Christopher Bageni agonga mwamba Mahakamani, sasa anasubiri Kunyongwa tu

Presidential Prerogative of Mercy.......may be anaweza kutokea huko kwa kuwa aliyokuwa anayafanya kwa sasa yanafanyika sana
 
Maisha yana formula...nayo ni mtu unapaswa kuwa mnyenyekevu, mcha Mungu, usiye na majivuno, mpenda haki, unayechukia rushwa na maovu yote, mwenye nidhamu na usiye na chembe ya sifa ya ukatili...
Aliyepaki gari kumuokoa dereva wa lori la mafuta Msamvu aliteketea kwa moto
 
Nakumbuka aliriport Alfred Masako....

Mwenye bakuri hayaaaaa
Mwenye ndoo hayaaaaa
Mwenye kidumu hayaaaa
Kizazaa ni paale jamaa akipotaka kuchomoa betriii....moto ukaripukaaa....pale ikawa patashiika nguo kuchanikaaa
 
Kanikumbusha wale wauza madini waliouawa kinyama,yule RPC wa mkoa flani anaitwa Zombe alipona vipi?Maana baada ya tukio eti akapata uhamisho kwenda kuwa RPC kama sikosei Rukwa.
Alirudishwa akaunganishwa katika kesi akaahinda akaachiwa
 
Ina maana hii kesi ilikuwa bado kutolewa hukumu tokea Enzi zile...!
Waliachiwa wote baadae serikali ikakata rufaa , naye badala ya kujiongeza na kusepa,baada kupita kama miaka 5 akakamatwa tena ndiyo yakamkuta hayo ya kunyongwa,mwenzie Makele yuko sentro anakula tu kipupwe,Zombe sijui kafia wapi,lakini nasikia kachoka anatembelea rimu.
 
Kanikumbusha wale wauza madini waliouawa kinyama,yule RPC wa mkoa flani anaitwa Zombe alipona vipi?Maana baada ya tukio eti akapata uhamisho kwenda kuwa RPC kama sikosei Rukwa.
Hii ishu ilikuwa imuondoe tiba ila bahati nzuri alikuwa likizo ,jumba bovu likamwangukia zombe ila inaonesha hizi zilikiwa dili zao za kupata pesa kwa kuwazurumu watu maisha
 
Halafu mimi huwa nawashangaa sana wale wanaosema adhabu ya kunyongwa iondolewe.

Yaani hata kwa mtu kama huyu Bageni naye asinyongwe?Kwamba ni halali awaue wengine kwa ukatili,awatangulize mbele ya haki ila yeye aachwe anapumua duniani?

Aiseee mtakuwa hamjui uchungu wa kuuawa kwa watu wenu wa karibu.Nasisitiza ADHABU YA KIFO ISIFUTWE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…