Hahahhahhah...bwoi!!Well ili nisichukiwe kwa kuchakachua thread ya Mbu ngoja niungame angalau kitu kimoja japo nilishapanga ntakua mwangaliaji tu.Siku chache zilizopita nimeambiwa kwamba NAFIKIRIA SANA na kuchambua mambo kupitiliza kwahiyo mwenzangu inabidi awe mwangalifu kweli na anayosema!!
Unajua unapompenda mtu mapungufu yake yote unayapuuzia (ukizingatia hakuna mtu asiye na mapungufu), lakini pale unapoanza kumchoka au penzi linapoanza kuwa baridi ndipo unapoanza kutafuta visingizio..., kwamba huyu sijui siku hizi yukoje..., kumbe ni kwamba badala ya kumuangalia kwa jicho la upendo sasa unaanza kumuangalia kwa chuki na ku-concentrate kwenye mapungufu yake.
Nakubaliana nawe VoiceOfReason.
Ila, si rahisi kutekelezeka kama ilivyo kuelezea. Labda tuanzie hapo kwenye kupenda ukweli, maana yake nini?[/QUOTE
Unajua unapompenda mtu mapungufu yake yote unayapuuzia (ukizingatia hakuna mtu asiye na mapungufu), lakini pale unapoanza kumchoka au penzi linapoanza kuwa baridi ndipo unapoanza kutafuta visingizio..., kwamba huyu sijui siku hizi yukoje..., kumbe ni kwamba badala ya kumuangalia kwa jicho la upendo sasa unaanza kumuangalia kwa chuki na ku-concentrate kwenye mapungufu yake.
Nimeupenda sana mchango wako. Halafu karibu tena jukwaani na usiwe unapotea bila taarifa na kuwaacha viumbe wengine wakinyong'onyea na kushindwa hata kula vizuri 🙂
dah! Akiniuzi na mimi nimuuzi litakuwa movie la revange.Mwanya wa kujirekebisha upo....Nice! ...Nimependa hiyo confession.Sasa je, unajiskiaje mwenzako anapokasirika/kununa/kuchukia kwa hilo unalotenda?Unadhani kuna mwanya wa kujirekebisha? au unatumia tabia hiyo kama kiboko cha kumchapiapale naye anapokuudhi? tit-for-tat!
Asante sana mkuu samahani sana kwa kutokuaga lakini nilijua nikiaga tashindwa kuondoka.., lakini hapa ni nyumbani hata nikipotea kidogo lazima kuna siku nitarudiNimeupenda sana mchango wako. Halafu karibu tena jukwaani na usiwe unapotea bila taarifa na kuwaacha viumbe wengine wakinyon'gonyea na kushindwa hata kula vizuri 🙂
Duh Mbu........aksante sana kwa hii mada duh mi hata sijui nisemeje hapa kwa sababu umenigusa.
Kama nimekuelewa vizuri unamaanisha mnapoamua kuwa wote kama wapenzi ambao mnatarajia kuwa wenzi kuna tabia mbalimbali ambazo kwa bahati mbaya hazifanani kwa kuwa sisi tu tofauti. Na katika tabia hizi kuna unayowezaipenda au ichukia kwa mwenzi wako na yeye anawezaipenda au ichukia kwa mwenzi wako (Nisahihishe kama nimekuelewa visivyo).
Mara nyingi katika mahusiano hii huwa inatokea sana na kwa bahati mbaya wengine huwa tunapuuzia mwanzoni kwa kufikiri kuwa tukioana 'nitambadilisha', nitamkataza/zuia na atanitii kwa kuwa ni mume/mke wake..........hali ambayo husababisha migongano baadaye ya kama ulivyosema ..oh umebadilika siku hizi..........kumbe ni tabia iliyokuwepo tangu mwanzo ambayo eiither kwa sababu ya penzi changa au makusudi ulilifumbia macho!!
Mimi napenda:
- Masikilizano kwa ujumla- toka mwanzo wa mahusiano. Nikisema nisikilize, nielewe na kunisaidia pale unapoona siko sawa (ila utoe sababu si kunipinga tu) nami ukisema nikusikilize, nikuelewe na ku'dialogue' nawe kama kuna ulazima huo.
- Kuelezana 'yanayojiri' kwenye 'private spheres' zetu yaani kama ni kazini kwako kuna issue tell me, we discuss and see where/ how to go about. Sio unanijia na mijimawazo nkikuuliza ....naishia kuambiwa ....we acha tu au ni mambo ya ofcn hutoelewa......nijaribu uone kama sielewi.
