Chuchu Saa 6! Msaada Please

Elisha

JF-Expert Member
Feb 5, 2011
315
504
Habarini wapendwa!

Naleta kwenu kisa cha rafiki yangu mpendwa kwa mategemeo ya kupata msaada toka kwenu.

Tatizo linalomsumbua rafiki yangu huyu ni matiti yaliyotuna kifuani pake ilihali yeye ni mwanamume.

Katika watu kumi atakaokutana nao katika matembezi, tisa humcheka na kumfanyia dhihaka. Jambo hili linamnyima sana amani. Kusema kweli amekuwa kama mfungwa ndani ya gereza lake mwenyewe. Amekosa uhuru!

Kotokana na kukosa amani kila wakati, huyu bwana amejikuta akipoteza ndoto zake kila uchao.

Tatizo hili halikumuanza utotoni limempata akiwa na umri wa miaka takribani 14 hivi. Chanzo chake anasema, anahisi ni yai la kuku wa kisasa alilokula likiwa bichi akiwa na lengo la kulainisha koo kwani kuna mtu alimsimulia kuwa mayai mabichi ni kilainisho kizuri sana cha koo. Wakati huo alikuwa akipenda sana kuimba na koo lilikuwa likimsumbua. Pasipo kujiuliza vizuri mpendwa huyu alikwenda dukani na kujipatia yai la kuku wa kisasa na kulitumia kulingana na maelezo aliyopewa.

Baada ya miezi kadhaa alianza kuona mabadiliko katika mwili wake ambayo hakuyapenda mojawapo likiwa la kuchomoza kwa matiti kifuani pake. Pamoja na hilo, yalikuwepo pia mabadiliko mengine kama 'abdominal discomfort', kutoa harufu mbaya sehemu ya haja kubwa (uchafu unatoka), matatizo katika koo nk.

Japokuwa hasemi na anaonekana mwenye furaha machoni, moyoni anaumia sana! namwona ni mtu mwenye uchungu mkuu.

Madaktari wameshindwa kumsaidia jambo ambalo linazidi kumkatisha tamaa.

Ni mtu mwenye akili sana lakini ameonekana kufanya vibaya katika masomo yake ya A level na chuo kikuu.

Amekuwa hafikilii tena kuhusu maisha yake anachowaza ni jinsi gani ataondokana na tatizo hili. Naogopa endapo hali hii itaendelea atapoteza kabisa muelekeo wa maisha yake na nikiwa kama rafiki yake sipendi hilo litokee.

Hili ni tatizo gani jamani? Linatibika? Ni kweli hayo ni matokeo ya lile yai alilokula? Afanye nini sasa? Tafadhali sana naomba tumsaidie huyu mtu.
 
Stress inaongeza tatizo directly/indirectly.......... Naamini atapata majibu humu............ Pole zake though!
 
kutoa harufu mbaya sehemu ya haja kubwa (uchafu unatoka), matatizo katika koo nk.
....mkuu pole sana kwa matatizo hayo?

Lakini of all the issues ako nazo, hilo hapo juu sijui linaconnection gani na kula lile yai aisee! Vipi hapumuliwi kisogoni na midume? Bahati mbaya sio mtaalam hapa.....!
 
Stress inaongeza tatizo directly/indirectly.......... Naamini atapata majibu humu............ Pole zake though!

Nakubaliana na wewe, na ndicho kinachomsumbua hivi sasa. Kwa kifupi ameshapata vidonda vya tumbo.
 
kutoa harufu mbaya sehemu ya haja kubwa (uchafu unatoka), matatizo katika koo nk.

....mkuu pole sana kwa matatizo hayo?

Lakini of all the issues ako nazo, hilo hapo juu sijui linaconnection gani na kula lile yai aisee! Vipi hapumuliwi kisogoni na midume? Bahati mbaya sio mtaalam hapa.....!

