Chuo kikuu cha Nairobi chagundua Samaki wanaotoka China wana sumu za Mercury, ZINK, COPPER,LEAD,IRON. Ni hatari kwa afya ya ubongo na mwili. Tz kimya

Tanzania tuna maziwa makubwa manne pamoja na Bahari, tuna mito mikubwa mingi yenye samaki lakini bado tunaagiza samaki nje....

Sent using Jamii Forums mobile app

samaki wengi duniani wana kiasi kidogo cha madin ya mercury na hili si jambo la kushangaza sana, yaani samaki wanatoka china alafu wanakuwa cheap kuliko samaki wetu kuna nini apo?? Ingekuwa vizuri watuambia samaki wetu wana kiwango gani cha mercury vilevile, isije ikawa samaki wa china wana mercury kidogo kuliko wetu
 
Umefanya vizuri kutuletea habari hii lkn Tanzania ilishatambua hili kitambo na ndio maana hakuna samaki kutoka china, ilishazuhiliwa kitambo.
Kwa taarifa wapo wengi tuu, yaani juzi tuu nimewaona Sangara wakubwa wengi tuu wanauzwa ferry soko la samaki, watu wanawagomba ia kweli kweli tena mita chache tuu kutoka ikulu kwa muheshimiwa
 
Return Of Undertaker,
Eti inaitwa ni study! Hiyo haihitaji study, ni monitoring tu ya vyakula vyote. Ni routine!
Halafu unataka tufanye hayo kwa kuwa Kenya wamefanya? Naangalia hiyo screen ni uozo tu! Tangu lini kukawa na kiwango recommended cha lead?? upuuzi tu!
 
Ni aibu kubwa sana, watu wa ukanda wa Afrika mashariki kula samaki kutoka china, tuna ziwa Tanganyika, Victoria, rukwa, nyasa, turkana, bahari ya hindi, mito ya kila aina..... tupewe nini zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
Samaki wenu munashindana kuiwauza nje ya nchi, halafu unadhani wapo? Sangala wote wanauzwa nje, Kenya inaongoza kwa unafiki wa kutotaka kukubaliana na wengine. Wakijidai kujua biashara. Let them eat chines rubbish.
 
Kwa taarifa wapo wengi tuu, yaani juzi tuu nimewaona Sangara wakubwa wengi tuu wanauzwa ferry soko la samaki, watu wanawagomba ia kweli kweli tena mita chache tuu kutoka ikulu kwa muheshimiwa
Nawe bwege tu! Tangu lini sangara wakapatikana china? Ngoja nipeleke ombi kwa Mod. kuomngeza screening ili michango kama hii iwe inafutwa kabla ya kutufikia wasomaji.
 
Umefanya vizuri kutuletea habari hii lkn Tanzania ilishatambua hili kitambo na ndio maana hakuna samaki kutoka china, ilishazuhiliwa kitambo.
Acha uongo, huku Zanzibar tunawaita Peduu yaan wamejaa kama wote, tena siku hiz wahuni wanauzia ufukweni kabisa unaweza dhania wametoka kuvuliwa nenda ukamtengeneze sasa ..........

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu, huku tunatumia parts per million (ppm) Kama SI Unit.
Kuhusu heavy metal toxicity levels, sikliza vidio c.

Science haijawahi danganya.

Tafiti inabishiwa Kwa tafiti. Vinginevyo ni hatari tupu.
Si hata hiyo 'ppm' bado inatakiwa kuonyeshwa hapo kwenye chart, mkuu mwanasayansi!

Huwezi kusema mtu asikilize video ndio atambue hivyo vipimo ni vya aina gani, hiyo sayansi haipo.

Sasa ngoja nikwambie; hata hiyo unayosema 'ppm' ambayo ni sawa, ukiwa mwelewa wa haya mambo utajua inatokana na hiyo, gram/mg, n.k.

Au wewe unasemaje mkuu mwanasayansi?

Na hiyo 'statement' yako ya mwisho inatia shaka. Sielewi hasa una maana gani.

Ndio, sayansi haiwezi ikadanganya, lakini kumbuka vipimo hivyo vinatokana na mpimaji na vyombo vilivyotumika. Je, maabara iliyotoa vipimo hivyo, unao uhakika wa uaminifu na ustadi wake?

Ni maabara inayotambuliwa kama kituo sahihi cha kufanya vipimo kama hivyo?

Je, 'data' hizo zimekuwa 'collaborated' na vituo vingine?

Nina hakika utakuwa umenielewa.

Mimi sikuandika kuwa sayansi "inadanganya" sehemu yoyote katika bandiko langu, sasa sijui ulitoa wapi dhana ya kufikiri kwamba kuhoji kwangu kwa hivyo vipimo kunatokana na "sayansi kudanganya."
 