Tabia Mbaya:
- Ukinikwaza kwa kosa flani, nitakueleza mara mbili, tatu ukirudia tena nachukulia makusudi and you wont hear me telling you anything about that......mf. unachelewa kurudi bila kutoa taarifa na ukirudi huo usiku mwingi nakwambia jinsi nnavyorukwa na roho kwa wasiwasi wa usalama wako, unapuuza then unarudia tena.......hutonisikia nikilizungumzia hilo. Ni tabia mbaya kwa sababu kwani ninadraw conclusion na kuanza kufanya maamuzi taratibu na siku nikisema basi yatosha.....inakuwa yatosha.
- Kupenda kutoa uhuru/freedom- tukiwa kwenye urafiki huwa sipendi kumbana mtu I know ana marafiki, ndugu n.k wa kukutana naye, i offer that freedom mradi taarifa itolewe, bahati mbaya even kwenye ndoa I tend to do teh same - ingawa sometimes ina maumivu yake. na
- Ni mzembe wa kufuatilia..............nikihisi kuna dalili ya kuibiwa penzi langu huwa naingiwa na woga wa kufind out to see if it is true or not......I just swallow it na kusubiria tu 'revelation' kutoka kwa MUNGU. Matokeo yake huwa ninajikuta ninaumia over nothing.
............eh mbona nina tabia mbaya nyingi?? Mbu ntarudi kuendelea.
-
Dah Mbu mwenzio mi nikiamini ninachokijua ndo ukweli huwa nakua mbishi na kuupigania huo ninaouamini kwa nguvu zangu zote. Labda baadae ntakaa nakufikiria kwa kina huku nikilingalisha na ile tofauti. Sasa napogundua kuwa mi nlikuwa wrong kinaniuma kweli kweli. Hata nkiomba msamaha naonekana hata si maanishi. Lakini hi ninayo kwa jinsia ya kiume zaidi. Siwezi kubishana sana na jinsia ya kike. Nkisema wasipoelewa naacha tu. Au nakua upande wao. Halafu pia nina moyo wa kujihukumu sana.
Wow...Mwj1 nice to read you wikiendi hii, Upo?
Well, ...kama kawaida yako, nimependa ulivyo muwazi.
I hope u muwazi kwenye kuongea pia, maana kuna wengine mwaweza kuishi nyumba moja usimsikie...
Yeye mazungumzo yake ni kwa email tu,..
eti mnapokuwa pamoja hawezi kuongea, ni bora ayapange kwa maandishi
Pheewww!
Hapo kwenye mapungufu yako 'in reaching conclusion slowly,' mbona si mbaya kiviiile?
Inaonekana huna maamuzi ya papara. Mtu mpaka akufikishe kwenye maamuzi hayo basi kweli atakuwa anashindwa kusoma alama za nyakati.
Nachelea kusema kutokana na tabia yako hiyo, huenda mtu akadhani hana analokukosea ilhali kiundani unaugulia.
Nadhani si vibaya uwe unakumbushia tena na tena unapokosewa, haswa makosa madogo madogo.
Usichoke kuwa mkweli. 'Ndoa ni bustani, palilia!'
Kumbuka nyie ni watu wawili tofauti, na kutokana na Life experiences zenu, makosa unayoyapima kuwa ni makubwa, huenda mwenzako anayachukulia ni ya kawaida. Ndio maana utasikia, "mambo madogo madogo unayakuuuuza!" LOL!
Mfano; hilo la kutokutoa taarifa, ... sidhani kama kuna ubaya wowote iwapo utachukua jitihada ya kupiga simu na kuulizia "muda gani utarudi Mume wangu?"...Ni mumeo, ni haki yako ya msingi kuwa na taarifa.
Kuugulia moyoni kunafukua makovu yaliyopita kiasi cha kuanza ku generalize "wote ndivyo mlivyo!"
naomba nijiongelee upande wangu, maana ninajijua ipasavyo.
-ve
Nina hasira tena hununa mpaka mashavu hujaa, yoyote anaenifahamu akiniona anajua nimevimba..inakera ila siwezi kujizuia nikiwa nimekwazika..ila mwepesi wa kuliongelea matatizo na kusuluhisha japo mnuno huanza...
