Hivi chuki dhuidi ya wana diaspora na hasa toka kwa wanasiasa na watu wenye hali nzuri za kimaisha hapa nyumbani inatokana na nini?
Cha ajabu ni kuwa mawaziri na viongozi kadhaa wa serikali ya nchi hii watoto wao wana uraia wa nchi mbili mbili japo sheria hiyo haipo. Mfano Waziri wa mambo ya nchi za nje ambaye diaspora iko chini yake, Bw Bernard Membe, watoto wake ni raia wa Canada, Sisemi kuwa kuwa na uraia wa nje ni dhambi lakini ungetegemea kuwa alikuwa na uwezo wa kuwaandikisha wanae kuwa ni raia wa Tanzania lakini alikubali waandikishwe kuwa ni raiua wa Canada. Cha ajabu ni kuwa Mheshimiwa Membe amekjuwa kimya sana huku watanzania ambao wako Diaspora wakiendelea kusulubiwa na wanasiasa na vyombo vya habari hii inanipelekea kulizia kuwa hivi chuki na husda dhidi ya wana Disapora (ambao wengi wao ni watoto wa maskini) inatokana na nini hasa?
Hivi vyama vya siasa vina maoni gani kuhusu hili suala?