Jimbi
JF-Expert Member
- Aug 16, 2010
- 3,951
- 4,264
Mkuu, wewe kama unajua alipo huyo askari kuna ubaya gani ukiweka wazi hapa? Unaogopa kitu gani Mkuu wangu? Ama wewe ndio Abdallah Zombe anayetajwa kikombe cha hukumu kumpitia mbali?Nauliza swali japo najua wewe si mhusika na unaweza usiwe na jibu. Hivi ni nani aliyemtorosha yule polisi aliyefyatua risasi ambaye ndiye kimsingi aliwauwa? Ni yeye alitoroka mwenyewe au kuna watu wako nyuma yake? Je hivi kweli serikali haijui aliko? Kuna juhudi zozote za kumtafuta kutoka kwa serikali? Laiti nchi yetu ingekuwa na waandishi wa habari wa ukweli wangechunguza mpaka wangejua alipo.