu kuhusu ukali wako alafu ikasumbua kupost mpaka nikapoteza nilichoandika.Sijui kama ntayapata tena maneno nliyotumia mwanzo.

Wewe kama mimi tu kwenye swala la ukali na kuchukia/ogopa malalamiko maana hua inaboa sana.Unakuta mtu badala ya kuuliza kwanini haikua hivi au vile anashutumu na kutoa sababu zake utadhani alikuwepo.Hua inanifanya nione kama mtu haniamini...maana hata ukimwambia hapana ilikua hivi hatotaka kuelewa badala yake anang‘ang‘ania kile anachotaka yeye.Kuhusu ukali mi nasifika nao...ila sijawahi kulalamikiwa kwamba ni mkali sana maana mwisho wa siku watu hua wanaapreciate niliwawakia kidogo na kuwaweka sawa.Cha muhimu ni kwamba usiwe tu mkali kwasababu unajisikia au umezoea kua mkali...hakikisha kwamba unamtendea haki yule unaemwia mkali kwa kutomwonea.Kama kweli alichofanya/sema kinastahili na alihitaji uwe mkali ili aweze kutambua ni kwa kiasi gani hakikua vizuri utaishia kupata ASANTE badala ya MALALAMIKO/HASIRA baadae.Pia jitahidi sana usimfanye mwenzako ahisi unamgombeza kama mtoto maana hapa ndo hasira hua inaanzia.
 
Sasa mpenzi duh.............Mr ana-cope vipi na hili lako?? hasa ukali maana hilo la kinyongo ataavoid kwa kuwa mkweli but la ukali??!!

kuhusu kinyongo cku hizi ameshajua, huwa anajua akiwa mkweli kwangu huwa nasamehe hapo hapo, hilo la ukali kwa kweli cjui nitalifanyaje, najitahidi kujishusha but kuna waakti inabidi nipande tu kutokana na tukio.
 
Mie kwakweli na hasira za haraka limenifanya mara nyingi nionekane mkorofi,lakini huwa sijui kuweka kinyongo nikikasirika ntakwambia na ndio imeisha huwezi nisikia nakumbushia makosa yaliyopita.

Chauro nadhani kuna 'tabia' nyingine ziko nje ya uwezo wako na mara nyingi tabia za hivi huenda isiwe rahisi kubadilika au inawezekana ikachukua muda mrefu under huge efforts ...... mfano tabia ya hasira na kwa kiasi flani ubishi...sometimes hivi vitu muhusika anaweza akashindwa kabisa kuvibadili. Dawa pekee tu ni kwa mwenzi wa muhusika (ambaye tunaamini hatokuwa na 'tabia'hizi) kuangalia namna ya kukuaccomodate.

Unajua si kula kitu/tabia uibadili wewe ili urekebishe mambo flani....yeye pia anastahili kubadilika ili aacomodate tabia zako kama ni zile ambazo ni ngumu kubadilika. Mfano hacra, basi ajitahidi asikuudhi. na wewe kumsupport katika kubadilika basi unajitengenezea control ya ni makosa ya aina gani uya'pandishie' na reaction gani utoe wakatui huo wa hacra.

sasa sijui na hii ni tabia mbaya na imenishinda kuacha kabisa, huwa napenda kuwa muwazi sana kwa mweza wangu wakati mwingine huwa najikuta nimemueleza vitu ambavo nahisi sikutakiwa kusema,ukikuta sio muelewa basi ndo kinabebewa bango mwaka wote.

Hii kusema ukweli Chauro imetucost wengi........I used to be like that na mara nyingi huwa tunafanya hayo si kwa kuwa tu wajinga! La hasha hufanya hayo ili tuwaweke karibu wenzi wetu kwa kuwajengea tabia ya kutuamini zaidi. Well inategemea na mtu na mtu, mwingine anawezakuwa mwelewa lakini mwingine akautumia ukweli huo kukuumiza. Nitakupa mfano, kuna rafiki yangu mmoja yeye alikuwa naye ni muwazi mmno kwa mwenzi wake, alikujampatia siri moja ya familia ya wazazi wake; siri ambayo ingetokea kusikiwa ingeweza hata kusambaratisha ndoa ya wazazi wake. Walipokorofishana na mwenzake, tusi kubwa alilokuwa akipewa ni........" Sikushangai kwa sababu hata baba yako alifanya a,b,c ..sembuse wewe!!!"