Lol! Hapana, hakuna kitu kama hicho. Madaktari walimpima na kuthibitisha hajawahi kuingiliwa. Japokuwa niliwahi kuhisi hivyo, hisia zangu ziliondoshwa na maelezo ya daktari wake.
 
mpe pole sana rafiki yako naweza kuona anavyojisikia vbaya asa kwenye ulimwengu huu wa utandawazi kuna mengi anayosemwa asa lakuhisiwa shoga hilo alikwepi kabisa na usumbufu wa wanaume wanaopenda huo mchezo natumai atapata jibu hapa
 
Pole zako zimefika. Ni kweli huwa inamuuma sana kwa kuhisiwa shoga. Just imagine if it were you how would you react ? na hasa kama si shoga but you are treated like one. Thanks again.
 
masikini mpe pole yake,asikate tamaa aendelee kuzunguka nwenye mahospitali mbalimbali na uhakika mwisho wa siku atapata ufumbuzi
 
Kwanza nampa pole sana huyu aliyepatwa na matatizo haya. Nahisi huyu mtu mwili wake umekuwa stimulated kutoa homone ya oestrogen kwa wingi kupita kiwango cha kawaida cha mwanaume.
Inatakiwa aende hospitali na Homonal profile ifanyike, na endapo itagundulika kuwa mwili wake unatoa oestrogen kwa wingi kuna dawa atakazopewa na hiyo kitu itashrink yote.
Lakini kama ni mnene, inabidi afanye mkakati wa kupunguza uzito na hali yake yaweza kurudi kama zamani.
 
'kupumuliwa kisogoni' hakusababishi mwanaume kuvimba matiti (ingekuwa hivyo kina Sir Elton John wangeshavaa bra!), naugana na ushauri wa post no. 11....sababu kubwa inawezekana ikawa ni kutoa hormone za kike 'oestrogen' kwa wingi kiasi kumfanya hivyo, japo hiyo nayo ingefuatana na dalili nyingine kama kuwa na sauti 'mororo' n.k. Iwapo ataenda hospitali akachekiwa 'hormonal profile' basi itakuwa rahisi kwa daktari kumshauri. Kama ana kiasi kikubwa cha hormones za kike basi kuna matibabu anayoweza kupatiwa.
 
masikini mpe pole yake,asikate tamaa aendelee kuzunguka nwenye mahospitali mbalimbali na uhakika mwisho wa siku atapata ufumbuzi

Thanks a lot for you advice. Nitaendelea kumfariji na kumshauri kulingana na ushauri wako.
 
Kwanza nampa pole sana huyu aliyepatwa na matatizo haya. Nahisi huyu mtu mwili wake umekuwa stimulated kutoa homone ya oestrogen kwa wingi kupita kiwango cha kawaida cha mwanaume.
Inatakiwa aende hospitali na Homonal profile ifanyike, na endapo itagundulika kuwa mwili wake unatoa oestrogen kwa wingi kuna dawa atakazopewa na hiyo kitu itashrink yote.
Lakini kama ni mnene, inabidi afanye mkakati wa kupunguza uzito na hali yake yaweza kurudi kama zamani.

Nashukuru sana kwa msaada wako. Bahati nzuri yeye siyo mnene . Nitamshauri aende hospitali na kuangalia hiyo hormonal profile ambayo nadhani hajawahi kutazama.

Umetoa mwangaza, nadhani huu utakuwa mwanzo mzuri kwake.

Ahsante, Mungu akubariki sana.
 
'kupumuliwa kisogoni' hakusababishi mwanaume kuvimba matiti (ingekuwa hivyo kina Sir Elton John wangeshavaa bra!), naugana na ushauri wa post no. 11....sababu kubwa inawezekana ikawa ni kutoa hormone za kike 'oestrogen' kwa wingi kiasi kumfanya hivyo, japo hiyo nayo ingefuatana na dalili nyingine kama kuwa na sauti 'mororo' n.k. Iwapo ataenda hospitali akachekiwa 'hormonal profile' basi itakuwa rahisi kwa daktari kumshauri. Kama ana kiasi kikubwa cha hormones za kike basi kuna matibabu anayoweza kupatiwa.

Thank you very much for your advice Riwa. May God bless you. Thank you again.
 
Lingine baada ya ku-disturb mtiririko wa hiyo hormone anaweza kufanya hata surgery ya kuondoa hayo matiti; ni bora awe na kovu ambalo halitaweza kuonekana kiurahisi kuliko hayo matiti saa 6. I feel sorry, but certainly he will get a solution!!!!
 
Lol! Hapana, hakuna kitu kama hicho. Madaktari walimpima na kuthibitisha hajawahi kuingiliwa. Japokuwa niliwahi kuhisi hivyo, hisia zangu ziliondoshwa na maelezo ya daktari wake.

na wewe unatuchezea akili, yaani ulimchukua rafiki yako hadi kwa madaktari ili ujue kama tigo yake ipo busy?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom