Christopher Bageni agonga mwamba Mahakamani, sasa anasubiri Kunyongwa tu

Erythrocyte

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Messages
62,932
Points
2,000
Erythrocyte

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2012
62,932 2,000
fb_img_1565787531747-jpg.1181240


Hii ni baada ya Mahakama kuifutilia mbali kesi yake ya kuomba uamuzi wa Mahakama kuu iliyomhukumu kunyongwa upitiwe upya .

Kwa faida ya wageni wa JF na wengine ni kwamba huyu Bageni ni mmoja wa washirika wa Abdallah Zombe kwenye Mauaji na uporaji wa mihela ya wafanyabiashara wa madini kutoka Morogoro uliotikisa nchi na kulidhalilisha jeshi la Polisi

12fd8421-e8d1-4fcd-90eb-b4432d6728ae-jpeg.1181803


======


DAR: RUFAA DHIDI YA HUKUMU YA KIFO KWA ALIYEKUWA MKUU WA UPELELEZI WA KINONDONI YAGONGA MWAMBA

Matumaini ya kukata rufaa yamefifia baada ya Mahakama ya Rufani kutupilia mbali maombi hayo yaliyowakilishwa na Wakili wa aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kinondoni, Christopher Bageni

Bageni aliiomba Mahakama iridhie kumfutiwe adhabu ya kunyongwa kwa kosa la mauaji ya Wafanyabiashara 3 wa madini kutoka Mahenge, Morogoro

Uamuzi huu wa Mahakama, umehitimisha kesi hii iliyodumu kwa miaka 13 tangu washtakiwa walipopandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza mwaka 2006

Tangu wakati huo washtakiwa walikuwa wakipungua katika kila hatua ya kesi, hadi kubakia ndugu Christopher Bageni pekee

Washtakiwa wengine waliowahi kujumuishwa katika kesi hii kabla ya kuachiwa huru ni aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar(RCO), Kamishna Msaidizi wa Polisi(ACP), Abdallah Zombe, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi, Kituo cha Polisi Urafiki, Mrakibu Msaidizi wa Polisi(ASP), Ahmed Makelle, na Askari wa Kituo cha Polisi Oysterbay, Rajabu Bakari


Zaidi soma.....

Mahakama yatupa rufani ya Bageni, ahukumiwa kunyongwa hadi kufa

-kwamba inatupilia mbali maombi yake ya mapitio.

Kadhalika, imesema imeangalia mwenendo mzima wa kesi, lakini haijaona kitu kipya katika hoja za mapitio zilizowasilishwa na mlalamikaji na kwamba ilitimiza majukumu yake kama Mahakama ya Kwanza ya Rufani.

Uamuzi huo ulisomwa jana na Naibu Msajili Mwandamizi, Elizabeth Mkwizu baada ya maombi hayo kusikilizwa na jopo la majaji watatu likiongozwa na Jaji Stella Mugasha, Ferdinand Wambari na Rehema Kerefu.

Hukumu hiyo inatokana na kesi ya msingi ya wafanyabiashara wanne wa madini kutoka Mahenge, Morogoro waliodaiwa kuuawa na polisi ambao ni Sabinus Chigumbi, maarufu Jongo na ndugu yake, Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe na dereva teksi, mkazi wa Manzese Dar es Salaam, Juma Ndugu.

Msajili alisema Mahakama ya Kwanza ya Rufani ina wajibu wa kuangalia kilichotokea katika ushahidi ili iweze kutimiza majukumu yake ya utoaji haki.

Alisema wakati hukumu iliyotolewa dhidi ya mshtakiwa, mahakama hiyo haikufanya kosa la kuathiri haki ya mshtakiwa kwa kuzingatia mambo mawili.

Moja, mahakama ilipomtia hatiani ilizingatia ushahidi uliotolewa na mshtakiwa mwenzake Rajabu Bakari, ambaye alishuhudia tukio la mauaji hayo.

Pili, katika msitu wa Pande mshtakiwa ndiye alikuwa ofisa wa juu kuliko wote ingawa Rajabu hakusikia akitoa amri ya kufanyika mauaji, lakini kwa mujibu wa Jeshi la Polisi ofisa wa juu ndiye mwenye mamlaka ya kutoa amri.

Jopo limeridhika na ushahidi huo na kwamba uliungwa mkono kwa namna nyingi na Bageni ikiwamo mwenendo wake baada ya tukio hilo.

Msajili aliendelea kusoma kuwa, Bageni alidanganya kwa viongozi wake kwamba kulikuwa na majibishano ya risasi kati ya wafanyabiashara na polisi eneo la Sinza, jijini Dar es Salaam huku akijua si kweli.

Hata hivyo, ushahidi wa Jamhuri unaeleza hapakuwa na majibishano ya risasi siku ya tukio.

Pia, Bageni aliamuru askari kwenda kupiga risasi baharini na kuonyesha maganda tisa kwa viongozi wake huku akijua si kweli.

"Mahakama hii imeona kwamba Bageni ameshindwa kuishawishi mahakama kwamba ilikosea kumtia hatiani, hatuna namna zaidi ya kutupilia mbali maombi yake," alisema Msajili Mkwizu, akinukuu jopo lililosikiliza maombi hayo.

Mapema mahakamani hapo, Bageni alifungua maombi ya mapitio akitaka imwachie huru kwa sababu uamuzi wa Mahakama ya Rufani Tanzania, uliomtia hatiani hakupata nafasi ya kujitetea.

Kadhalika, alidai kuwa uamuzi wa rufani iliyomtia hatiani iliyofunguliwa na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), ilikuwa na hoja za kisheria na kwamba mlalamikaji Bageni hakupata nafasi ya kujibu na kujitetea.

Wakili wa upande wa mlalamikaji, Gaudiosis Ishengoma, wakati akiwasilisha hoja za mapitio mbele ya jopo la majaji watatu, likiongozwa na Jaji Mugasha, Wambari na Kerefu.

Ishengoma alidai kuwa maombi ya mlalamikaji dhidi ya DPP ni kuiomba mahakama kufanya mapitio ya uamuzi wake wa Septemba 16, 2016, uliomtia hatiani kigogo huyo wa zamani wa polisi.

Vile vile, alidai kuwa uamuzi huo ulikuwa unalenga kutengua hukumu ya Mahakama Kuu iliyowaachia huru baada ya ushahidi wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha tuhuma za mauaji ya wafanyabiashara watatu na dereva taksi mmoja.

Alidai kuwa pamoja na mambo mengine mamlaka ya mahakama hiyo ni kufanya mapitio uamuzi wake pale inapotokea ukiukwaji wa haki haiwezi kuachwa ikawa hivyo.

"Kwa uhalisia wa kesi hii rufani iliyoletwa na DPP, mlalamikaji hakupata nafasi ya kusikilizwa wakati Mahakama ya Rufani ilipotengua uamuzi wa kumtia hatiani, uamuzi huo wa Mahakama Kuu katika kutafsiri kifungu cha kanuni ya 22 na cha 23 ya adhabu kwamba huwezi kumtia hatiani mtu aliyesaidia kuua ukamwacha aliyeua," alidai Ishengoma.

Upande wa mlalamikiwa DPP ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ladislais Komanya, ulidai kuwa mlalamikaji hana sababu za msingi za kutengua uamuzi uliomtia hatiani.

Komanya alidai kuwa rufani ya kesi hiyo ilishasikilizwa kwamba sasa si wakati wake kusikilizwa kwa mgongo wa mapitio.

Alidai kuwa SP Bageni alipata nafasi ya kusikilizwa na kwamba mahakama itupilie mbali mapitio hayo.

"Mahakama hii ilitoa uamuzi wake kupitia hukumu ya Mahakama Kuu ikionyesha kuwa ilitolewaje, jopo la majaji lilijadili kwa kina hukumu ya mahakama ya chini na uamuzi wake ulikuwa sahihi," alidai na kuongeza:

"Mahakama hii ina uwezo wa kusikiliza jambo na kulifanyia uamuzi kwa hiyo mambo yatakayoletwa yazingatie kifungu cha 66 kidogo cha (1) (b) cha kanuni ya adhabu, maombi ya mlalamikaji tunaona hayajakidhi vigezo vinavyotakiwa, kwa kuruhusu maombi kama haya ambayo hayafiki mwisho, tunafungua mwanya kwa wengine yatupiliwe mbali," alidai Komanya.

