Chuchu Saa 6! Msaada Please

kama mtu huna cha kuchangia ni vizuri sana ku kaa kimya na kuwaachia wenye msaada wakatoa, kwani ni lazima kila post ujibu?
watu mwe na ustarabu, mtu kauliza swali anataka msaada halafu mnakuja na kejeli:A S thumbs_down:
Anaweza akahamia Qatar/Oman atapata msaada!
 
Hpa kuna swala la hormonal imbalance.
Katika binadamu huwa tunakuwa na hormone zote lakini kwa mwanamme anakuwa na hormone kidogo sana za oestrogen/progestrogen tatizo lina kuja ni pale hizo hormone zinapokuwa zinazalishwa kwa wingi ndani ya huyo mwanamme( kadhalika na kwa wanawake kama ikitokea akawa na hormone nyingi za kiume huwa giant/loud voice ,muscular shape etc) ndio kunamfanya abadilike umbile na vionjo ndani ya mwili wake.
Kinachotakiwa hapo ni kwenda hospital na kuchukua vipimo vya hormone na gland ili kujua tatizo ni nini?
sababu lnaweza kuwa primary or secondary causes.
Kama ni primary causes maana yake hilo yai sio tatizo kabisa hata kidogo bali kuna tatizo katika mfumo mzima toka kwenye gland( sehemu hizo hormone zinapotengenezwa) hadi sehemu hizo hormone zinpokuwa discharged and released.
Na kama ni secondary caused basi aidha hilo yai linaweza kuwa ni precipitating au exacerbating/triggering causes maaana yake ni kuwa kama ikiondolewa hiyo source basi atapona maramoja.

Nadhani utakuwa umenipata vizuri.
Mpe pole sana na mwambie kuwa hayo yanaweza kuwa ni mabadiliko ya kawaida tu ya kimaumbile, hivyo asiwe na huzuni na hofu.
hilo tatizo linatibika
 
Sorry for him. I suggest that he should go to the reputable hospital and meet specialists as it seems he went to the wrong hospital meeting general doctors (wrong doctors).

I also suggest that when seeking for serious advice like this it is better to have a dissent title. This also assists to get serious viewers and responses.
 
Ndugu, kulingana na maelezo kuhusu matatizo ya huyo jamaa , ni kwamba yupo na hali ngumu sana! Tatizo la msingi ni size kubwa ya 'breasts' wakati yeye ni mme kwa jinsia. Hilo tatizo lipo miongoni mwa watu katika jamii yetu inayotuzunguka. Mara nyingi ni 'hormonal influenced'. Hormones zenyewe ni zile zinazo determine sex differentiation wakati wa ukuaji wa mwanadamu. Kwahiyo at puberty, mme na mke wana different characteristics. Mfano; mme: sauti inakua nzito na kuanza kuota ndevu. mke: sauti nyororo, matiti kuongezeka ukubwa na kuanza kupata 'menses' yaani menstruation cycle. Kwahiyo hormonal imbalance inapotokea kwa jinsia yoyote, basi inapelekea mchanganyiko wa hizo tabia kwa jinsia yoyote kulingana na hormone inayohusika. Mfano , kuna wanawake pia wana ndevu kama wanaume na pia kuna wanawake wana 'physique' kama ya kiume - kumbuka yule dada wa south Africa; Semenya!
Tukimzungumzia jamaa yetu, nadhani tatizo lake ni hormonal imbalance.
Kuhusu kutoa uchafu kwenye njia ya haja kubwa hilo ni kawaida kwa kila binadamu kwani sehemu hiyo imeumbwa kwa ajili ya kutoa kinyesi ambacho mara zote kina harufu mbaya. Mimi binafsi sijawahi kutoa kinyesi chenye harufu kama ' VANILLA au Pafyumu ya isey miyake' . Tabia mojawapo ya kinyesi ni kutoa harufu mbaya. Kama unabisha , leo nenda ukanuse kinyesi chako na utanielewa ninachokizungumza hapa. Abdominal pain au discomfort inahitaji kuchunguzwa kujua tabia zake na kupata underlying cause. Otherwise jamaa anahitaji kuwaona medical doctors for further treatment pamoja na counselling ya kutosha. Huduma ya counselling inapatika Muhimbili department ya Psychiatry. Kuhusu tatizo la maziwa makubwa akamuone gynaecologist.
 
