Christopher Bageni agonga mwamba Mahakamani, sasa anasubiri Kunyongwa tu

SSP Christopher Bageni atanyongwa hadi kufa. Ndivyo mahakama ya rufaa ilivyoamua. Maamuzi ya leo ni ya mwisho ktk mwenendo wa kesi yake. Hana pengine pa kukata rufaa, pa kukimbilia, wala pa kupinga. Mahakama imeamua anyongwe hadi afe. Jaji Stellah Mugasha amegonga nyundo. Itz over.

Hawezi kukata rufaa tena kwa sababu hukumu ya leo ni review ya hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo September 16, 2016, ambapo alihukumiwa kunyongwa hadi kufa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Benard Luanda. So hakuna mahakama ya kujadili tena shauri lake, labda Rais ampe msamaha.

Kwa wasiokumbuka Bageni alikua Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Kinondoni. Mwaka 2006 yeye na wenzie wakiongozwa na aliyekua Kaimu RPC Dar, Abdalah Zombe, walituhumiwa kupanga njama za kuwauwa wafanyabiashara watatu wa Morogoro.

Zombe anadaiwa ndiye aliyeongoza wenzie kwenye mpango huo, baada ya kujulishwa kuwa wana madini na fedha kiasi cha shilingi milioni 200.

Walikamata gari waliyokua wameikodi. Wakamuongoza dereva hadi msitu wa Mabwepande. Wakapora madini pamoja na fedha zote walizokua nazo. Kisha wakawafunga vitambaa vyeusi usoni na pingu mikononi. Kisha wakawapiga risasi za kisogoni na kuwauwa wote akiwemo dereva wa taxi waliyemkodisha.

Kesho yake Zombe akaita media na kusema wameua majambazi yaliyokua yanarushiana risasi na Polisi. Rais Kikwete akaunda tume ya Jaji Kipenka kuchunguza. Ikabainika hawakuwa majambazi. Kilichouma zaidi walikua ndugu wa familia moja. Mama mmoja alipoteza wanae watatu. Watoto wa familia 4 wakapoteza baba zao, na wake wanne wakawa wajane kwa tamaa za polisi.

Zombe alifanikiwa "kuchomoka" kwenye kesi hii baada ya kusota rumande kwa miaka kadhaa. Lakini Bageni alipatikana na hatia akahukumiwa kunyongwa. Akakata rufaa ikafeli, akaomba review ya kesi, na rulling imesomwa leo kuwa ANYONGWE HADI KUFA.

Waliomtuma hawapo nae Segerea, wala hawatanyongwa pamoja nae. Atanyongwa peke yake. Wanaohangaika nae saivi angalau kumfariji ni familia yake. Zombe hayupo, OCD wake hayupo hata IGP wa wakati huo hayupo. Ni yeye mwenyewe, na atanyongwa mwenyewe.

Hii iwe fundisho kwa wote wanaotumwa kufanya maovu leo e.g kuteka, kuua na kupoteza watu. Ipo siku utajikuta peke yako. Anayekutuma hatakuwepo. Utasimama wewe mwenyewe kutoa hesabu ya maovu yako. Kama si hapa duniani basi hata mbinguni, lakini ipo siku utalipa. Kama ambavyo wema ni mbegu, na ubaya pia ni mbegu. Humea, hukomaa, na ni lazima UVUNE.!
 
Niliwahi kuingia katika reli zake, kwa uonevu uliokithiri mwkaa 2004, nikajumlishwa na kundi la watu ambao simjui hata mmoja Kati yao, na kwa ujumla wetu tukapewa kesi ya udhururaji, hamna dhamana straight segerea,
Nikiangalia kesi anayanguruna nayo naona no bora apate majibu ya ushenzi wake hapa hapa duniani
Alikuwa na makeke sana
Alitakaga kunitingisha issue ya ndiga alikuwa anadai ya uwizi.... Kisa ilitoka dzonga plate # za Mandela....alinilaza obay siku 1 na alinambia Gari sitoipata.... Nkamwambia mm nmezaliwa ocean road nmekuliaa Kino..... Utaonaaaaa
Nlimpigiaaa ndefuuuu kwa kling@+tiba
Mwenyewe alisandaaaaa

Ova
 
Maisha hayana formula.Mungu Fundi yuko jela na aliowabambikia kesi.Sawa na Dikteta Bashiru na wapinzani wake aliowasukumixa jela.Saddam alihukumiwa kifo na jaji aliye kuwa amkitumia kuvunja haki za watu yaani maagizo toka juu kuna siku yataexpire
 
Walibambikia snaa watu Hawa

Ova
 
Alikuwa na makeke sana
Alitakaga kunitingisha issue ya ndiga alikuwa anadai ya uwizi.... Kisa ilitoka dzonga plate # za Mandela....alinilaza obay siku 1 na alinambia Gari sitoipata.... Nkamwambia mm nmezaliwa ocean road nmekuliaa Kino..... Utaonaaaaa
Nlimpigiaaa ndefuuuu kwa kling@+tiba
Mwenyewe alisandaaaaa

Ova

Ndio kawaida ya wakuja huwezi ukakuta born town yeyeto awe na nafasi au askari akawa na shobo au maringo au mnoko wengi huwa wamekuja mjini wakubwa.
 
Hivi mauaji yale yangetokea wakati wa utawala wa Rais Magufuli, je tume huru ya kuchunguza mauaji yale ya Polisi ingeundwa na Rais? Je Bageni na wenzake wangekuwa huru na kutoshtakiwa kwa lolote? Maswali ni mengi sana lakini muenendo wa nchi unavyokwenda nadhani unaweza kupata jibu kwa mbali.
 
