Chumvi imeharibika, itatiwa nini hata ikolee?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,789
. CHUMVI YA ULIMWENGU

. NURU YA ULIMWENGU

Vitu hivi ni muhimu sana kwa mustakabali wa Maisha ya Mwanadamu

Mathayo 5:13 Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu.

Yesu anatuita sisi ni CHUMVI ya DUNIA! Kazi ya CHUMVI ni kutia ladha kwenye CHAKULA, na haihitajiki Chumvi nyingi ili kukifanya Chakula kiwe kitamu

Chakula hicho, hakiwezi kutamanika na kuliwa na watu, japo ni kizuri, ikiwa CHUMVI sisi tumeharibika! Yesu ametuita CHUMVI na siyo SUKARI kwa sababu CHUMVI haina gharama kubwa, na matumizi yake ni mengi.

Chumvi ya tsh 500 Unaweza kuitumia Wiki nzima, kwenye FAMILIA ya watu 10, Lakini Sukari ya tsh 2800 Huwezi kuitumia kwa wiki nzima kwenye FAMILIA ya watu 6 kuna watu VIJIJINI chai, Hawanyi, lakini wanapika MBOGA, wanahitaji CHUMVI, wakipika Wali, wanahitaji Chumvi, Wakikaanga CHAPATI, wanahitaji Chumvi, Wakipika Makande, Maharage, Choroko, Wanahitaji CHUMVI, nyama ya Kuku, Maini, na uzuri wake, hata Ukiirost vipi, usipoitia CHUMVI, chakula hakitanoga kabisa.

Mathayo 5:14 Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima.

15 Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani.

16 Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.

Matendo yetu, yawe Nuru, Yawe Chumvi kwa watu, wapate kumtukuza MUNGU, kupitia sisi, Mungu hajataka yeye mwenyewe kushuka, ili kuja kuwafanya watu wamjue yeye, bali ametuweka sisi tumwakilishe kwa watu wake, MATENDO yetu yawe Nuru, ya kuwatoa watu gizani. yawe Chumvi ya kuwapa watu ladha ya kumjua BWANA YESU KRISTO.

Badala yake tumegeuka na kuwa CHUMVI iliyoharibika, tukizani kwamba, watu wanapendezewa nasi, kumbe huko wanamuona Kristo ni asiyefaa, aliyeshindwa Kutufanya sisi tuwe safi, Je! atawezaje kuwafanya wao kuwa SAFI? ikiwa Chumvi wewe, Nuru wewe, Unashiriki, UZINZI, ULEVI, KIBURI, UCHAWI, UASHERATI, ULAWITI, UFIRAJI, UJAMBAZI, USENGENYAJI, hivi utaweza kuwamurikia Nuru wengine wakati umeshageuka na kuwa GIZA? Kristo anatazamwa uwezo na nguvu yake kupitia wewe, kama ilivyo kwa CHAKULA, utamua wa Chakula unajulikana kupitia CHUMVI!

Wakati mwingine Chumvi wewe usijiweke sawa na Chakula utaharibu ladha, usijifanye kuwa Sawa na Kristo, UTUKUFU wa Yesu, usiubebe wewe, Utageuka Chakula kilichozidi CHUMVI, na kuwafanya watu KUUGUA SAFURA. naamaanisha usiweke mbwembwe kwenye Suala zima la UTUMUSHI.

Kama hukuwa unajua kuwa, hayo ambayo unafanya siyo sawa, basi geuka sasa! Uwe Chumvi kweli na Nuru kweli, maana tunaambiwa.

2 Korintho 3:2 Ninyi ndinyi barua yetu, iliyoandikwa mioyoni mwetu, inajulikana na kusomwa na watu wote;

3 Mnadhihirishwa kwamba mmekuwa barua ya Kristo tuliyoikatibu, iliyoandikwa si kwa wino, bali kwa Roho wa Mungu aliye hai; si katika vibao vya mawe, ila katika vibao ambavyo ni mioyo ya nyama.

Na watu wengi bado hawajajua umuhimu wa CHUMVI, siku Chumvi ikiwa ADIMU kama ilivyotokea kwa Sukari hapa kwetu TANZANIA! watakuja kuona umuhimu wake, ndivyo itakavyokuwa kwa Kanisa la Kristo, litakapoondolewa,

Jr
 
Safi sana Mkuu Mshana Jr
Lkn umesahau nawe wakati mwingine taa yako unaiweka chini ya pishi na chumvi kuinyanganya na mchanga hasa pale unapong'ang'ania ndoto, utabiri wa nyota, uchawi na majini badala ya kusisitiza meditation katika tafakuri ya nafsi tupu Katka kumwelekea Mungu ili akujalize na sio kutafuta nguvu
Mjazilizo kama anavyohubir Rakims

Kanisa la kristu!
Kanisa la mitume!

Upo wapi mshana ?
 
wengi hawajui kua ndumba pia ni nguvu za mungu ndo maana wanakushangaa mshana
Nguvu ziko mbili duniani tu

Mizimu ilikuwepo zaman kbla ya yesu na aliposhukia kuzimu na mizimu ikafa kwani alikutokomeza kwa kuzipeleka mbinguni na zisizostahili motoni hivyo hukumu yetu ni ya walio hai yaani walioishi baada ya kristu kufufuka
Juju kwa dhana ya kiafrika ramli ni uongo( deception) isipokuwa kuna talanta >>>> kama magic au mitindo ya juggery nk isiyozuru ukiona imezuru roho basi nguvu ya pepo inahusika


Mshana Jr tulifundishe hili ( dini ya afrika ilifundisha uwepo wa Mungu 1 na si tofauti yaani Leo mti huu kesho mti ule hapana, hasipowajibu wanasubiri, au kufanya jitihada kama sadaka na maombi ya kujitakasa lkn leo waganga wanaamini ktk wapi?-- in kawaida ya mwanadamu na historia inaonesha watu walimtafuta Mungu lkn baadhi wamwshindwa kubadilika kama Buddha, Hindu nk lkn pia wanaamini Mungu 1)
 
Safi sana Mkuu Mshana Jr
Lkn umesahau nawe wakati mwingine taa yako unaiweka chini ya pishi na chumvi kuinyanganya na mchanga hasa pale unapong'ang'ania ndoto, utabiri wa nyota, uchawi na majini badala ya kusisitiza meditation katika tafakuri ya nafsi tupu Katka kumwelekea Mungu ili akujalize na sio kutafuta nguvu
Mjazilizo kama anavyohubir Rakims

Kanisa la kristu!
Kanisa la mitume!

Upo wapi mshana ?
Ni kwa vile nami si mkamilifu natenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu... Ndio maana ni muhimu sisi sote kudumu katika toba na maombi

Jr
 
Back
Top Bottom