Ni vema kujifunza kujizuia. Chambua yale yenye mahusiano ya moja kwa moja kati yenu wawili au yanayowaunganisha.

Napenda sana kuwa na marafiki zangu na wakati mwingine huwa nasahau kuaga basi tifu lake, taratibu siku izi nimejifunza kuaga ingawa wakati mwingine bado najisahau.

hii inabadilika mydia, taratibu naye ataanza kukuelewa kuwa sometimes huwa unasahau.
 
Baada ya kazi napenda sana kukaa na marafiki tukiwa tunapata moja baridi moja moto. Jambo hili mwenza wangu hapendi tabia hii anapenda nifike home before sitting on table.
 
kuhusu kinyongo cku hizi ameshajua, huwa anajua akiwa mkweli kwangu huwa nasamehe hapo hapo, hilo la ukali kwa kweli cjui nitalifanyaje, najitahidi kujishusha but kuna waakti inabidi nipande tu kutokana na tukio.

Ni kweli nyamayao, kuhusu hacra sasa itabidi ajitahidi kukuelewa na pia kama unavyosema huchangiwa pia na tukio so at least uko kwenye safe side kuwa kuna baadhi ya matukio huyapandishii kiviiile........ but also ukipandisha unareact vije? Usije ukawa ukipandisha basi anakula matusi kuanzia yeye mpaka kuku wa kujijini kwao. ....hii si hacra nzuri.
 
Baada ya kazi napenda sana kukaa na marafiki tukiwa tunapata moja baridi moja moto. Jambo hili mwenza wangu hapendi tabia hii anapenda nifike home before sitting on table.
And why dont you do what she likes?? compromise au kama huko unakokutana na marafiki ni mbali na home kuwa haitawezekana kwenda na kurudi basi uwe unaweka siku chache chache za kukutana na hao marafiki wa mbali!
 
Unajua ndg yangu ninapoishi ni mbali na ninapofanya kazi, muda wa kutoka kazini barabarani kunakuwa na folen ya kufa mtu. Hivyo tunashtukia wengi tunaoishi mbali tunapendelea kukaa mahali tukisubiria mabari yapungue barabarani ndo twende home kwa raha. Mwenzangu analijua hilo ila sometimes huwa analalamika.
 
Okay nimekuelewa at least unayo sababu ya kueleweka... but ndo hivyo tena jamani huwa tunawamiss sana bana.......muda wa kuwa na nyie wapenzi wetu wa usiku hautoshi bana.............na wengine mpaka weekend wako buzy
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
- kuna ulazima wa kupeana passwords i.e simu, email, bank nk? Binafsi nachukulia hiyo kama invasion of my privacy japo sina la kuficha. Sijui nyie wenzangu mnaichukuliaje hii?

Nadhani kuaminiana kunatosha badala ya kutaka chunguza kila sms, simu na email ya mwenza.
 
Ni kweli nyamayao, kuhusu hacra sasa itabidi ajitahidi kukuelewa na pia kama unavyosema huchangiwa pia na tukio so at least uko kwenye safe side kuwa kuna baadhi ya matukio huyapandishii kiviiile........ but also ukipandisha unareact vije? Usije ukawa ukipandisha basi anakula matusi kuanzia yeye mpaka kuku wa kujijini kwao. ....hii si hacra nzuri.

hahaha haya bwana...cnaga za hivyo, sema nikipandwa na hacra kuzishusha ni ngumu sana, huwa anajitahidi acnijibu coz tunakuwa tumeingia kwenye ushindani sasa mpaka nitulie tuweke mambo sawa....
 
- kuna ulazima wa kupeana passwords i.e simu, email, bank nk? Binafsi nachukulia hiyo kama invasion of my privacy japo sina la kuficha. Sijui nyie wenzangu mnaichukuliaje hii?

Nadhani kuaminiana kunatosha badala ya kutaka chunguza kila sms, simu na email ya mwenza.

kwangu mie hiyo sio lazima kabisa, cmpi/acnipe yake....yaeh kuna privacy jamani.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
mwanajamiione umenigusa na tabia ulizozisema kwa kweli hautofautiani sana ni mimi. Mie pia hupenda sana kuwa na 'mawasiliano' na mume wangu. chochote ambacho anaona ni kizuri au ni kibaya kinamkwaza whatsoever napenda aniambie tu bila kuficha ili either nitoe maelezo, utetezi au kujirekebisha, sipendi tabia ya mtu unamfanyia kitu hapa hasemi then miezi kadhaa baadae aanze kukumushia eti wakati uleeee ulifanya hivi hivi nikanyamaza, swali huja kama kweli ulikereka na ukaamua kunyamaza, then why now unaniambia, why cant u keep quet as u did last time etc etc!

napenda sana usawa hasa katika relationships, sio tu kwa kuwa ni mume basi awe juu yako bila sababu NO mimi pia kama binadamu nina mambo yangu yanazunguka kichwani, I have to think and decide sio kila kitu unitolee maamuzi na mie nibaki mtu wa 'ndio mzee"

napenda sana kuonyesha true colour of me, sio mtu wa kupretend! kama kitu sikipendi ni lazima nitakwambia and vice versa ili nisije nikajikwaza bure kwa kukubaliana na mambo ilimradi unione mzuri while rohoni naumia. Naipenda sana nafsi yangu na sipendi kuiumiza kwa namna yoyote ile labda iwe lazima sana.

Napenda kuheshimu maamuzi ya mtu na uhuru wake, sipendi sana kuingilia maamuzi binafsi ya mtu au uhuru wake unless vimekuwa kero sana kwangu hapo lazima nita-intervene, otherwise katika ndoa yangu tumepeana uhuru wa kutosha na inatusaidi kutokupigizana kelel zisizo za msingi .. ni mengi sana lakini hayo yatosha kwa leo.

SIPENDI mambo ya kupekuana pekuana kwa kuniwekea wapelelezi wa kunifuatilia mambo yangu au kuchunguza chunguza simu yangu.... hilo SILIPENDI Kabisa hadithi za MULIKA MWIZI kwani ni kero jamani ... mie sipekui mtu na sipendi kupekuliwa kwa kuwa nimejifunza kitu kimoja 'UNACHOKIPENDA USIKITAFUTIE KASORO' maana ukiigundua kasoro itakuumiza sana!
 
- kuna ulazima wa kupeana passwords i.e simu, email, bank nk? Binafsi nachukulia hiyo kama invasion of my privacy japo sina la kuficha. Sijui nyie wenzangu mnaichukuliaje hii?

Nadhani kuaminiana kunatosha badala ya kutaka chunguza kila sms, simu na email ya mwenza.

Hahahah Mbu .......hapa nadhani ni makubaliano pia yana huu.mfano mie niliamua kumpa passwords zangu zote (ingawa ilinicost- kama alivyosema Chauro too much uwazi). But when I did that I wasnt expect him/wala sikuwahi kunote kuwa yeye hajanipa...........to me it was a way of making him trust me completely. Kwake sikuhitaji hilo kwani nadhani niliamua tu kumtrust na nadhani ndio maana niliumia sana baada ya kujua ukweli.

Tabia yangu nyingine sijui iite mbaya au vije: Mwenzenu mie kuomba sijui!! yaani enzi zile za ubf na uchumba wakati tuko mbalimbali nina shida siweziomba-si kwamba nilikuwa nazo la hasha ila tu ni tabia tangu utoto (Nilizoeshwa na malezi ya shida utotoni-ukiwa na njaa unaogopa kusema; huna pesa ya shule -boarding unaogopa kusema - yaani maisha ya uwoga -nadhani nikisema hivi wengi mnaelewa nina maanisha nini) Hii imeniathiri mpaka ukubwani na matokeo yake naambiwa nina jeuri.

Hii imenipepekea kujitegemea zaidi kiasi kwamba hukwaruzana na mwenzangu pale ninapomwambia kuna dili nalifuatilia hebu nitafutie ED ya wiki moja au mbili! Huwa anakuja juu sana (hasa kama linahusisha safari au kulala nje ya nyumbani). lakini pia kuna kipindi ilikuwa inanicost pale ambapo mwenzangu alijisahau majukumu yake nyumbani- maana akirudi anakuta kila kitu kipo na mimi wala sioni tabu.

Natamani sana niishi kiuanamke lol............he used to tell me to be a lady loh.........kumwelewa ilikuwa ngumu kwa kweli na mpaka sasa sijafaulu.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Back
Top Bottom