Mhandisi Mzalendo
JF-Expert Member
- Aug 23, 2010
- 8,084
- 15,069
- Thread starter
- #21
Kwa wahaya inabidi useme okashenye ikishakuwa usuku
Nadhani ni karibu makabila yote....je ni kwa nini?
Kwa wahaya inabidi useme okashenye ikishakuwa usuku
Umenichosha tu, nilidhani chumvi kuu.
Nafikiri ilkuwa aina ya mafunzo fulani, kama mifano inavyojieleza hapo chini
Mfano unaambiwa usishone usiku - unafundishwa usalama wako unaweza kujitoboa/kujidunga na sindano
Usifagie usiku - usiku kuna giza kwahiyo hutoweza kufagia kama inavyotakiwa
Usimruke mtu utakuwa mfupi - unafundishwa nidhamu unapotaka kupita muombe mtu akupishe sio unaruka ruka
Umenichosha tu, nilidhani chumvi kuu.
Nadhani hayo ni mambo yanayowatokea huko kwenye vinchi uchwara lakini huku majuu hatunaga ushamba-ushamba wa aina hiyo kila kitu kinaitwa kwa jina lake halisi, iwe usiku ama mchana.
Umemaliza mkuu, ni mbinu za kufundishana tabia bila ya wewe muhusika kujua kinachoendeleaukipishana na mkubwa wako mlangoni utakufa...kumbe nidhamu tu,huwez kupishana watu wawili mlangoni.istoshe ni Baba au mama yako.
unamjua holygrail?
Aisee!
Kumbe ndo maana kuna duka moja pale kinondoni shamba nilienda kununua chumvi saa mbili usiku nikanyimwa wakati naziona kabisa! Eti ananiambia hawauzi chumvi usiku!
Nilijiuliza maswali Mengi sana!