Christopher Bageni agonga mwamba Mahakamani, sasa anasubiri Kunyongwa tu

Presidential Prerogative of Mercy.......may be anaweza kutokea huko kwa kuwa aliyokuwa anayafanya kwa sasa yanafanyika sana
 
Maisha yana formula...nayo ni mtu unapaswa kuwa mnyenyekevu, mcha Mungu, usiye na majivuno, mpenda haki, unayechukia rushwa na maovu yote, mwenye nidhamu na usiye na chembe ya sifa ya ukatili...
Aliyepaki gari kumuokoa dereva wa lori la mafuta Msamvu aliteketea kwa moto
 
Bro labda kipindi kile cha akina zombe yeye alikuwa na 10 yrs. sasa ana 25+yrs. Sidhani kama atajua kinachoongelewa hapa. Ni sawa wale wa kuchota mafuta Moro, wakati wengine walipo kuwa wanaungua kule Mbeya, pengine wao walikuwa 11 and below, umri huo wala hawakujua kilichotokea, 20yrs from then wana below 31. Hawakumbuki kitu, ndiyo maana lori lilipo anguka walikimbilia eneo na tukio wakiwa na madumu. Matokeo yakawa, tukio lilelile lililotukia miaka 20 iliyopita likajirudia.
Nakumbuka aliriport Alfred Masako....

Mwenye bakuri hayaaaaa
Mwenye ndoo hayaaaaa
Mwenye kidumu hayaaaa
Kizazaa ni paale jamaa akipotaka kuchomoa betriii....moto ukaripukaaa....pale ikawa patashiika nguo kuchanikaaa
 
Kanikumbusha wale wauza madini waliouawa kinyama,yule RPC wa mkoa flani anaitwa Zombe alipona vipi?Maana baada ya tukio eti akapata uhamisho kwenda kuwa RPC kama sikosei Rukwa.
Alirudishwa akaunganishwa katika kesi akaahinda akaachiwa
 
Ina maana hii kesi ilikuwa bado kutolewa hukumu tokea Enzi zile...!
Waliachiwa wote baadae serikali ikakata rufaa , naye badala ya kujiongeza na kusepa,baada kupita kama miaka 5 akakamatwa tena ndiyo yakamkuta hayo ya kunyongwa,mwenzie Makele yuko sentro anakula tu kipupwe,Zombe sijui kafia wapi,lakini nasikia kachoka anatembelea rimu.
 
Kanikumbusha wale wauza madini waliouawa kinyama,yule RPC wa mkoa flani anaitwa Zombe alipona vipi?Maana baada ya tukio eti akapata uhamisho kwenda kuwa RPC kama sikosei Rukwa.
Hii ishu ilikuwa imuondoe tiba ila bahati nzuri alikuwa likizo ,jumba bovu likamwangukia zombe ila inaonesha hizi zilikiwa dili zao za kupata pesa kwa kuwazurumu watu maisha
 
Halafu mimi huwa nawashangaa sana wale wanaosema adhabu ya kunyongwa iondolewe.

Yaani hata kwa mtu kama huyu Bageni naye asinyongwe?Kwamba ni halali awaue wengine kwa ukatili,awatangulize mbele ya haki ila yeye aachwe anapumua duniani?

Aiseee mtakuwa hamjui uchungu wa kuuawa kwa watu wenu wa karibu.Nasisitiza ADHABU YA KIFO ISIFUTWE.
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom