Chungeni msiingizwe kingi na majini bandia

Chungeni msiingizwe kingi na majini bandia

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
374,468
Reaction score
867,166
Vyuma vikikaza utapeli uongo na ulaghai vinazidi kuongezeka.. Hakuna wakweli siku hizi si wanawake si wanaume... Zamani zile haya Mambo yalikuwepo lakini kwa kiwango cha chini sana
Miaka ya hivi karibuni kutokana na ongezeko la wanawake kuzidi wanaume.. Kuna kundi la wanaume wakachukua advantage ya kuwadekea wanawake.. Yani wao ndio wahudumiwe kama mademu karibu huduma zote... Ikawa ni kama fasheni, wanawake wakaanza kuwashtukia kuwa hawana mapenzi wala mpango kazi yao ni moja tu kulelewa.. Wakaitwa Mario
Wanawake kushtuka kulipozidi jamaa nao wamebadili mbinu, kujifanya wana mashetani ama wana majini... Dada na wadogo zangu wa kike GUTUKENI MNAPIGWA! MNAIBIWA!
Majini huchagua watu wake na kugeuza mili ya hao watu kama makazi yao... Wenyewe wanaita KITI
KITI hupangiwa masharti na jini, kwa sehemu kubwa hupangiwa cha kufanya na jini... Na kwa sehemu kubwa pia KITI huwa ni mwanamke... Ni kwa asilimia ndogo mno kukuta KITI ni mwanaume
Limeibuka kundi la wanaume wanaojifanya ni KITI cha jini na kuwatapeli wanawake vitu vingi fedha nk... Jini likitaka kitu litataka liletewe hapo hapo haliwezi kukwambia KITI akalete au KITI apeleke! Jini akitaka kupandisha hatakwambia ufiche sura.. Jini akitaka kufanya mengine hatakwambia KITI aondoke usiku mzima au hataagiza vitu vizuri kisha akielekeze KITI kivipeleke kusikojulikana... Hapa ni pamoja na pesa....
Kinachofanyika ni mazingaombwe na utapeli wa kawaida kabisa ukichanganywa kidogo na ulozi pori....!!! Dada zetu wanaaminishwa kuwa jamaa aliyenaye ana majini na jini likipanda linataka laki ukiitoa eti linamuelekeza KITI aipeleke hiyo hela mahali tena usiku... Dada kwa woga kabisa unakubali unatoa pesa unampa jamaa anaenda zake kula bata batani... Na hakuachi mpaka uishiwe kabisa ndio anasepa! Siku akijua umezipata tena ATARUDI...

NB: KITI hapigwi
Nina simulizi ya kweli na nitakuja kuisimulia hapa hapa kuhusu mpenzi niliyekuwa naye ambaye alikuwa ni KITI.... Niliwahi kula kipigo kitakatifu baada ya kujifanya Bouncer mbele ya KITI... Nitasimulia kwakuwa mavi ya kale hayanuki.....
 
Mwezi km huuuu mwaka 2011..... ulichokiongea nikweli mtupu mkuuuuu ..UKWELI kabisaaa haaaaaaa...... Daahhhhh yule jamaaa Hatutomsahau.
 
Hahahaha nimefurahi sana Kwahyo kuna wanaume sasa hivi ni viti? pesa inatafutwa kiukweli
 
mshana jr
Kiti anapoamriwa kuondoka safari za usiku kwenda hata mlimani au kijiji flan cha mbali, je; Jini huyo humlinda kiti wake ili asidhurike ama inakuaje? Maana anaweza kutana na maswahibu mfano kukutana na wanyama wakali au kunyeshewa mvua ya mawe? Inajuaje hapo, na je una mfano halisi?
 
Kuna kiti alijifanya anataka hela na pombe, nikalivuta Panga alitoka mbio. Siku ya pili alinifata na kuniuliza jana ulitaka kuniuwa na lile Panga? Nikamuuliza ulijuaje na wewe ulipandisha mashetani?. Hii mbinu kwa wadada ukiona mwanaume wako kapandisha mashetani mtie kidole cha tigo. Hapo utajua kama kweli Kiti au kigoda dadeki zake
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] usimdanganye mdada wa watu atakufa mapema nakuambia
 
Je kiti huumwa magonjwa ya kawaida ya binadamu, akiumwa kiasi cha kupoteza fahamu, jini lina uwezo wa kuwendelea kufanya kiti kuw active japo mhusika kapoteza fahamu kwa kuumw?

Jini anaweza kuishi kwenye kiti cha mtu aliyefariki, yaani jini aingie kwenye mwili wa marehemu na kuuamsha na kuutumia km kiti?
 
mshana jr
Kiti anapoamriwa kuondoka safari za usiku kwenda hata mlimani au kijiji flan cha mbali, je; Jini huyo humlinda kiti wake ili asidhurike ama inakuaje? Maana anaweza kutana na maswahibu mfano kukutana na wanyama wakali au kunyeshewa mvua ya mawe? Inajuaje hapo, na je una mfano halisi?
KITI hupewa ulinzi maalum na jini wake hivyo hawezi kudhurika na lolote
 
Kuna kiti alijifanya anataka hela na pombe, nikalivuta Panga alitoka mbio. Siku ya pili alinifata na kuniuliza jana ulitaka kuniuwa na lile Panga? Nikamuuliza ulijuaje na wewe ulipandisha mashetani?. Hii mbinu kwa wadada ukiona mwanaume wako kapandisha mashetani mtie kidole cha tigo. Hapo utajua kama kweli Kiti au kigoda dadeki zake
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji87] [emoji87] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Je kiti huumwa magonjwa ya kawaida ya binadamu, akiumwa kiasi cha kupoteza fahamu, jini lina uwezo wa kuwendelea kufanya kiti kuw active japo mhusika kapoteza fahamu kwa kuumw?

Jini anaweza kuishi kwenye kiti cha mtu aliyefariki, yaani jini aingie kwenye mwili wa marehemu na kuuamsha na kuutumia km kiti?
Jini huwa dormant mpaka anapotaka kutumia KITI wake hivyo vitu kama magonjwa haya ya kawaida humpata KITI. Jini hana uwezo wa kuzuia kifo kitokanacho na MwenyeziMungu.. Ila vifo vitokanavyo na husuda za dunia
 
hahaha imenikumbusha mbali nlikuwa na demu alikuwa KITI alinichagulia hadi rangi za mashuka, ila alikuwa ananistua vitu vingi sana ila aliniacha bila sababu na wala hatukugombana aliniacha tu since then cjamuona ila ananitafutaga akitaka kuniambia nijihadhari na baadhi ya vitu
 
Back
Top Bottom