Chuo cha Kumbukumbu ya Mwl Nyerere kuwa Chuo cha Mfano?

Uzalendi

JF-Expert Member
Jun 24, 2013
221
15
Chuo cha Kumbukumbu ya Mwl Nyerere kuwa Chuo cha Mfano kama ni kweli kuwa Serikali imefanya kweli kwa kuuweka Uongozi mpya ambao ni wasomi na weledi. Sisi wanafunzi tunaorudi Chuoni hivi karibuni tunafarijika kwa kuwa tulinyanyasika sana huko nyuma. Mabadiliko haya ni matokeo ya malalamiko mbalimbali ya wanafunzi kutokana kuonewa katika taaluma na mazingira mabovu yaliyokuwa Chuoni hapo. Wito kwa Uongozi mpya wa Chuo ni kuuondoa uozo kutoka kwa walimu hasa waomba rushwa ya ngono na wasio na sifa sitahiki. Tunaishukuru sana Serikali yetu kama imesikia kilio chetu na kuweka mabadiliko yanayosemwa yamefanyika kwa sasa tunaporejea Chuoni kuendelea na masomo. Wenye uhakika wa hili mtujuze ili tufarahi.
 
Nilijua una habari kamili!?? Huo uongozi uliochukua nafasi ni UPI!?
 
Back
Top Bottom