Thubutu yake !
 
Ila jamaa walitenda unyama sana hawa. Na yule PC Saad ambaye inaaminika ndo alifyatua triger baada ya tukio akaenda Misri... Hapa namkumbuka Marehemu Koplo Lema kabla huyu Lema wa Chadema hajawa maarufu alivokiri ukweli na kuwageuka wenzie kabla hajaugua magonjwa ya ajabu na kufa...
Nakumbuka maisha ya akina Chigumbi na dereva wao wa Tax Juma Ndugu wa Manzese yalivokatishwa kule msitu wa Pande...
Nakumbuka uporaji wa fedha za roli ya Bidco ambapo polisi wale walidai kuzikomboa kumbe nao walipora wale wafanyabiashara na kuwaua kabisa... Dereva wa Bidco aliyeporwa na majambazi wenyewe hakuuawa na akakataa kuwa zile pesa si zenyewe baada ya kuoneshwa na polisi... Nakumbuka tume ya kijaji na mahakama ilipohamia msitu wa Pande kuona maisha ya wale wafanyabiashara yalipokatishwa kiss walikuwa na milioni 200....
Nakumbuka kilichomponza huyu bwana Christopher kuwa ndo alikuwa mwenye cheo kikubwa pale na angezuia mauaji PC Saad asingefyatua risasi...
Mwisho nakumbuka hotuba ya Mh. Kikwete aliposema.... "Nikasikia minong'ono kuwa Mzee, waliouawa siyo majambazi... Nikaamua kuteua tume ya Kijaji ili kujiridhisha..." Hapa hata nilikuwa sijui maana ya tume ya kijaji ni nini...
Namkumbuka PC Jane "Cynthia" ambaye alikuwa anakuwa front kupambana na majambazi kama mwanaume na anasikika kwa ujasiri akiwa ni mshitakiwa pekee kwenye ile kesi...
Nakumbuka siku ya hukumu mama wa marehemu akilia.... Sijui zile milioni 200 zilirudi....

Nimekumbuka mengi sana....
Ni mwaka huo huo akina Richmond walizaliwa...
Mkuu umeelezea vizuri na imefanya huzuni irudi upya japo wale wafanyabiashara na tax driver nilikuwa siwajui hata kwa sura. Kilichowaponza ni zile fedha. Hao polisi waliona wakiwauwa itakuwa rahisi kugawana zile fedha na watenge kidogo za kupeleka kituoni ili ionekane kama ziliokolewa fedha kidogo na nyingine zilipotea. Walijua wakipelekwa mbele ya sheria wakiwa wazima hata kama wangekuwa majambazi kweli wangeeleza fedha zimechukuliwa na polisi. Kwa kifupi zile fedha ndiyo ziliwapofusha macho wale polisi wakashindwa kujiridhisha kama kweli ni majambazi au siyo. Walifanyiwa mauaji mabaya sana.
 
Late Celina Kombani alikomalia sana hii issue otherwise ingepotezewa.......BAGENI anyongwe tu na pia namuomba Mwanaharakati "HURU" akakate rufaa dhidi ya ZOMBE kuachiwa huru,inabidi Zombe na Yeye aning'inizwe KITANZI.
Mkuu Zombe siyo rahisi kukutwa na kosa. Kinachomuokoa zaidi ni yeye kutokuwepo kwenye sehemu ya tukio. Hata kama aliwapa amri baada ya mambo kubuma hawezi kukubali kuwa aliwaambia. Ndiyo maana bianadamu inatakiwa tutumie akili na haki hata tunapokuwa kwenye shinikizo.
 
Inauma sana kuona kesi ya wazi kabisa inachukua miaka zaidi ya 15 huku baadhi ya wahusika wakiwa mtaani wakijsifu

Mh waziri husika saidia hili waliohusika na hayamauwaji wote waunganishwe na bageni na haki itendeke

Na yulemama anaetunza wajane nae asaidiwe ikiwezekana wahuiska wauziwe malizao mama apewe zile milion kadhaa za mwanae atunze wajukuu

Mungu azidi kukutangulia kwa hili hii kesi mwanangu alikuwa anazaliwa mpaka leo hii yuko form two bado inaendelea na wahusika walijulikana inaumiza sana
kesi iliisha siku nyingi mazee. Hizi ni rufaa za huyo aliyekutwa na hatia.
 
Alikuwa na makeke sana
Alitakaga kunitingisha issue ya ndiga alikuwa anadai ya uwizi.... Kisa ilitoka dzonga plate # za Mandela....alinilaza obay siku 1 na alinambia Gari sitoipata.... Nkamwambia mm nmezaliwa ocean road nmekuliaa Kino..... Utaonaaaaa
Nlimpigiaaa ndefuuuu kwa kling@+tiba
Mwenyewe alisandaaaaa

Ova
Nauliza swali japo najua wewe si mhusika na unaweza usiwe na jibu. Hivi ni nani aliyemtorosha yule polisi aliyefyatua risasi ambaye ndiye kimsingi aliwauwa? Ni yeye alitoroka mwenyewe au kuna watu wako nyuma yake? Je hivi kweli serikali haijui aliko? Kuna juhudi zozote za kumtafuta kutoka kwa serikali? Laiti nchi yetu ingekuwa na waandishi wa habari wa ukweli wangechunguza mpaka wangejua alipo.
 
Swali zuri sana

Ova
 
Back
Top Bottom