Chumba cha sindano DTB....!!!!

donlucchese

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2011
Posts
17,258
Reaction score
22,140
Wakuu nipo hapa DTB harbour view posta ndio tunasubiri kuingia mmoja mmoja kwenye interview (3rd interview). Kwa kweli matumaini ni madogo sana kwani wapo jamaa ninao wafahamu ambao walifanya zote tatu still wakachinjiwa baharini. Ila naomba Mungu mambo yaende sawa tu tuone tunafanya nini. Daah, kuna jamaa kaja na suti hapa yaan utadhani yeye ndio meneja uajiri na mkwara wake kwamba haelewi kiswahili vizuri. Pia kuna mhindi mmoja amevaa silver kibao, wahindi wa humu ofisini kila wakipita wanampa hi nyingi aisee sijui mtoto wa mdosi mwenzao? Huyu wanaweza wakampa kiundugu. Ngoja mimi mjukuu wa Mwangungumile Mwampuza nisubiri kuitwa. Salaam!
 
Vipi mkuu? nakutakia kila la kheri katika iterview yako ya mwisho, ila nakuomba uwe na confidence otherwise itakula kwako mkuu, zingatia vigezo hivi
1 jiamini
2 sikiliza swali kwa makini kama hujaelewa uliza
3 mwangalie usoni anayekuuliza swahili
4 pangalia maelezo yako na tumia lugha rahisi,
5 uliza maswahili
6 aliyevaa suti achana naye wewe fanya yako, inawezekana aliyevaa suti ni garasa, hivyo basi maelezo yako na kujiamini kwako mkuu, unaweza ukapata kazi , DTB wanalipa vizuri, inshallaah
 
Acha uoga hizo mbwembwe tu,piga moyo konde utashinda tu!
 
kwa maelezo yako tu yanakufunga, I thought utajijengea trust na kumshukuru MUNGU kuwa umetoka mbali hadi hapo ulipo badala yake unaanza kulalama?? Kuwa na confidence na MUNGU akutangulie
 

Thanx a lot mkuu, umeniboost energy sana. Thanx alot
 
Shida yako ya uwoga ni kuwa utakosa kazi hiyo au hao wa suti, kiswaengl?
 
vijana wa leo bwana badala ya kutafakari interview uko jf alafu unategemea upate kazi mtu kama wewe hufai ktk benk hata ukiona siri za watu utaleta jf mambo mengine siyo ya kuleta hapa jf alafu unataja na tasisi huna ethics wewe
 
kwa maelezo yako tu yanakufunga, I thought utajijengea trust na kumshukuru MUNGU kuwa umetoka mbali hadi hapo ulipo badala yake unaanza kulalama?? Kuwa na confidence na MUNGU akutangulie

Amina mkuu.
 
Kama kuna mdosi kwishney maana DTB ni ya wadosi.
 
vijana wa leo bwana badala ya kutafakari interview uko jf alafu unategemea upate kazi mtu kama wewe hufai ktk benk hata ukiona siri za watu utaleta jf mambo mengine siyo ya kuleta hapa jf alafu unataja na tasisi huna ethics wewe

Mbaya zaidi wanaoendesha Interview ni Members na Guests wa hapa JF! Wanaona uzi huu halafu ....... as much as we dare to speak openly!
 
Hureeey wakuu,
Everything went well, perfect if I might say coz it waz more than I expected to be. The interview went well, the bosses jokingly ask me silly questions (tell me your first date, how many gfs you got, how many beers you can take etc.) After leaving em without no further questions. They assured me by giving me the exactly date and time theyr expecting to give me a call about the briefings. Thank you Lord and thanks for the prayers.
 

thanks God for this happines to your creature!
 
ushafeli wewe yaani badala ya kujiandaa kiakili kuwa naenda kwenye usahili ,wewe unaanza kuperuzi JF ,Sasa ukipata hiyo kazi si utakuwa unashinda tu kwenye mitandao ya kijamii badala ya kufanya kazi?
 
congrats!...but dont get ur hopes so high...not just yet...be patient...sometimes wale jamaa wanazingua
 

Hongera kwa kumaliza kitimoto salama ila hizi interview za kusubiri kama mnakwenda kumwona daktari huwa unakutana na watu wenye mbwembwe, na ndio maana huwa napenda zile kile mtu anapangiwa saa maana kisaikolojia kila mtu huwa anamwona mwenzake ni threat kutokana na mapozi anayopiga wakati anasubiri kuchomwa sindano. Kikubwa ni kujiamini tu hata mie niliwahi kukutana na mtu kapiga suti na kujiamini kupita maelezo lakini mwisho wa siku nikalamba ajira
 
jodoki Kalomilo ni kweli kuna interview nilikwenda nilikata tamaa nikiwa sijaingia na nilipanic mbaya..kuna watu wawili wanajulikana ile sehemu kila mtu apitaye anawasalimu tena kwa furaha..mm ht sijulikani daaah nilijickia vibaya ht hivyo hao maincharge nilikua nishasikia tabia zao ni wabaguzi wanapenda kupitisha walokole wenzao..basi nikichanganya na niliyaona ya kujuana nikajua sina kzz..niliingia basi tu..na kweli wakaitwa hao hao na kuajiriwa
 
Last edited by a moderator:

dah mkuu tofali nilidhani story yako itaishia kwa ushindi. dah. ila hatuchoki mkuu. pole. imeniuma na mimi.
 
Last edited by a moderator:
dah mkuu tofali nilidhani story yako itaishia kwa ushindi. dah. ila hatuchoki mkuu. pole. imeniuma na mimi.

Mimi kiukweli sijawahi kufail interview ht moja..kwa hilo nashukuru Mungu..lkn naamini Mungu hakunipangia ile kazi cz nilifunga siku ile na kusali kabla...ila km Mungu hakupanga huna sababu ya kuforce...ningeweza kuona Mungu kaninyima ile kazi kumbe alinipangia kukosa ili nipate kwingine though kwa ubinadamu unaweza mlaumu...sio siri nilivyoona kile kitendo niliumia saanaa na confidence iliisha pale pale....imagine kila mtu anawajua na anawasalimia wao...halafu wewe hujulikani ht kidgo means lile eneo ni wenyeji..bora ufanye interview ukiwa hujui wenzio
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…