Chopa 3 = visima vya maji vingapi?

Chopa 3 = visima vya maji vingapi?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
16,252
Reaction score
16,171
Badala ya kununua au kukodi chopa za kufanyia kampeni fanyeni kampeni kwa kutatua kero za wananchi (maji, madawati, umaskini, n.k) matunda yataonekana. Wanachi washajua kuwa mbunge mmoja wa upinzani hawezi kuleta kisima hata kimoja kwanini wapoteze kura zao?
 
unataka kutukanwa wewe..hawa pendi ushauri hawa wanajua kila kitu,kwanza wanasema hiyo ni kazi ya serikali wao kazi yao ni porojo za majukwaani na kuorodhesha matatizo ya nchi bila kuonyesha utatuzi
 
Naomba unitajie eneo mojawapo ambalo CCM wamechimba Kisima/Visima au kujenga Barabara kwa kutumia fedha za CCM, Ukiishanipatia hili jibu naomba unifafanulie zile 90,000,000/= Mwigulu alizochukua Bank siku moja kabla ya Uchaguzi zimeenda Kalenga kuchimba visima vingapi?
 
Hoja ya kizamani hiyo tunachangia sherehe,michezo,sadaka nk wakati maisha yetu ni yakawaida kabisa.everything at a time
 
Ulishawahi kujiuliza ndege ya raisi ni visima vingapi?
Ulishawahi pia kujiuliza yale magari ya mawaziri ya almost milioni mia mbili kila moja, na yale magari ya wabunge ni visima vingapi?
Au wewe hayo macho yako ya "makengeza" yanaona chopa zaCDM tu, ndio zichimbe visima!?, CDM ambao hata hivyo hawachukui kodi kwa wananchi!?
 
unataka kutukanwa wewe..hawa pendi ushauri hawa wanajua kila kitu,kwanza wanasema hiyo ni kazi ya serikali wao kazi yao ni porojo za majukwaani na kuorodhesha matatizo ya nchi bila kuonyesha utatuzi
Kwa hiyo wewe unajua hizo kazi kama za kuchimba visima ni za wapinzani?, kwa pesa ipi, ya ruzuku!?
CCM walishawahi kuchimba kisima kwa pesa za chama??, inaonyesha wewe aidha ni mpotoshaji tu ama ni mbumbumbu wa kutupwa!!!
 
Eh mara tu mmesahau wafadhili waliotoa pesa kwa ajili ya visima? Ama mgawo umekupitia
 
Kwa hiyo wewe unajua hizo kazi kama za kuchimba visima ni za wapinzani?, kwa pesa ipi, ya ruzuku!?
CCM walishawahi kuchimba kisima kwa pesa za chama??, inaonyesha wewe aidha ni mpotoshaji tu ama ni mbumbumbu wa kutupwa!!!

mimi ni mbumbumbu kabisa nimekubali,lakini wewe ndugu yangu ni hayawani nambari moja kwasababu mwalimu wakipindi hajaingia darasani eti na wewe ndo husomi kabisaaa,mpaka aje akufundishe..ikiwa yanayo ongowea jukwaani kwa uchungu hadi kutamani kulia angalau yangefanyika walau hata kwaudogo fulani nadhani yangeweza badili muonekano wa chama chako kwasasa..lakini kwakuwa nigenge la matapeli hili nieneo lao la ujangili hawana budi kuwa kama waigizaji

"analyze your performance in a box score,to demand change "
 
Badala ya kununua au kukodi chopa za kufanyia kampeni fanyeni kampeni kwa kutatua kero za wananchi (maji, madawati, umaskini, n.k) matunda yataonekana. Wanachi washajua kuwa mbunge mmoja wa upinzani hawezi kuleta kisima hata kimoja kwanini wapoteze kura zao?

CCM imekusanya kodi kwa miaka 50.Wamefanya nini?Sisi tunawaonyesha watawala na watanzania kile ambacho tutafanya jinsi ambavyo Mwalimu Nyerere na TANU alivyofanya dhidi ya serikali ya kikoloni
 
Naomba unitajie eneo mojawapo ambalo CCM wamechimba Kisima/Visima au kujenga Barabara kwa kutumia fedha za CCM, Ukiishanipatia hili jibu naomba unifafanulie zile 90,000,000/= Mwigulu alizochukua Bank siku moja kabla ya Uchaguzi zimeenda Kalenga kuchimba visima vingapi?

Safi sanaaaaaa good question
 
Badala ya kununua au kukodi chopa za kufanyia kampeni fanyeni kampeni kwa kutatua kero za wananchi (maji, madawati, umaskini, n.k) matunda yataonekana. Wanachi washajua kuwa mbunge mmoja wa upinzani hawezi kuleta kisima hata kimoja kwanini wapoteze kura zao?
wenzio wako buze na mkakati wa kuongeza ruzuku kwa kuongeza wabunge. suala la maendeleo kwao ni kibwagizo tu.
 
Badala ya kununua au kukodi chopa za kufanyia kampeni fanyeni kampeni kwa kutatua kero za wananchi (maji, madawati, umaskini, n.k) matunda yataonekana. Wanachi washajua kuwa mbunge mmoja wa upinzani hawezi kuleta kisima hata kimoja kwanini wapoteze kura zao?
Salute kwako Kavulata
 
unataka kutukanwa wewe..hawa pendi ushauri hawa wanajua kila kitu,kwanza wanasema hiyo ni kazi ya serikali wao kazi yao ni porojo za majukwaani na kuorodhesha matatizo ya nchi bila kuonyesha utatuzi

Hana hata haja ya kutukanwa, mawazo yake tu na yako ni dhalili tosha, yaani mnajitukan wenyewe.

Km unajua kazi ya upinzani ni kuonesha njia ya utatuzi, unadhani kujenga kisima ni kuonesha au kutatua?

Shida ya watu mlio wengi ni umbumbumbu, mbunge si kazi yake kutumia mshahara wake au fedha za chama chake kujenga kisima, ni fedha za serikali ndio zenye kazi hiyo, akiamua yeye basi katoa msaada.

Kwa akili fupi km zenu, mnadhani barabara hizi zikejengwa na fedha za CCM, si hivyo ni za Tanzania
 
Naomba unitajie eneo mojawapo ambalo CCM wamechimba Kisima/Visima au kujenga Barabara kwa kutumia fedha za CCM, Ukiishanipatia hili jibu naomba unifafanulie zile 90,000,000/= Mwigulu alizochukua Bank siku moja kabla ya Uchaguzi zimeenda Kalenga kuchimba visima vingapi?

mkuu hebu tuambie hizo halmashauri zinazoongozwa na CDM nini wamefanya tofauti na serikali ya CCM?
 
Ulishawahi kujiuliza ndege ya raisi ni visima vingapi?
Ulishawahi pia kujiuliza yale magari ya mawaziri ya almost milioni mia mbili kila moja, na yale magari ya wabunge ni visima vingapi?
Au wewe hayo macho yako ya "makengeza" yanaona chopa zaCDM tu, ndio zichimbe visima!?, CDM ambao hata hivyo hawachukui kodi kwa wananchi!?
mkuu hizo ruzuku za zaidi ya mil 200 ni kodi za kina nani?
 
Badala ya kununua au kukodi chopa za kufanyia kampeni fanyeni kampeni kwa kutatua kero za wananchi (maji, madawati, umaskini, n.k) matunda yataonekana. Wanachi washajua kuwa mbunge mmoja wa upinzani hawezi kuleta kisima hata kimoja kwanini wapoteze kura zao?
acha maneno ndg yangu, kampeni meneja kawapoteza
 
Back
Top Bottom