Ahsanteni kwa mawazo na ushauri wenu. Nitaufikisha na ninaamini utazaa matunda. Mungu awabariki sana.
 
Breast surgery ndio suluhisho, lakini inabidi afanyiwe na vipimo vingine, kuna watu huwa wanakuwa phenotypically males lakini genetically females, atakuwa na enlargement ya breast, atakuwa na ovaries na hata uterus, atakuwa na clitoris kubwa(hypertrophied clitoris) ambayo yeye atadhani ni penis. Lakini pia hatakuwa na ndevu.

Ni vitu vingi vinasababisha matatizo ya ukuaji wa matiti kwa mwanaume (gynecomastia) ambavyo huanzia tumboni kabla mtoto hajazaliwa hormone (oestrogen) za mama huenda kwake na kuzaliwa na matiti ingawa ni mtoto wa kiume, pia kwenye adolescence mtu anaweza kupata matiti kwa sababu mbalimbali ikiwemo dawa (kama frusemide au lasix), pia vivimbe kwenye pituitary ambapo ndipo hormone huzaliswa na kusababisha kuongezeka kwa hormone za kike na mtu kupata hayo matatizo, sababu ni nyingi lakini kitu chochote kitakachosababisha kuongeza kwa estrogen au kupungua au kutofanya kazi kwa androgen (testosterone) hormone ya kiume husababisha mtu kuwa na maumbile ya kike pamoja na kuota matiti.

kama anaweza akafanyiwe na vipimo pia vya kigenetic na akigunduliwa ni mwanamke anaweza akachagua kuwa mwanamke au mwanaume, akafanyiwa vagina reconstruction kama atapenda kuwa mwanamke, lakini kwa kuwa amekua kama mwanaume ni better akafanywa mwanaume, ataondolewa matiti, ovaries na uterus, halafu atapewa testosterone ili adevelop male characteristics.

Kama gyanecomastia yake si kwa ajili ya hormonal imbalance, yaani kuzidi kwa hormone ya kike (oestrogen) au mwili kukosa response ya hormone ya kiume (androgen insensitivity) matibabu yake ni rahisi tu, kukata hayo matiti na maisha yataendelea.

Namuona huruma sana kwani ni kweli hali hii inaleta sana emotional stress.
 
Habarini wapendwa!

Naleta kwenu kisa cha rafiki yangu mpendwa kwa mategemeo ya kupata msaada toka kwenu.

Tatizo linalomsumbua rafiki yangu huyu ni matiti yaliyotuna kifuani pake ilihali yeye ni mwanamume.

Katika watu kumi atakaokutana nao katika matembezi, tisa humcheka na kumfanyia dhihaka. Jambo hili linamnyima sana amani. Kusema kweli amekuwa kama mfungwa ndani ya gereza lake mwenyewe. Amekosa uhuru!
Kotokana na kukosa amani kila wakati, huyu bwana amejikuta akipoteza ndoto zake kila uchao.

Tatizo hili halikumuanza utotoni limempata akiwa na umri wa miaka takribani 14 hivi. Chanzo chake anasema, anahisi ni yai la kuku wa kisasa alilokula likiwa bichi akiwa na lengo la kulainisha koo kwani kuna mtu alimsimulia kuwa mayai mabichi ni kilainisho kizuri sana cha koo. Wakati huo alikuwa akipenda sana kuimba na koo lilikuwa likimsumbua. Pasipo kujiuliza vizuri mpendwa huyu alikwenda dukani na kujipatia yai la kuku wa kisasa na kulitumia kulingana na maelezo aliyopewa.