Kalamu1, Wewe umesoma taarifa ya television. Ungesoma chapisho la hao wanasayansi usingekuta mapungufu hayo. Makosa ni ya mtoa taarifa sio watafiti.
 
Wewe umesoma taarifa ya television. Ungesoma chapisho la hao wanasayansi usingekuta mapungufu hayo. Makosa ni ya mtoa taarifa sio watafiti.
Unaweza ukawa sahihi. No, na-edit: Huwezi ukawa sawa.
Mimi naangalia tu hiyo 'chart' ilivyo hapo kwenye screenshort. Ni lazima ionyeshe 'units'. kama ilivyo ili iwe kamili, bila kujali imenukuliwa kutoka wapi..
 
Nani karuhusu haya masamaki ya nje kuingizwa tanzania,Hivi kweli hii bahari ,mito na maziwa yote hayatutoshi kuvua samaki freshi?Nani katuroga?
 
Eti inaitwa ni study! Hiyo haihitaji study, ni monitoring tu ya vyakula vyote. Ni routine!
Halafu unataka tufanye hayo kwa kuwa Kenya wamefanya? Naangalia hiyo screen ni uozo tu! Tangu lini kukawa na kiwango recommended cha lead?? upuuzi tu!
Lead inapatikana naturally katika udongo, hewa, vumbi na maji ya kunywa. Huwezi kuikwepa Lead hata ufanye nini na ndo maana kuna recommended intake amount. Ukizidi hiyo unakuwa hatarini.
 
Unaweza ukawa sahihi.
Mimi naangalia tu hiyo 'chart' ilivyo hapo kwenye screenshort. Ni lazima ionyeshe 'units'. kama ilivyo ili iwe kamili, bila kujali imenukuliwa kutoka wapi..
Sasa mbona unalaumu waliotoa chapisho. Kwani hiyo tv channel iinamilikiwa na wale wanasayansi. Badala ya kumkosoa anayetoa taarifa zikiwa na upungufu unamshambulia aliyeandaa utafiti. Hakuna mwanasayansi mpuuzi anayeweza kuweka vipimo bila kubainisha units gani katumia, form 2 wanajua hili sembuse wanachuo.
 
Mkuu, mbona huelewi?
Makosa sio ya hiyo TV kuhusu mwonekano wa chart hiyo. TV haiwezi kuondoa alama yoyote kwenye 'powerpoint' presentation.

Makosa ni ya waliotengeneza 'chart' hiyo. Bado huelewi tu!
 
Hivyo vipimo ni vya aina gani?

Hawa wanasayansi wetu nao wakati mwingine wanayo matatizo.

Hiyo 'chart' inaonyesha vipimo na kiasi walichopata, na 'Limits' zake; lakini haisemi 'units' zake ni nini, milligrams/au micrograms ama nanograms ama picograms, au ni 'asili mia'?

Je hizo limits za madini hayo, ni kiasi anachotakiwa mtu asizidishe kiasi hicho kwa siku ama?

Au ni vipimo tu kulinganisha kiasi kinachotakiwa kisizidi kwa uzito maalum wa samaki huyo?

Kuna maswali mengi hapo!

Lakini kwa upande wa pili, waChina waliweka ngumu sana kuruhusu Kenya wauze 'avocado' zao huko China kwa visingizio chungu nzima kama 'sanitary standards' hadi wakalazimu 'avocado' yawe yanagandishwa nyuzi za sentigredi chini ya -30 C jambo ambalo mkulima na wafanya biashara wadogo linawaongezea gharama mara dufu.
Upo sahihi..na waseme pia walitumia kifaa gani kupima, walifanyaje sampling.wasije kuwa wametumia vifaa au njia za kikanjanja.
 
Mkuu, mbona huelewi?
Makosa sio ya hiyo TV kuhusu mwonekano wa chart hiyo. TV haiwezi kuondoa alama yoyote kwenye 'powerpoint' presentation.

Makosa ni ya waliotengeneza 'chart' hiyo. Bado huelewi tu!
".....Hivyo vipimo ni vya aina gani?

Hawa wanasayansi wetu nao wakati mwingine wanayo matatizo.

Hiyo 'chart' inaonyesha vipimo na kiasi walichopata, na 'Limits' zake; lakini haisemi 'units' zake ni nini, milligrams/au micrograms ama nanograms ama picograms, au ni 'asili mia'?

Je hizo limits za madini hayo, ni kiasi anachotakiwa mtu asizidishe kiasi hicho kwa siku ama?

Au ni vipimo tu kulinganisha kiasi kinachotakiwa kisizidi kwa uzito maalum wa samaki huyo?......"

Hapa ulikuwa unalaumu wanasayansi sasa sijui unachobisha na kusema sielewi ni nini. Rejea ulichokiandika #10.
 
Back
Top Bottom