Katika maombi yake SP Bageni, alipinga hukumu iliyotolewa katika mahakama hiyo chini ya jopo la majaji watatu likiongozwa na Jaji Bernard Luanda, Sauda Mjasiri na Senistocles Kaijage, kwamba lilifanya makosa ya dhahiri.

Pia, alidai kuwa jopo hilo lilifanya makosa katika mwonekano na kusababisha haki kutokuzingatiwa mahakama hiyo itengue hukumu hiyo.

Septemba 16, 2016, 3:45 asabuhi, Msajili wa mahakama hiyo (kwa sasa Jaji wa Mahakama Kuu), John Kahyoza, alisoma hukumu hiyo baada ya kusikilizwa rufani iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP).

DPP alipinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyowaachia huru aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) Kamishna Msaidizi wa Polisi wa zamani, Abdallah Zombe na maofisa wenzake watatu akiwamo Bageni, mwaka 2009.

Akisoma hukumu hiyo Msajili Kahyoza, aliwataja walalamikiwa kuwa ni ACP Zombe, SP Bageni, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Kituo cha Polisi Urafiki, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Ahmed Makelle na Rajabu Bakari.

Alisema Mahakama ya Rufani ilipitia ushahidi uliotolewa Mahakama Kuu na kuona kwamba ilishindwa kuwatia hatiani washtakiwa kwa mauaji na kwa kosa la kusaidia mauaji kufanyika.

"Kosa la kuua na kosa la kusaidia kuua ni makosa mawili tofauti, si sahihi kwa mtu aliyeshtakiwa kwa mauaji kutiwa hatiani kwa kosa jingine, tangu mwanzo mshtakiwa alitakiwa kulijua ili aweze kujitetea," alisema na kuongeza:

"Washtakiwa wote katika utetezi wao walipinga kuhusika katika mauaji hayo, lakini mlalamikiwa wa nne Rajabu alisema ukweli katika ushahidi wake kwa kueleza tukio la mauaji lilivyofanyika katika msitu wa Pande, lakini ushahidi wake ulitakiwa kupokelewa kwa makini na ulitakiwa kuwapo na ushahidi mwingine wa kuunga mkono," alisema Msajili Kahyoza.

Akifafanua msajili alisema, “mlalamikiwa wa kwanza Zombe, mahakama haioni kama kuna ushahidi wa kumtia hatiani kwa mauaji wala kwa kusaidia kuua japo kuna jambo kichwani mwake ninalolifahamu kuhusu mauaji hayo, ushahidi mwingine unaonyesha wajibu rufani watatu walishuhudia mauaji, lakini hawakuua," linasema jopo.

Jopo lilisema wamekubaliana kwamba watu wanne waliuawa kwa bunduki na mauaji yalikuwa ya kinyama katika msitu wa Pande.

“Mahakama hiyo ilijiuliza maswali kwamba je, wajibu rufani walikuwapo Pande? Jibu ni kwamba walalamikiwa wa pili, wa tatu na wa nne walikuwapo katika msitu huo na kwamba mlalamikiwa wa nne alisema ukweli mahakamani kuhusiana na tukio hilo.”

Ilidaiwa kwamba mauaji hayo yalifanywa na askari polisi Sadi, lakini mshtakiwa huyo hajawahi kushtakiwa, mahakama inajiuliza marehemu walipelekwa Pande kwa amri ya nani.

Kwa mujibu wa ushahidi mahakama inajiuliza nini nia ya kuwapeleka marehemu Pande sehemu ambayo haina hata nyumba, mlalamikiwa wa pili, Bageni ndiye alitoa amri ya kuua, ushahidi unaonyesha washtakiwa waliwapeleka wakiwa hai Pande na waliwarejesha wakiwa marehemu.

"Marehemu walipelekwa huko ili tukio la mauaji lifanyike bila kipingamizi kwa kibali cha Bageni, ushahidi wa mlalamikiwa wa nne uliungwa mkono na tabia ya Bageni kwamba alikuwa akificha ukweli kuhusu mauaji hayo," alisema.