Baada ya miezi kadhaa alianza kuona mabadiliko katika mwili wake ambayo hakuyapenda mojawapo likiwa la kuchomoza kwa matiti kifuani pake. Pamoja na hilo, yalikuwepo pia mabadiliko mengine kama 'abdominal discomfort', kutoa harufu mbaya sehemu ya haja kubwa (uchafu unatoka), matatizo katika koo nk.

Japokuwa hasemi na anaonekana mwenye furaha machoni, moyoni anaumia sana! namwona ni mtu mwenye uchungu mkuu.

Madaktari wameshindwa kumsaidia jambo ambalo linazidi kumkatisha tamaa.

Ni mtu mwenye akili sana lakini ameonekana kufanya vibaya katika masomo yake ya A level na chuo kikuu.

Amekuwa hafikilii tena kuhusu maisha yake anachowaza ni jinsi gani ataondokana na tatizo hili. Naogopa endapo hali hii itaendelea atapoteza kabisa muelekeo wa maisha yake na nikiwa kama rafiki yake sipendi hilo litokee.

Hili ni tatizo gani jamani? Linatibika? Ni kweli hayo ni matokeo ya lile yai alilokula? Afanye nini sasa? Tafadhali sana naomba tumsaidie huyu mtu.

Re: Chuchu Saa 6! Msaada Please

pole sana, naona kweli upo katika wakati mgumu. Tatizo ulilonalo hutokea na wewe si wa kwanza. Zipo sababu nyingi ambazo zinaweza kusababisha tatizo hilo.Tatizo hilo laweza tokea wakati wa uchanga yaani mara tu baada ya kuzaliwa, au wakati wa kubalehe au wakati baada ya kubalehe au wakati wowote katika umri wa mwanadamu.
Sababu zipo nyingi na hutegemeana hasa na umri wa mwathirika. Hata hivyo sababu kubwa huwa ni uwiano mbaya wa vichocheo vya mwili. (hormonal imbalance). Sababu nyingine ni matumizi ya madawa kwa kutibu ugonjwa mwingine. Hapa nina maana kuna baadhi ya dawa unapozitumia kwa ajili ya kutibu ugonjwa fulani zinaweza zikawa na athari hizo.
Tiba ya matiti kuwa makubwa inapatikana katika hospitali nyingi, hukusema upo wapi na ulienda hospitali gani. Nenda hospitali umtafute daktari bingwa wa magonjwa ya ndani yaani Physician kama itahitaji matumizi ya dawa tu. Kama dawa pekee hazitakusaidia atakurifaa kwa daktari bingwa wa upasuaji ambapo utafanyiwa operesheni na yatapona kabisa.
Sidhani kama shida ya kutoka uchafu sehemu ya nyuma inahusiana na hilo. Japo ni dhahiri kuwa kwa mwanadamu akipata ugonjwa moja upo uwezekano akapata na mwingine. Na hii hutokana na sababu kuwa aidha ugonjwa wa mwanzo unaweza kuathiri zaidi ya system moja au system moja iloyoathirika inaweza ikasababisha matatizo kwenye system ingine. Cha muhimu tu ni kuwa hali hiyo nayo hutokea na inatibika pasipo shaka, kwa kuwaona au physician au surgeon.

kwanza wakati wa uchanga yaani mara baada ya kuzaliwai,matiti ya mtoto yanaweza yakawa makubwa wakati mwingine hata yakatoa maziwa
 
Habarini wapendwa!

Naleta kwenu kisa cha rafiki yangu mpendwa kwa mategemeo ya kupata msaada toka kwenu.

Tatizo linalomsumbua rafiki yangu huyu ni matiti yaliyotuna kifuani pake ilihali yeye ni mwanamume.

Katika watu kumi atakaokutana nao katika matembezi, tisa humcheka na kumfanyia dhihaka. Jambo hili linamnyima sana amani. Kusema kweli amekuwa kama mfungwa ndani ya gereza lake mwenyewe. Amekosa uhuru!