Siyo mvumilivu, yani inapokuja suala la ku-give up huwa inakuwa mapema zaidi ya kuvuta subira mana kuna makosa nimeshajiwekea yakitokea hamna 2nd chance..
Mawasiliano siko mzuri sana..saa sita usiku kokote nitakapokuwa nazima simu yangu na hii kati ya makubaliano na mpz nilionae, nimezoea kuzima simu..halafu napenda sana kutext kuliko kuongea..
Sometimez, huduwaa na wanaume wanaovutia yani nashangaa au kumwonyesha mwenza wangu kiuchokozi..i guess inakera but naangalia uumbaji hamna zaidi!! ha ha ha
+ve
Ni muwazi kwa mambo yangu mf. nikiwa natoka na my friends nitamwambia naenda mahali sipendi habari za kuwa ameambiwa.
Napenda kutumia muda mwingi na mwenza siyo tu kimahaba bali kuongelea shughuli za maendeleo na kupeana shauri za hapa na pale kimaisha.
Ninajali sana na hii ni kutokana na roho ya utu niliyonayo. napenda napopendwa yani kwangu definition ya upendo ni nipe nikupe.
Yani package yangu ni kuwa 'what you see is what you get' sibadiliki kama kinyonga.
Mbu bwana....haya ngoja nijichambue kidogo kwa hisani yako!!
Yanayonihusu....
1.Ni msikilizaji mzuri kitu ambacho hua kinamfanya mwenzangu ajisikie huru kunieleza mambo yake.
2.Si hukumu....japo napenda kujua ya kale siwezi kumchukia au kumuona tofauti kwasababu ya yaliyotokea huko nyuma.
3.Nampa uhuru...ana marafiki zake na wana nafasi yao hivyo ruksa kuwapa muda wake kidogo.Ili mradi isiwe kama mimi na hao marafiki zake tunagombania/shindania muda na attention toka kwake.
4.Sidhani kama nna wivu...na kama nnao ni kidogo sana kwahiyo kumfuatilia...kumchunguza na kumlinda kama mtoto hamna.
5.Mbishi ila nikiwa na ushahidi na nnachokitetea.
6.Mgumu kuomba samahani kama najua fika sijakosea alafu awe kama ananilazimisha kukubali mimi ndo mwenye kosa!
7.Napenda sana kuongea kwenye simu na kuchat kwahiyo anaweza akaboreka kuniona niko bize na watu wengine muda mwingi.Ila kama ye yuko tayari kupiga story na mimi kwa muda huo ntawaweka wengine pembeni kidogo.
1.Nachukia sana kutuhumiwa vitu ambavyo sio vya ukweli.Unakuta mtu hajui kwanini hukupokea simu na wala haulizi ila automatically anaamua kwamba hukujali simu yake au ulikua unaongea na watu wengine wa maana zaidi yake.
2.Nachukia saaaaana kuagizwa....yani hata kama nimeenda jikoni kuchukua kitu alafu akashout niletee maji sitomletea...ila akiniambia naomba uniletee maji hata kama mimi nipo mbali nayo kuliko yeye ntaenda kumchukulia!!Napenda sana mtu anaeweza kutumia haya maneno mawili NAOMBA na ASANTE.
3.Nachukia pale mwenza anapokua hajiamini au haniamini bila sababu yoyote ya msingi.
Nadhani haya yanatosha!
Nipo mydia natawa mwenzangu kama kawaida yakek ...'am too wifey to accompany him' kwenye outings!! ......................lol
[/SIZE][/COLOR][/FONT]
Mbu hapa mimi ni mwongeaji sana...I wish ungenifahamu!! ninaongea sana na pale ninapoudhiwa siwezilala hadi niseme baada ya kusoma mazingira lakini...maana siku nyingine wawezasema umeudhiwa na ungependa kulitoa but mwenzio anarudi amevaa 'koti la chuma' halivuliki au anakuja na mawazo mengi ya 'kazini' huwezisema naye akakusikiliza. Otherwise 'nasema sana' kwa upole lakini loh..... ila ikileta ubishi nakaa kimya na kuliacha ..............hadi siku nyingine... ntaliamsha tu .. hadi unielewe au nikuelewe.
[/I]
[/SIZE][/COLOR][/FONT]
Kusema ukweli hadi nifikie hatua ya ku'mute' huwa ninakuwa nimeshalisema sana kwa marudio mengi tu na warning........huwa nasema.... "Baby....... unajua fika ninavyoumia unafanya a,b,c na nimeshalisema hili mara nyingi mydia....nadhani sina jipya la kuongeza nalichukulia hili kuwa unafanya kusudi..............na jua iko siku nitashindwa.... hii warning huwa inatolewa mara nyingi tu..........ili siku nikiamua vya kuamua nakuwa sina lawama......... ntaishia kusema ....mydia nilishakwambia muda tu.
[/I][/SIZE][/COLOR][/FONT]
.................Samahani kwa kutoweka wazi.....huwa ninatake all the possible means za kuhakikisha ninawasiliana na mwenzi.....uko wapi mpenzi? na nani? bahati mbaya experience yangu ya zamani ni kuwa simu zangu hazikuwa zinapokelewa kuanzia saa nne usiku (nilikuwa nakataa kuanza kumtafuta kabla ya hapo nsijeonekana nambana...... my weakness ya giving too much freedom)
[/SIZE][/COLOR][/FONT]
........Mh hili lina ukweli kaka!!
Hahahhha...no. 1 na 2 inawezekana vikawa vinapingana kweli ila sio hapa!!!I just love KNOWING...thats all!!Ya kununa na ukaribu wa hasira ngoja niache kwanza!...Lizzy you are so good kwenye uchaguzi wa maneno yako.Ahsante kwa mchango wako ila inabidi uwe muwazi zaidi mydear, LOL...Hapo kwenye namba moja na namba mbili zinashabahiana kuonyesha una tabia gani.Mimi nitaweka kiporo kwanza, ila nimekusoma na nimekuelewa namba mbili inaitangulia namba moja;2.Si hukumu....japo napenda kujua ya kale siwezi kumchukia au kumuona tofauti kwasababu ya yaliyotokea huko nyuma.1.Ni msikilizaji mzuri kitu ambacho hua kinamfanya mwenzangu ajisikie huru kunieleza mambo yake.Unaonaje? Contradictory? Wewe ni Mchambuzi ndio maana ni msikilizaji mzuri.Sifa mojawapo ya Analysts (Wachambuzi) ni uwezo wao mkubwa wa kuhukumu.-"Vulture is a patient Bird!"-Thanks for sharing Lizzy.
...Dah, BJ there you Go!
What can I say bana. Mimi ningekushauri hapo kwenye makosa uliyokwisha jiwekea jaribu tena kutafakari.
Sipendi kuwa too judgemental ingawa hili nalo ni tatizo langu, lakini unaposema una Give Up easily...nadhani pia
inaku cost sana maishani mwako.
Nahisi tatizo lako unaamini mwenza wako hakutaka kukuelewa.
Je, ulifanya juhudi za kutosha kuhakikisha anakuelewa? Uki Give up haraka haraka sidhani kana unajipa muda wa kutosha kujuana/somana tabia, au?
Je, hayo mapungufu yako, mfano huo uchokozi. Una uhakika gani anakuelewa dhamira yako?
Mimi ni mwanaume, na nisingependa kufanyiwa hivyo.
Je yeye akikufanyia hivyo kwa warembo wengine utaelewa uchokozi wake?
All in all, it's so nice of you kuwa muwazi.
Naamini wachangiaji wengine watakuja na maoni tofauti.
Da! mbu thread yako imegusa sana si member sana wa chumba hi lakini imenigusa sana maana muda huu nimenuna kwa sababu mama baby wangu ametoa priority kwa shughuli za nyumbani mpaka nahisi upweke na nimejaribu kumbeep ananiambia its not right time while ni wkend ya kuwa hm nae. -ve side yangu ni kutokurudia jambo ambalo tayari nilishasema pia napenda sana atambue thamani yangu kwake kama nifanyavyo mimi kwake. kuwa na misimamo isiyobadilika conservative mind. kuamini kile nifikiricho mimi ni bora zaidi, kutokuwa mwepesi kusamehe na hi inampa wakati mgumu sana mamsap wangu na huishia kulia tu, ninapokuwa na mawazo kichwani sipendi kubughudhiwa wakati wife hataki niwe kwenye deep feeling. ila mtu ambaye ni muwazi sana kwake since 1day hupenda ajue nini napenda na nini nachukia. anyway yanatosha kwa sasa ngoja niende ndani maana nipo sebuleni najiliwaza na mziki laini wakati yupo anahuzunika maana hajajua nini kimenifanya niwe kimya