KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,189
- 17,157
Imenibidi nirudi na kulisoma bandiko lako hili kwa umakini.Sasa mbona unalaumu waliotoa chapisho. Kwani hiyo tv channel iinamilikiwa na wale wanasayansi. Badala ya kumkosoa anayetoa taarifa zikiwa na upungufu unamshambulia aliyeandaa utafiti. Hakuna mwanasayansi mpuuzi anayeweza kuweka vipimo bila kubainisha units gani katumia, form 2 wanajua hili sembuse wanachuo.
Ulichoandika hapa hii ndio siasa yenyewe, siyo sayansi hata kidogo.
Jaribu kulitafakari hili utaona ukweli ninaousema.
Na wanasayansi kama wewe, kama kweli wewe ni mwanasayansi, ndio mnaoturudisha nyuma sana katika nchi zetu hizi changa.
Mna-'dismiss' tu kirahisi rahisi mambo ya msingi ili muonekane nyinyi ndio mnaohodhi eneo hilo mnalodhani mnalo ufahamu nalo.
Matokeo ya kukosa umakini huo, ndiyo yanayotusababishia matatizo.