Kotokana na kukosa amani kila wakati, huyu bwana amejikuta akipoteza ndoto zake kila uchao.

Tatizo hili halikumuanza utotoni limempata akiwa na umri wa miaka takribani 14 hivi. Chanzo chake anasema, anahisi ni yai la kuku wa kisasa alilokula likiwa bichi akiwa na lengo la kulainisha koo kwani kuna mtu alimsimulia kuwa mayai mabichi ni kilainisho kizuri sana cha koo. Wakati huo alikuwa akipenda sana kuimba na koo lilikuwa likimsumbua. Pasipo kujiuliza vizuri mpendwa huyu alikwenda dukani na kujipatia yai la kuku wa kisasa na kulitumia kulingana na maelezo aliyopewa.

Baada ya miezi kadhaa alianza kuona mabadiliko katika mwili wake ambayo hakuyapenda mojawapo likiwa la kuchomoza kwa matiti kifuani pake. Pamoja na hilo, yalikuwepo pia mabadiliko mengine kama 'abdominal discomfort', kutoa harufu mbaya sehemu ya haja kubwa (uchafu unatoka), matatizo katika koo nk.

Japokuwa hasemi na anaonekana mwenye furaha machoni, moyoni anaumia sana! namwona ni mtu mwenye uchungu mkuu.

Madaktari wameshindwa kumsaidia jambo ambalo linazidi kumkatisha tamaa.

Ni mtu mwenye akili sana lakini ameonekana kufanya vibaya katika masomo yake ya A level na chuo kikuu.

Amekuwa hafikilii tena kuhusu maisha yake anachowaza ni jinsi gani ataondokana na tatizo hili. Naogopa endapo hali hii itaendelea atapoteza kabisa muelekeo wa maisha yake na nikiwa kama rafiki yake sipendi hilo litokee.

Hili ni tatizo gani jamani? Linatibika? Ni kweli hayo ni matokeo ya lile yai alilokula? Afanye nini sasa? Tafadhali sana naomba tumsaidie huyu mtu.

Re: Chuchu Saa 6! Msaada Please

Tatizo hilo huweza kutokea wakati wa uchanga, yaani mara tu mtoto anapozaliwa (na hata kinaweza kitoe maziwa) wakati wa kubalehe, wakati wa utu uzima au wakati wowote wakati wa uhai wa mwanadamu.
Kimsingi sababu zipo nyingi, hata hivyo kubwa kati ya hizo ni uwiiano mbaya wa vichocheo vya mwiilini (Hormonal imbalance). Sababu nyingine huwa ni matumizi ya baadhi ya madawa. Kuna dawa unapozitumia kwa sababu ya kutibu baadhi ya magonjwa zinaweza zilete athari hizo. Pia yapo baadhi ya magonjwa haswa ya ini yanaweza yasababishe hali hiyo.
Ugonjwa huu wa kuwa na matiti makubwa unatibika. Hukusema upo wapi ulienda hosp. gani na ulimwona daktari mwenye ujazi gani. Kwa sababu daktari anayeweza kukutibu ni pysician kama itahitaji matumizi ya dawa tu. Na kama uchunguzi utaonesha unahitaji upasuaji basi utapata rufaa kwenda kumuona surgeon. Cha muhimu naomba ufahamu kuwa unatibika hospitalini pasipo shaka.

Kuhusu suala la kutokwa na uchafu wenye harufu sehemu ya nyuma nalo linaweza sababishwa na mambo mengi. Cha muhumu ni kwamba nalo linatibika vizuri ikiwa utawaona wataalamu niliowaandika hapo juu.
Pole sana utapona ukiwaona wataalamu. Usione aibu kuwaeleza madaktari.
 
Mjepu mbona wafanya masihara ilhali mwenzio anataabika! pole mkuu, nafikiri umepata pa-kuanzia! what next is to take action!
 
Ndugu, kulingana na maelezo kuhusu matatizo ya huyo jamaa , ni kwamba yupo na hali ngumu sana! Tatizo la msingi ni size kubwa ya 'breasts' wakati yeye ni mme kwa jinsia. Hilo tatizo lipo miongoni mwa watu katika jamii yetu inayotuzunguka. Mara nyingi ni 'hormonal influenced'. Hormones zenyewe ni zile zinazo determine sex differentiation wakati wa ukuaji wa mwanadamu. Kwahiyo at puberty, mme na mke wana different characteristics. Mfano; mme: sauti inakua nzito na kuanza kuota ndevu. mke: sauti nyororo, matiti kuongezeka ukubwa na kuanza kupata 'menses' yaani menstruation cycle. Kwahiyo hormonal imbalance inapotokea kwa jinsia yoyote, basi inapelekea mchanganyiko wa hizo tabia kwa jinsia yoyote kulingana na hormone inayohusika. Mfano , kuna wanawake pia wana ndevu kama wanaume na pia kuna wanawake wana 'physique' kama ya kiume - kumbuka yule dada wa south Africa; Semenya!
Tukimzungumzia jamaa yetu, nadhani tatizo lake ni hormonal imbalance.
Kuhusu kutoa uchafu kwenye njia ya haja kubwa hilo ni kawaida kwa kila binadamu kwani sehemu hiyo imeumbwa kwa ajili ya kutoa kinyesi ambacho mara zote kina harufu mbaya. Mimi binafsi sijawahi kutoa kinyesi chenye harufu kama ' VANILLA au Pafyumu ya isey miyake' . Tabia mojawapo ya kinyesi ni kutoa harufu mbaya. Kama unabisha , leo nenda ukanuse kinyesi chako na utanielewa ninachokizungumza hapa. Abdominal pain au discomfort inahitaji kuchunguzwa kujua tabia zake na kupata underlying cause. Otherwise jamaa anahitaji kuwaona medical doctors for further treatment pamoja na counselling ya kutosha. Huduma ya counselling inapatika Muhimbili department ya Psychiatry. Kuhusu tatizo la maziwa makubwa akamuone gynaecologist.

Mkuu hapo kwenye red umenchekesha sana..kinyesi chenye harufu ya Isey Miyake!!!
Ila nadhani alikuwa anamaanisha kutokwa na uchafu tofauti na kinyesi...yaani uchafu kutoka wenyewe bila kwenda chooni unakuta tu "ushajichafua"
 
Mbarikiwe wote, mliotoa ushauri mzuri kwa huyo mpendwa.
Nawashauri wale wanoleta mzaha kwenye mambo muhimu kama haya waache,
Kuna jukwaa la umbea na udaku na utani na stress free zone MMU nendeni huko,

Hili jukwaa nahisi lingekuwa kama linavyotakiwa liwe, kuna watu wana matatizo ya kiafya kweli, na
wakati mwingine hawezi kuyasema popote lakini anaweza akawa na uhuru wa kulisema hapa!!

Nawaomba wale wote wenye ujuzi (madaktari na nk nk ) msikae mbali na jukwaa hili ili
mweze kutoa msaada kwa matatizo mbalimbali kwa wakati pia.
Mbarikiwe Zaidi na Zaidi.
 
Habarini wapendwa!

Naleta kwenu kisa cha rafiki yangu mpendwa kwa mategemeo ya kupata msaada toka kwenu.

Tatizo linalomsumbua rafiki yangu huyu ni matiti yaliyotuna kifuani pake ilihali yeye ni mwanamume.

Katika watu kumi atakaokutana nao katika matembezi, tisa humcheka na kumfanyia dhihaka. Jambo hili linamnyima sana amani. Kusema kweli amekuwa kama mfungwa ndani ya gereza lake mwenyewe. Amekosa uhuru!

Kotokana na kukosa amani kila wakati, huyu bwana amejikuta akipoteza ndoto zake kila uchao.

Tatizo hili halikumuanza utotoni limempata akiwa na umri wa miaka takribani 14 hivi. Chanzo chake anasema, anahisi ni yai la kuku wa kisasa alilokula likiwa bichi akiwa na lengo la kulainisha koo kwani kuna mtu alimsimulia kuwa mayai mabichi ni kilainisho kizuri sana cha koo. Wakati huo alikuwa akipenda sana kuimba na koo lilikuwa likimsumbua. Pasipo kujiuliza vizuri mpendwa huyu alikwenda dukani na kujipatia yai la kuku wa kisasa na kulitumia kulingana na maelezo aliyopewa.

Baada ya miezi kadhaa alianza kuona mabadiliko katika mwili wake ambayo hakuyapenda mojawapo likiwa la kuchomoza kwa matiti kifuani pake. Pamoja na hilo, yalikuwepo pia mabadiliko mengine kama 'abdominal discomfort', kutoa harufu mbaya sehemu ya haja kubwa (uchafu unatoka), matatizo katika koo nk.

Japokuwa hasemi na anaonekana mwenye furaha machoni, moyoni anaumia sana! namwona ni mtu mwenye uchungu mkuu.

Madaktari wameshindwa kumsaidia jambo ambalo linazidi kumkatisha tamaa.

Ni mtu mwenye akili sana lakini ameonekana kufanya vibaya katika masomo yake ya A level na chuo kikuu.

Amekuwa hafikilii tena kuhusu maisha yake anachowaza ni jinsi gani ataondokana na tatizo hili. Naogopa endapo hali hii itaendelea atapoteza kabisa muelekeo wa maisha yake na nikiwa kama rafiki yake sipendi hilo litokee.

Hili ni tatizo gani jamani? Linatibika? Ni kweli hayo ni matokeo ya lile yai alilokula? Afanye nini sasa? Tafadhali sana naomba tumsaidie huyu mtu.

Tatizo linalomsumbua rafiki yangu huyu ni matiti yaliyotuna kifuani pake ilihali yeye ni mwanamume.

alikwenda hospitali gani? alionana na daktari mwenye taaluma gani? ukisema madaktari wameshindwa kumsaidia una maana gani ni ugonjwa hawaujui au hauna tiba?
kwa kifupi ni kuwa tatizo hilo kitalaamu linaitwa gyanocomastia. laweza kutokea wakatu wowote. laweza tokea mara tu baada ya kuzaliwa ambapo hupotea lenyewe muda mfupi, au laweza tokea wakati wa kubalee, au laweza tokea wakati wowote wa uhai. Ni muhimu sana kujua lilitokea katika umri gani kwa sababu visababishi ni vingi, navyo hutegemeana na umri wakati alipopata tatizo hilo.
Baadhi ya sababu ni pamoja na kupokea vichocheo (hormones)kutoka kwa mama wakati wa uchanga. vichocheo hivyo huvimbisha matiti. Bahati ni kwamba vitoto vinavyopata shida hiyo hupotea yenyewe muda mfupi. kwa watu wazima sababu kubwa huwa ni uwiiano mbaya wa vichocheo mwilini (hormonal imbalance). kunapokuwa na uwiiano huo mbaya hufanya matiti yawe makubwa. zipo sababu nyingine kama vile matumizi ya baadhi ya madawa.
Tiba nenda hospitalini kamuone daktari mwenye ujuzi wa internal medicine (physcian) yeye atakufanyia uchunguzi na anaweze akutibu na dawa na upone. Wakati mwingine dawa pekee zaweza zisikusaidie, na hivyo aweza kukupatia rufaa kwenda kwa surgeon ambapo operation itafanyika na utapona kabisa. Cha nyongeza ni kuwa ni vizuri zaidi kama shida hiyo itatibiwa hospitali ya rufaa na uhakikishe unaonana na madaktari niliowataja hapo juu, yaani physycian au surgeon.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom