Christmas ya mwisho kuelekea 2020 oktoba ndio mbaya zaidi

cutelove

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
3,317
7,509
Kuelekea 2020 hizi sikukuu ndio mbaya kuwahi kutokea

Biashara haziendi, wanunuzi wananunua kiduchu

Zile amsha amsha za sikukuu mtaani hakuna, halafu watu hawana sura ya tabasamu,watu wamejikunyata, nadhani wale watafiti wa viwango vya furaha wakija sasa hivi sijui tunakuwa namba ngapi? Sokoni wanapigwa na butwaa nini hiki,mzee wa kitambi anakuja kwako unafikiri hapa biashara itasogezwa angalau, loh anachanga kilo 4 za mchele anasepa

Naamini kiongozi atakayekuja wa upinzani akawa na sera za kiuchumi imara zinazoiponda za Magufuli, ataweza kutikisa nchi

Upinzani jiandaeni kuchukua nchi,hali si shwari kwa wananchi, uchumi unaendeshwa kwa matamko ya kisiasa hali ni mbaya kutokea

Ukiwa na nyumba yenye kila kitu halafu unalala njaa, hiyo nyumba haina faida kwako, bora ungelala kwenye gofu angalau ushibe ili upate nguvu ya uzalishaji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi mtu kununua kilo nne kunathibitishaje kuwa hana fedha ya kumkizi sikukuu..? Kwani unaifahamu familia yake..?, mipango yake je..? Kwani lazima kila sikukuu mtu ale pilau..?
 
Hivi mtu kununua kilo nne kunathibitishaje kuwa hana fedha ya kumkizi sikukuu..? Kwani unaifahamu familia yake..?, mipango yake je..? Kwani lazima kila sikukuu mtu ale pilau..?
Acha kujitoa ufahamu kama hujui kinachoendelea mtaani. Kuna watu ugali ambao ulishaonekana ni chakula cha kimasikini wanashindwa kabisa kununua unga. Upatikanaji wa pesa umekuwa mgumu sana,na ukiipata haina thamani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom