Chuo cha Madini Dodoma kunani?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Ndicho chuo ambacho kinatarajiwa kutoa wataalamu wa fani ya madini nchini. Unaweza kutembelea tovuti yao HAPA Kwa miezi ya karibuni (kama siyo miaka) chuo kimejikuta kikiwa na matatizo mengi hasa yakihusiana na uwezo wake wa kuwapika wataalamu waliobobea katika fani hiyo (matatizo ya kitaaluma) na vile vile matatizo ya vyombo na nyezo mbalimbali. Katika pita pita zangu za kufungulia mwaka nimekutana na moshi ukifurukuta kutoka kwenye chuo hicho ambao unahusiana na uongozi mbovu na ukosefu wa msukumo kutoka kwa wabunge na wizara pamoja na wananchi kutokujua umuhimu wa chuo hicho.

Moshi huu umezidi na natarajia siku si nyingi tukaona moto wake kwani lile dudu tusilolipenda limepiga kambi!! More to come...

LInanifanya nijiulize - ni taasisi gani inayofanya kazi yake vizuri sana katika mfumo wa watawala waliopo?
 
Hapo kwenye red: kuna tija kwa TAIFA?
 
i see kumbe kuna chuo cha madini? ndo unanifumbua macho!!! kina wanafunzi wanasoma huko?
 
Well wapo ila matokeo ya hivi majuzi asilinia kumi wamefeli wanatakiwa kurudia mtihani.
 
i see kumbe kuna chuo cha madini? ndo unanifumbua macho!!! kina wanafunzi wanasoma huko?

Wengi tu wame graduate pale as mine technician na wanafanya kazi sehemu tofauti tofauti tanzania kwenye mining and Exploration and Drilling.
 
Ni jambo la faraja na kushukuriwa sana.
Ni kweli isiyo na kificho kuwa chuo cha madini dodoma sasa kinayumba.
Na kimejikita zaidi katika kukomoa kuliko kutoa mafunzo.
Kuna ndugu yangu anasoma pake na matokeo yao ya semister iliyopita ni aibu.na hili limetokana na kuwepo kwa uongozi wenye mapungufu.

Huyo katibu mkuu mpya aliyeteuliwa afanye hima afike pale,chuo hakina muelekeo kwa sasa.
Wachache wanataka kukibomolea sifa chuo hicho.
Viva mwanakijiji
Viva jf.
 
hiki chuo niliwahi kufanya hapo interview miaka ya nyuma kilikuwa vizuri.
ila sasa nasikia kuna mkubwa serikalini anataka kukichukua awe mwekezaji(poultry project)
dodoma kuna wanachuo wengi kwa hiyo mayai ya chips yameadimika na yanalipa ile mbaya.
 
Mkubwa gani tena?
 
heee yaani chuo iwe sehemu ya kuku kutaga mayai duuu!
 
Back
Top Bottom