Hata hivyo, ushahidi wa maofisa watatu wa Jeshi la Polisi, wote walidanganya kwamba mauaji yalitokea Sinza katika majibizano kati ya Polisi na marehemu wakati wengine wa Sinza walisema hawakusikia tukio la aina hiyo kutokea.

"Mahakama hii imeona walalamikiwa wa kwanza, wa tatu na wa nne, rufani dhidi yao inatupwa hakuna ushahidi wa kuwatia hatiani, mlalamikiwa mahakama inatengua kuachiwa kwake kutiwa hatiani na Mahakama Kuu, inamuhukumu kunyongwa hadi kufa kwa mauaji ya watu wanne," alisema Msajili Kahyoza na kusababisha mahakama hiyo kulipuka kwa vilio.

Katika kesi ya msingi, wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge, Morogoro waliouawa ni Sabinus Chigumbi, maarufu Jongo na ndugu yake, Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe na dereva teksi, mkazi wa Manzese Dar es Salaam, Juma Ndugu.

Walidaiwa kutenda makosa hayo Januari 14, 2006, katika msitu wa Pande, uliopo wilayani Kinondoni baada ya kuwakamata wafanyabiashara hao Sinza, walipokuja Dar es Salaam kuuza madini.


Chanzo: Nipashe
 
Kurzweil

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Messages
6,204
Points
2,000
Kurzweil

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined May 25, 2011
6,204 2,000
Mahakama ya Rufani imetupilia mbali maombi ya kupitia upya uamuzi wa kesi ya aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kinondoni, Christopher Bageni ya kutaka afutiwe adhabu ya kunyongwa kwa kosa la mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge, Morogoro.

Watetezi TV
Dar es Salaam
 
Sibonike

Sibonike

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2010
Messages
13,884
Points
2,000
Sibonike

Sibonike

JF-Expert Member
Joined Dec 23, 2010
13,884 2,000
Wale wafanya biashara vijana waliuwawa kinyama sana.
Ukweli hata kabla ya hapo, kuna wengi waliuwawa kwa njia hizo ili polisi wapore mali au fedha zao. Wengine walisingiziwa ujambazi.
 
thetallest

thetallest

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2017
Messages
5,838
Points
2,000
thetallest

thetallest

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2017
5,838 2,000
View attachment 1181240

Hii ni baada ya Mahakama kuifutilia mbali kesi yake ya kuomba uamuzi wa Mahakama kuu iliyomhukumu kunyongwa upitiwe upya .

Kwa faida ya wageni wa jf na wengine ni kwamba huyu Bageni ni mmoja wa washirika Abdallah Zombe kwenye Mauaji na uporaji wa mihela ya wafanyabiashara wa madini kutoka Morogoro uliotikisa nchi na kulidhalilisha jeshi la Polisi
Angekua wa chadema mngesema mahakama imemuonea kwa kua ni mwanachama wenu
 
davisoni

davisoni

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2014
Messages
361
Points
500
davisoni

davisoni

JF-Expert Member
Joined May 3, 2014
361 500
Wale wafanya biashara vijana waliuwawa kinyama sana.
Ukweli hata kabla ya hapo, kuna wengi waliuwawa kwa njia hizo ili polisi wapore mali au fedha zao. Wengine walisingiziwa ujambazi.
Kwa Sasa hali si nzuri.Binafsi ninapokuwa na hela naogopa polic wasijue Bora lijambaka lijue kuliko Hawa polic wetu(sio wote),Sasa hawachepewi kuita makamera eti 'Tumelimwagia njugu lijambaka limoja lililojaribu kupanga mkwapuo wa mavitu ya raia'
 
1

1954

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2006
Messages
6,070
Points
2,000
1

1954

JF-Expert Member
Joined Nov 14, 2006
6,070 2,000
Huyu ndata Enzi zake obay pale alikuwa mtata Kweli!
Maisha hayana formula kabisa

Ova
Maisha yana formula...nayo ni mtu unapaswa kuwa mnyenyekevu, mcha Mungu, usiye na majivuno, mpenda haki, unayechukia rushwa na maovu yote, mwenye nidhamu na usiye na chembe ya sifa ya ukatili...
 

Forum statistics

Threads 1,325,728
Members 509,278
Posts 32,201,000
Top